Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!


Ingizo Jipya Money Flower..

Izi Episode Mbili Nilizoangalia Hii Drama Nayo Ni Motoo,Daebak!!

Wale Wapenzi Wa Kicheko Kazi Yake Mpya Iyo...Imeanza Vizuri Ata Ratings Zake Ziko Juu....
 

Ingizo Jipya Money Flower..

Izi Episode Mbili Nilizoangalia Hii Drama Nayo Ni Motoo,Daebak!!

Wale Wapenzi Wa Kicheko Kazi Yake Mpya Iyo...Imeanza Vizuri Ata Ratings Zake Ziko Juu....
Ep ya 2 ilipoisha ilinibidi nianze tena ep 1. (Sinaga hiyo tabia ya kurudia episode)
Hahahaha. Huo kweli motoo!
 
Ep ya 2 ilipoisha ilinibidi nianze tena ep 1. (Sinaga hiyo tabia ya kurudia episode)
Hahahaha. Huo kweli motoo!
Bonge Moja La Drama Nimepanda Akili Zake Jinsi Zinavyotumika Umu Ndani Yuko Simple Sana Ila Anayoyafanya Ni Makubwa...Iko Poa Sana...
 
Hawa watu nawaelewa mno Aisee. Hasa huyo jamaa ananifurahisha anavyo kuwa anajiongelesha Sijuhi Human Kitu gan utafikiri yy sio Hahahahahaaaaa. Ila jamaa yuko poa sana yaani anavyo jiongelesha ndio mm nimependa kwake na kule kuvunga yuko serious Kumbe utumbo tu. Kuna yule polisi kila jamaa akiingia chooni anamkuta Hahahahahaaaaa huyo nae ni kituko. Penda sana hili picha Aisee.
 
Nimependa tabasamu zao.

Mkuu,
Hilo vazi la Noona vipi? Au ndio msimu wa baridi?
 
  1. umefanya kosa kubwa sana na malaika ameshakuandikia dhambi kwa kitendo chako cha kumwita king gwaggaeto na ili dhambi yako ifutwe unapswa ukasujudie ukuta wa gwaggaeto stele. ulipaswa uanze na The great king gwaggaeto a.k.a taewang gwaggaeto, a.k.a go damdeok, a.k.a Broad Expander of Domain, a.k.a peace maker,mwanadamu aliyerudisha heshima ya goguryeo kwa kuwafunza adabu mataifa kama baekje, shilla, japan,khitan,china na maeneo ya urusi na bahati mbaya sana alikufa akiwa na pungufu ya miaka miwili kufikia miaka 40 na laiti kama angeliishi miaka 20 zaidi naamini kwa kutumia jambia lake angelifika hadi nyanda za juu kusini alikotokea babu yake Khantwe.
  2. ni wafalme wawili tu ndio waliopewa heshima ya the great katika eneo la korea na mwengine ni the great king sejong ambaye alikuwa ni mfalme wa nne wa joseon. mnamo mwaka 396 mfalme gwaggaeto aliuteka mji mkuu wa taifa la baekje ambao uliitwa Wiryeseong ambapo kwa sasa ndio panaitwa Seoul ambao ndio mji mkuu wa korea kusini. wakati anaipiga baekje alikuwa na miaka 25 tu.
  3. mnamo mwaka 399 aliongoza kikosi cha wanajeshi 50000 na kuelekea taifa la Silla na aliwasambaratisha wajapan waliokuwa wanaleta fujo nchini shilla, baada ya hapo wajapan na shilla wakaamua kujisalimisha kwa goguryeo.
  4. baadae akawatwanga wachina wa Xianbei na akarudisha eneo la liaodong ambalo kabla ya kuanzishwa kwa goguryeo ilikuwa ni eneo la gojoseon kabla taifa hili halijaangamiza na china (han dynasty)
  5. mnamo mwaka 371 ambapo ilikuwa ni miaka 3 kabla hajazaliwa go damdeok taifa la goguryeo lilipoteza nguvu yake ya kiutawala kwa ndugu zao ambao ni baekje chini ya mfalme wao aliyejulikana kwa jina la geunchogo ambaye ndiye mwanadamu aliyeifanya baekje kuwa ni taifa tishio.mfalme geunchogo alimuua mfalme gogukwon wa goguryeo na kuuteka mji wa pyongyang ambao kwa sasa ndio mji mkuu wa korea kaskazini. mfalme gogukwon ndie mfalme pekee kwenye nchi ya goguryeo kufia vitani na alirithiwa na mwanawe aliyeitwa go gubu (king sosurim).
  6. mfalme sosurim alikufa bila ya kuwa na mtoto ndipo akatawala mdogo wake aliyeitwa go iryeon ambaye ndiye baba wa go damdeok (gwaggaeto)
  7. muigizaji Lee tae gon ndiye aliyeigiza nafasi ya damdeok kwenye drama ya king gwaggaeto lakini umenikera mjr95 uliposema jamaa anamzidi song il kook. Ili amzidi song il kook anapaswa kwanza amzidi choi soo jong na jang hyuk
  8. link ya king geunchogo drama https://ondramanice.io/drama/king-geunchogo-detail
 
