Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hongera Oppa,..Uendeleee Kuwepo Daima InshaAllah
[HASHTAG]#KOREANDRAMAFEVER[/HASHTAG] Miaka Yote InshaAllah
 
nikimnukuu dk shika itapendeza zaidi kama ungelitaja drama zote ulizoziangalia zenye maudhui ya action ili iwe rahisi kuzitafuta na nyengine.
  1. https://ondramanice.io/drama/healer-detail
  2. https://ondramanice.io/drama/iris-detail
  3. https://ondramanice.io/drama/iris-2-detail
  4. https://ondramanice.io/drama/athena-goddess-of-war-detail
  5. https://ondramanice.io/drama/two-cops-detail : hii inaendelea
  6. https://ondramanice.io/drama/heartless-city-detail
  7. https://ondramanice.io/drama/bad-guys-detail : anza na hii kupitia (OCN)
  8. https://ondramanice.io/drama/bad-guys-age-of-evil-detail: season 2 imeanza jana kupitia (OCN). nimeangalia comment za mashabiki wanasema ni mwendo wa mapigano mpaka wakati wa ibada.
  9. https://ondramanice.io/drama/the-k2-detail
  10. https://ondramanice.io/drama/tunnel-korean-drama-detail (OCN)
  11. https://ondramanice.io/drama/signal-korean-drama--detail (OCN)
  12. https://ondramanice.io/drama/voice-korean-drama-detail (OCN)
  13. https://ondramanice.io/drama/secret-forest-detail :seoul best drama 2017. aigooooooo naomba uniagizie Bibimbap (Mixed Rice) na kinywaji cha Bokbunja ju ili nikumalizie
 

Attachments

  • upload_2017-12-17_13-21-12.jpeg
    9.2 KB · Views: 40
hahahaaaaaa kuna waigizaji wa kiume hata kama binti ni kilaza basi atang'arishwa akitaka asitake,hivyo hivyo kwa muigizaji kilaza wa kiume akikutana na muigizaji hodari wa kike naye atang'arishwa akipenda asipende.
Akipenda mungu wiki hii nitaitafuta doctors ili nimuangalie yeye tu na si park shin hye japo kuwa si mpenzi mkubwa sana wa medical drama.
https://ondramanice.io/drama/doctors-detail
basi siku moja nilitembelea forum soompi special thread ya kingdom of the wind ili nijifunze masuala mbali mbali kuhusiana na production ya drama ile, asilimia kubwa ya mashabiki walikuwa wanamponda sana mwanadada choi jung won, wengi wao walikuwa wanamuona uwezo wake ni mdogo kusimama pamoja na king of historical drama( song il kook/guk). mwisho wa siku kwenye KBS drama awards za mwaka 2008 alipata tunzo tatu ikiwemo ya best actress. mashabiki wengi hawakufurahishwa kwani wengi waliamini sung yuri aliyeigiza hong gil dong ndiye anastahili tunzo ya best actress.
lakini nilipenda style yake ya kuvaa magauni mawili kwa usiku mmoja,hahahahaaaaahaaaaaaa alikuwa anaingia na kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kama waimbaji wanapofanya matamsha.


mimi naamini song joong ki amen'garishwa na song hye kyo kwenye descendent of the sun drama.nitaendelea kuamini hata kama stering angelikuwa kim woo bin basi mwanadada song hye kyo angelimfanya aonekane ni bora.
 
Pole Sana Sana,Aigooooo Usijari Tuaze zichanga Zengine Za Seung Ji Na Chang Wook Ata Rae won Pia.
labda kim rae won kwa sababu anaelekea miaka 37 lakini hao wengine bado kabisa kwenye suala la ndoa.
ni sisi tu waswahili na waarabu ndie tuna mawazo ya kuoa mapema eti ili tupate watoto mapema pindi tutakapozeeka waje watusaidie, utagundua asili ya maisha yetu mpaka tunakufa ni watu wa kutegemeana.
kwangu mimi kiupande fulani naona ni utamaduni mzuri na pia kiupande mwengine ni utamaduni wa kijinga.
 
hapo ndio unakata mzizi wote wa mawasiliano ya mchepuko wake kwa sababu.
  1. kama mtoto ataendelea kuishi kwa mama yake mzazi tafsiri yake ni kwamba mwanaume ataendelea kwenda kwa mchepuko wake kwa kutumia kisingizio cha kupeleka huduma za mtoto na mama jambo ambalo litaibua tena hisia za kimapenzi za wawili hao.
  2. lakini kama ulivyosema inataka moyo sana hususani huko kwenu bara ndio kunaongoza matukio ya ajabu ya kuwadhuru watoto wa kambo.hahahahaaaa siku moja nilisikia taarifa mwanamama kamchoma moto mtoto kwa kumuibia shilingi 500, ni ukatili usiovumilika.
  3. ni sawa sawa na zari amlee mtoto wa hamisa mobeto........ daebak..... daebak...... daebak.
  4. lakini kama mwanamme ataendelea na tabia yake basi njia halali unayopaswa kuifuata ni kuachana naye kwa amani.
 
Hahahahhahah!!! Utamaduni Siyo..

Kuzaa Mapema Damushin kuna Umuhimu Wake Basi Tuuh Tunaenda tofauti Sababu Ya Aya Maendeleo ya Tecnologia..
Duuh 37 Bado Ajaoa Lol!!!!
 
Iyo Namba 13 drma nilianzaga Vizuri ila Sijuh kilinikuta Nini Nikaiachia Katiii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…