Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

h4hTWui.png

OpGkHyl.png

Radio Romance,.

Okay Okay.. Si Mbayaa Ila Ni Stori Itayokufanya Uiangalie Tena Ndo Kwanza Episode 2, Imeanza Juzi
Mi Nimempenda Uyo Mkaka Tu Kama Kawaida.
 
Damushin Sunbae na EMPTY Sunbae mkuje huku kuna jambo nimegundua kwenye hizi Drama zetu za Historical. Je, umewahi fikiria ni kipi hufanyika katika kuwafanya baadhi ya wahusika katika historical drama waonekane wadogo? Hii kitu nimeifikilia sana bila ya kupata majibu kabisa na bado inanisumbua kichwa. Je, ni nn hutumika kuwafanya waonekane namna hiyo? Nitachukulia mifano michache hapa chini katika Drama zilizo niacha hoi kabisa.

Katika Drama ya The Kingdom of the wind muhusika Song il Gook aliye cheza kama Muhyul alinipa wakati mgumu sana mpaka kuja kutambua kuwa ni Song il Gook mwenyewe. Nilifahamu kuwa ni yy baada ya yeye kuota ndevu ndio nikatambua kuwa mbona huyu nilimuona kwenye Drama pendwa kabisa ya Jumong. Hahaha ilinichukua mda sana kumwelewa Mshikaji wangu Song il Gook.
3fc74cbd2a984b3a749139f6fcd516ad.jpg

Katika Drama niliyo nayo kwa sasa The Immortal Yi Soon Shin kuna vichwa viwili vimenipa wakati mgumu mpaka kuamini kuwa ni wenyewe Hahaha. Muhusika wa kwanza ni huyu wanamuita Kim Myoung Min huyu brother nilimtambua mara moja pale nilipo muona kwenye episode ya kwanza tu. Huyu nilimtambua kwamba niliwahi muona kwenye Drama ya Six Flying Dragons aliye cheza kwa jina la Teacher Sambog hakunipa wasiwasi kabisa katika episodes za mwanzo. Mtihani ulikuja katika episodes za mbele zilipo anza elezea maisha yake. Sikutaka kuamini kabisa kwamba huyu ndio nilie muona katika episodes za mwanzo na katika Drama ya Six Flying Dragons. Yaani akawa mdogo alafu akawa sie mtu yule mwenye mienendo ya episodes za mwanzo. Mpaka sasa siamini kama ni yeye, hahaha huenda nikaamin kwa mbeleni.
16cd26c52bda9e74b7c7d81e421905ec.jpg

Aliye nishangaza zaidi ni Kim Kyu Chul.
223e94edef2e6d33f9966b535919cbf5.jpg
Hahaha sasa huyu ndio alikuwa komesha kabisa, huyu ni yule rafiki yake Yi Soon Shin kipindi yupo Ahsan. Katika Drama hiyo ametumia jina la Chun Su, huyu nimekuja kutambua kuwa ni Kim Kyu Chul katika episode ya 18 tena baada ya Baron Huh kumpa cheo cha Supervisor. Bila ya cheo hicho sidhani kama ningemtambua kwa kweli. Bwana huyu niliwahi muona katika Drama ya The Great King Gwanggaeto akiwa pamoja na kikosi chake (jina nimesahau) mambo aliyo fanya mule na aliyo fanya katika Drama ya The Immortal Yi Soon Shin yalinifanya nisiamini kabisa kwamba ni yeye. Kawa mdogo alafu matendo yake sasa Hahaha
fb2a6c643ec680eb5bbf2e860ba580b4.jpg
Aiseee huyu mtu matendo yake ni kichekesho tosha na yalinifanya nisiamini kuwa ni yeye Kim Kyu Chul.

