DAEMUSHIN
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,428
- 120,464
naamini Khantwe noona maswali yako utakuwa umeshapata majawabu kwa sababu naamini utakuwa ushamaliza kuiangalia while you were sleeping ila si vibaya na mimi nikaweka mawazo yangu kama ulivyoniomba siku ya tarehe 21/10/2017.Damushin sunbae nisaidie kuunganisha dots kabla hunaondoka (while yo were sleeping)
1.Han woo Tak ni nani? Mbona uwepo wake siuelewi hata
2. Kuna siri gani kubwa inayomhusu? Nakumbuka yule rafiki yake alimwambia asipomuokoa na ile kesi atatoa siri
3. Yule kaka wa muuaji wa baba wa Hong Joo na mwenzie yuko wapi?
4. Yule mtuhumiwa wa mauaji ni nani mbona kama anafanana na yule mwanajeshi?
5. Mbona lawyer Lee anatumia nguvu kubwa kumkandamiza yule mtuhumiwa. Mimi nahisi yeye ndo anahusika kwa namna moja au nyingine na mauaji ya yule dada maana alipaniki sana aliposikia mtuhumiwa ameachiwa huru
- han woo tak ni askari ambaye naye pia ana uwezo wa kuona matukio yatakayotokezea mbeleni kwa kuota ndoto.
- siri kubwa aliyokuwa nayo ni kwamba ana tatizo la color blindness, kiufupi anashindwa kutofautisha rangi na jambo hili alilificha wakati anafanya vipimo kwa ajili ya kuwa askari na kisheria inavyoonekana kama una tatizo la color blindness hupaswi kuwa askari.kuna episode moja nakumbuka nam hong joo alisahau power bank yake kwenye gari la wootak na ilikuwa ina rangi kijani lakini cha kushangaza woo tak anasema power bank ilikuwa ni rangi nyekundu. hata siku waliomfukuza yule kijana aliyeitupa simu kwenye maji alishindwa kutofautisha rangi ya flana aliovaa mtuhumiwa ambayo ilikuwa ni gray,na ndio maana baada ya kesi kuisha aliamua kuacha kazi.
- yule kaka wa muuaji aliyemuua baba yake hong joo na jae chan ndiye Mr choi dam dong, aliamua kuachana na kazi ya polisi na kuamua kufanya kazi kitengo cha sheria kinachohusika na masuala ya uhalifu.
- yule mtuhumiwa wa mauaji ya mwanadada ambaye ni bingwa wa kurusha mishale ni rafiki na woo tak tokea shuleni, wala si yeye aliyemuua marehemu ila marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa ambao ulikuwa unamsababisha kuanguka na kupoteza fahamu.mwanasheria lee yeo beom alipaniki kwa sababu tayari alikwisha tia fitina kwa baba wa yule mwanamke ndio maana yule baba baada ya mtuhumiwa kuachiwa kwa hasira aliamua kumtwanga panda ya mzungu (risasi) wakili jae chan.