Money flower drama nimeshindwa kuangalia episode ya 1 hivyo basi naomba EMPTY dongsaeng na aminas noona munirekebishe pindi nitakapokosea.
  • nimeangalia episode ya 2 na kwa jinsi inavyoonekana kang pil joo (jang hyuk) ana uhusiano wa damu na hii familia ya mzee jang kook hwan na ameamua kufanya kazi kwenye kampuni ya mzee jang kook hwan ili alipe kisasi.
  • kwa jinsi inavyoonekana yule mzee mgonjwa aliyemtembelea gerezani hakuwa baba yake mzazi, sijajua mpaka sasa sababu iliyopelekea kang pil joo kufungwa jela kama nilivyosema hapo juu episode ya 1 sijaiangalia.
  • kang pil joo na jang bo cheon kivyovyote watakuwa wana udugu kwa sababu kang pil joo nae ni mjukuu wa jang kook hwan, sasa balaa ni kwamba wote watampenda mwanamke mmoja anayeitwa na mo hyun japo kuwa kang pil joo anataka kumtumia na mo hyun aolewe na jang boo cheo ili alipe kisasi.
  • kang pil joo,mama yake na mdogo wake walifanyiwa maujanja na wakajikuta wakipelekwa kwenye ziwa na kuzamishwa.ameamua kujifanya kama ni puppetdog wa mama yake jang boo cheon ili kutimiza lengo lake alilojiwekea.
  • kwa mujibu wa stori inasemekana jang boo cheon na na mo hyun watafunga ndoa na watapata mtoto.
  • kang pil joo alikutana kwa mara ya kwanza na mwanadada na mo hyun kwenye maji wakati kang pil joo anaokolewa.mwanzo alikuwa anatumia jina la jo in ho na hata kile kitabu alichokipost kwenye mtandao amekiandika jina hilo, kang pil joo anamfahamu na mo hyun lakini na moo hyun hamfahamu kang pil joo kwa sababu amebadilisha jina.
  • scalethat rais wako amerudi tena
  • M.C THE MAX ni miongoni mwa bendi za muziki za korea ninayoipenda sana, ost 1 ameimba lee soo.
 
tokea nianze kufuatilia korean drama haijawahi kutokezea kuangalia zaidi ya drama 3 kwa wakati mmoja lakini wakati huu nimepitiliza.naomba muniombee na mimi kama munavyomuombea mzaliwa wa chato.
  • black drama - song seung hun
  • joseon gun man drama - lee joon gi
  • kings dream drama - choi soo jong
  • goblin drama - gong yoo
  • because this is my first life - lee min ki
  • money flower - jang hyuk
  • romantic doctor teacher kim - yoo yeon seok
  • witch court - jung ryeo won
  • temperature of love drama - yang se jong
  • rebel thief who stole the people drama - yoon gyun sang
 
kweli mungu ndiye mpangaji wa yote kwa sababu nimekuwa nikijiuliza
je song joong ki na song hye kyo uhusiano wao ungelikuwa maarufu duniani kama ingelitokezea kati ya gong yoo, kim woo bin, jo in sung na hyun bin mmoja wao angelikubali offer ya kuwa muigizaji mkuu wa descendent of the sun?
 
Director John Woo kutoka Hong Kong amewapa zawadi ya bracelet iliotengenezwa kwa madini ya dhahabu wanadoa song joong ki na song hye kyo kama ni zawadi ya ndoa.

 
kituo kimoja cha habari cha china wameweka hadharani kiapo au ahadi iliotolewa na song joong gi kwa mke waka mpendwa song hye kyo siku ya ndoa yao.
song joong ki alianza kwa kusema
Kama mume wa song Hye Kyo nina ahidi,
Tumeamua kutembea njia hii ambayo watu wengi mbele yetu wamechagua kutembea kabla yetu,kutakuwa na mvua kubwa sana, upepo mkali sana na tutakutana na vikwazo vikubwa sana lakini naahidi licha ya vikwazo tutakavyokutana navyo tutaendelea kushikana mikono kwa pamoja na kuvishinda vikwazo vyote.
baadae tutatabasamu kwa pamoja na kusema its nothing na kisha tutajifunza kutembea tena tukiwa imara kwa ujasiri na bidii zaidi
wangu mpendwa song hye kyo

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…