Ila Jamaa anakipaji sana Damushin na EMPTY hilo mmegundua lakin? Kaishi na Yi Soon Shin kwa upendo na furaha kabla ya kutengana nae baada ya kusemekana eti Yi Soon Shin alimchomesha kumbe sio. Basi toka kipindi hicho akawa na chuki juu yake, kitendo hicho kinanirudisha mpaka katika Drama ya The Great King Gwanggaeto nakumbuka aliwahi fanya kitendo kama hicho. Jamaa aliishi vizuri na Damdeok kipindi wamekamatwa lakini wakaja kuwa maadui tena akiapiza kurudisha kisasi kwa Damdeok. Ila kwa baadae walipatana tena hahaha ndio raha ya kutizama Korea Drama tena ziwe historical. Nimependa sana jinsi Jamaa anavyo badilika yuko vizuri sana kipaji anacho kwakwel. Nacheka sana na Kufurahi pindi nikikumbuka maisha aliyo ishi na rafiki yake Yi Soon Shin na maisha baada ya kupewa Cheo cha Supervisor. Huyu Jamaa ni kituko

mjr95.
 
Na Ilitoka Mwaka Huo Kweli??
Ilitoka mwaka 2006. Hii drama inaelezea mambo yaliyotokea nchini korea kabla na baada ya vita vya pili vya dunia, tukio kubwa ni lile lililotokea mwaka 1950 hadi 1953 ambapo kim il sung na kabinet yake walipoamua kuamsha jeshi lake kutoka Pyongyang na kuipiga na kuichukua mji wa seoul uliokuwa chini ya president rhye na dola ya marekani (miguk). Pia inaelezea jinsi gani wajapan walivyoiachia ardhi ya korea na mengineyo mengi kama kubadilishwa kwa mpaka wa korea mbili kutoka 38 parallel na kuamishiwa pahala pengine kwa makubaliano ya kivita DMZ.
 
Damushin Sunbae na EMPTY Sunbae mkuje huku kuna jambo nimegundua ya Six Flying Dragons. Yaani akawa mdogo alafu akawa sie mtu yule mwenye mienendo ya episodes za mwanzo. Mpaka sasa siamini kama ni yeye, hahaha huenda nikaamin kwa mbeleni.
16cd26c52bda9e74b7c7d81e421905ec.jpg

Aliye nishangaza zaidi ni Kim Kyu Chul.
223e94edef2e6d33f9966b535919cbf5.jpg
fb2a6c643ec680eb5bbf2e860ba580b4.jpg
aada ya kupewa Cheo cha Supervisor. Huyu Jamaa ni kituko

mjr95.
Huyu mzee namkubali sana. Pia kacheza kwenye drama ya king dae joyeoung ya mkali choi soo jong, pia ktk drama ya jingbirok, the memoir of imjin war kama mfalme wa wae (emperor haedayoshi)
 
hili andiko lako nimelirejea kulisoma mara nne ndipo angalau nikapata cha kukujibu, kiukweli hili andiko limenifanya muda huu niitafute episode ya 11 hadi ya 15,wakati asubuhi nilisema nataka niiweke kiporo sasa kwa huu ushawishi wa andiko lako kwa nini nisikuite sunbaenim?
kiukweli nimevutiwa zaidi na urafiki wa tokea utotoni kati ya ryu seung ryong, yi soon shin na won kyun. huyu ryu seung ryong baadae anakuja kuwa na nyadhifa mbali mbali kwenye utawala wa mfalme seonjo na kwenye vita ya imjin war alishika nyadhifa ya waziri wa ulinzi na ndie aliekuwa akimpa support kubwa sana yi soon shin. baada ya kuona mfalme seonjo amekuwa na hofu na yi soon shin aliamua kuacha shughuli za kisiasa, kama sikosei episode ya 3 ya drama hii anaamua kupeleka barua ya kuacha kazi kwa mfalme seonjo.
hembu naombeni jina ya hii serious
 
