Damushin Sunbae na
EMPTY Sunbae mkuje huku kuna jambo nimegundua kwenye hizi Drama zetu za Historical. Je, umewahi fikiria ni kipi hufanyika katika kuwafanya baadhi ya wahusika katika historical drama waonekane wadogo? Hii kitu nimeifikilia sana bila ya kupata majibu kabisa na bado inanisumbua kichwa. Je, ni nn hutumika kuwafanya waonekane namna hiyo? Nitachukulia mifano michache hapa chini katika Drama zilizo niacha hoi kabisa.
Katika Drama ya The Kingdom of the wind muhusika Song il Gook aliye cheza kama Muhyul alinipa wakati mgumu sana mpaka kuja kutambua kuwa ni Song il Gook mwenyewe. Nilifahamu kuwa ni yy baada ya yeye kuota ndevu ndio nikatambua kuwa mbona huyu nilimuona kwenye Drama pendwa kabisa ya Jumong. Hahaha ilinichukua mda sana kumwelewa Mshikaji wangu Song il Gook.
Katika Drama niliyo nayo kwa sasa The Immortal Yi Soon Shin kuna vichwa viwili vimenipa wakati mgumu mpaka kuamini kuwa ni wenyewe Hahaha. Muhusika wa kwanza ni huyu wanamuita Kim Myoung Min huyu brother nilimtambua mara moja pale nilipo muona kwenye episode ya kwanza tu. Huyu nilimtambua kwamba niliwahi muona kwenye Drama ya Six Flying Dragons aliye cheza kwa jina la Teacher Sambog hakunipa wasiwasi kabisa katika episodes za mwanzo. Mtihani ulikuja katika episodes za mbele zilipo anza elezea maisha yake. Sikutaka kuamini kabisa kwamba huyu ndio nilie muona katika episodes za mwanzo na katika Drama ya Six Flying Dragons. Yaani akawa mdogo alafu akawa sie mtu yule mwenye mienendo ya episodes za mwanzo. Mpaka sasa siamini kama ni yeye, hahaha huenda nikaamin kwa mbeleni.
Aliye nishangaza zaidi ni Kim Kyu Chul.
Hahaha sasa huyu ndio alikuwa komesha kabisa, huyu ni yule rafiki yake Yi Soon Shin kipindi yupo Ahsan. Katika Drama hiyo ametumia jina la Chun Su, huyu nimekuja kutambua kuwa ni Kim Kyu Chul katika episode ya 18 tena baada ya Baron Huh kumpa cheo cha Supervisor. Bila ya cheo hicho sidhani kama ningemtambua kwa kweli. Bwana huyu niliwahi muona katika Drama ya The Great King Gwanggaeto akiwa pamoja na kikosi chake (jina nimesahau) mambo aliyo fanya mule na aliyo fanya katika Drama ya The Immortal Yi Soon Shin yalinifanya nisiamini kabisa kwamba ni yeye. Kawa mdogo alafu matendo yake sasa Hahaha
Aiseee huyu mtu matendo yake ni kichekesho tosha na yalinifanya nisiamini kuwa ni yeye Kim Kyu Chul.
Ila Jamaa anakipaji sana
Damushin na
EMPTY hilo mmegundua lakin? Kaishi na Yi Soon Shin kwa upendo na furaha kabla ya kutengana nae baada ya kusemekana eti Yi Soon Shin alimchomesha kumbe sio. Basi toka kipindi hicho akawa na chuki juu yake, kitendo hicho kinanirudisha mpaka katika Drama ya The Great King Gwanggaeto nakumbuka aliwahi fanya kitendo kama hicho. Jamaa aliishi vizuri na Damdeok kipindi wamekamatwa lakini wakaja kuwa maadui tena akiapiza kurudisha kisasi kwa Damdeok. Ila kwa baadae walipatana tena hahaha ndio raha ya kutizama Korea Drama tena ziwe historical. Nimependa sana jinsi Jamaa anavyo badilika yuko vizuri sana kipaji anacho kwakwel. Nacheka sana na Kufurahi pindi nikikumbuka maisha aliyo ishi na rafiki yake Yi Soon Shin na maisha baada ya kupewa Cheo cha Supervisor. Huyu Jamaa ni kituko
mjr95.