kiukweli tokea saa 10 nipo kwenye thread hii nafuatilia update kuhusiana na MBC drama awards, hongera kwako
aminas noona kwa kutuhabarisha taarifa muhimu ambazo zinamhusu kila mpenzi wa korean drama, mungu akujaalie mwaka 2018 uwe na baraka zaidi kwako kuliko mwaka 2017.
pia nikuombe radhi kwa kupuuzia wito wako na kama sikosei umeniita mara tatu na katikati ya wiki pia niliona alert yako ila nimejifanya kama sijaziona alerts zako,
chingus baadhi ya nyakati inabidi tuvumiliane tu huwa inafika wakati huwa sina mzuka kabisa wa kuandika chochote na matokeo yake huishia kusoma comment zenu na kuishia kucheka peke yangu.
omo omo omo
EMPTY dongsaeng heshima kwako kwa kuamua kutumia muda wako kumpa sapoti noona naamini uwepo wako umempa hamasa na morali kubwa sana leo hii.
kwa kauli ya dk shika noona ingependeza zaidi kama ungeliweka na picha ya kila mshindi wa tunzo ila si mbaya umenifanya kila wakati nipitie google niweze kujua picha za baadhi ya waigizaji washindi.
hongera kwake mzee
kim sang joon kiukweli amestahili tunzo ya grand prize, nilipokuwa naangalia city hunter nilimchukia sana huyu mzee kutokana na nafasi aliyoigiza na nilimuona ni muigizaji wa kawaida tu kumbe nilikuwa mjinga niliyevuka mipaka.
ila baadae nikapata nafasi ya kuangalia historical drama inayoitwa
the jing birok: the memoir of imjin war ambapo alicheza nafasi ya waziri wa ulinzi akijulikana kwa jina la ryu seung ryong na alikuwa muigizaji mkuu, alinifuta ujinga na kunifanya kuwa mwerevu baada ya episode 50.
kitendo cha kutangazwa kuwa ni mshindi muda huu kimenifanya nikirudie kiporo changu cha rebel thief who stole the people japo episode mbili ambayo niliiacha episode ya 8.