Ilitoka mwaka 2006. Hii drama inaelezea mambo yaliyotokea nchini korea kabla na baada ya vita vya pili vya dunia, tukio kubwa ni lile lililotokea mwaka 1950 hadi 1953 ambapo kim il sung na kabinet yake walipoamua kuamsha jeshi lake kutoka Pyongyang na kuipiga na kuichukua mji wa seoul uliokuwa chini ya president rhye na dola ya marekani (miguk). Pia inaelezea jinsi gani wajapan walivyoiachia ardhi ya korea na mengineyo mengi kama kubadilishwa kwa mpaka wa korea mbili kutoka 38 parallel na kuamishiwa pahala pengine kwa makubaliano ya kivita DMZ.
aigooooo naomba jina la hii drama niicheki mamaana wengine hapa tunataka tujue maisha ya Korea ili tuje kwenda Ku suverve life huko Seoul or busan
 
Huyu mzee namkubali sana. Pia kacheza kwenye drama ya king dae joyeoung ya mkali choi soo jong, pia ktk drama ya jingbirok, the memoir of imjin war kama mfalme wa wae (emperor haedayoshi)
Mkuu hapo unamsemea nani? Maana nimeongelea Kim Kyu Chul na Kim Myoung Min. Kama ni Kim Kyu Chul huyu jamaa ni moto kabisa anajua sana aisee. Napenda sana anavyo tulia katika nafasi anayo pewa kucheza kwakwel anauvaa uhusika vile itakavyo haswaa.

Dae Jo Young ni drama niliyo itafuta bila ya mafanikio yoyote yale website zote nimepita lakin chakushangaza sijaikuta. Kama kuna website ama link Yenye hiyo Drama basi iweke hapa nikaishushe haraka sana.
 
Namkusudia huyu

fb2a6c643ec680eb5bbf2e860ba580b4.jpg
 
K
Mkuu hapo unamsemea nani? Maana nimeongelea Kim Kyu Chul na Kim Myoung Min. Kama ni Kim Kyu Chul huyu jamaa ni moto kabisa anajua sana aisee. Napenda sana anavyo tulia katika nafasi anayo pewa kucheza kwakwel anauvaa uhusika vile itakavyo haswaa.

Dae Jo Young ni drama niliyo itafuta bila ya mafanikio yoyote yale website zote nimepita lakin chakushangaza sijaikuta. Kama kuna website ama link Yenye hiyo Drama basi iweke hapa nikaishushe haraka sana.
King dae joyeoung Website ya kuipata siifahamu. Ila mm nilinunua DVD yake
 
d49173a9-83eb-4839-8e1f-232fb03c891e.jpg

Ni Medical Drama Lakini Naweza Sema Ni Drama Bora Kati Ya Hizi Zilizoanza Wiki Hii...
Iko Na Stori Tamu Sana Kama Ni Mtu Unayependa Medical Ishu..

Nimempenda Bure Uyu Kijana Kwenye Strongest Alinivuta ila Now Kanikamata..

Kuna ichi kitu Ninakiona Kwenye Korean Drama Kuna Utofauti Mkubwa Sana Kati ya Celeb Na Actor au Actress
Uyu Kijana Na Soo Bin Ni Waigizaji Wazuri Sana Japo Izi Drama Walizocheza Tofauti Ni Zimekuwa Na Mapokeo Madogo Kwa Maana Ya Rating Zake Ni Ndogo Sana Ukilinganisha Na Izi Drama Za Maceleb Ambazo Zinalushwa Muda Mmmoja Kwa Station Tofauti..

Kuna Tofauti Kubwa Sana Kati Ya Soo Bin Na So hyun...
So Hyun Sijawahi Muelewaga Sijuhi Kwa Nini Uigizaji Wake Aujawahi Niivuta Kivilee Naangalia RADIO ROMANCE Coz Ya Male Lead Kuna Kitu Nimekiona Kwake Natamani Nikione Tena Na Tena..

Ila CROSS Itafuteni Ila Mwenye Kupenda MEDICAL Ishu.
 
Huu uzi nilipotea sana kutoka kitambo, Now nimerudi
Cc. Aminas
noona naomba uniandikie list ya hottest korean drama za kuanzia june 2017 mpaka leo hii ila ziwe tayari completed sio on going.
ahsante

Poa Ngoja Nikuangalizie...
Karibu Tena..
Na Pole Na Kupotea
 
Back
Top Bottom