Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Haha nisamehe my dongsaeng kiukweli nashukuru kunipa moyo maana nilikuwa naitamani siku nyingi sana ila nilikuwa naziogopa zile episode 62. Lakini bado naona empress Ki bado itabaki kuwa drama bora kabisa kwangu ingawa hii pia ni fire

Mimi drama zangu bora ni
1.Jumong
2.The Great Queen Seondeok
3.Dong Yi
Empress Ki ni kali sana lakini kwangu bado hazijafikia balaa la hizo 3 hapo juu.
 
Hata mimi Alcheon nilimkubali sana, ila baadae Bidam nikamkubali zaidi [emoji4]
Mimi alikuwa ananikera mtu gani anabadilika ka kinyonga bwana..tufanye nae yalikuwa ni malengo yake ila alipokuwa ananikera zaidi ni pale alipokuwa anaenda kujiliza liza kwa Deokman wakati anajua ana mambo yake ya chini ya kapeti, yaani anataka malkia amuamini kwa asilimia zote wakati ndumilakuwili
 
watanzania mna mda sana.tuombeeni hata sisi tulio huku maana hata kumuona mwanamke anazubaa zubaa ni vigumu.Mungu atusaidie sana.
 

Sasa wa kulaumiwa hapo si writer jamani? Bidam hana kosa [emoji4]
Halafu inashangaza kwanini drama zenye sad ending ndio tunazipenda? Hakuna drama ambazo zimewahi kuniumiza kihisia kama hizo 2 za mwanzo ila ndio nazipenda kupitiliza.
Yenye good ending (Dong Yi) ndio nimeiweka ya mwisho heheeeee

Sijui kwanini muandishi yule genius aliamua kuharibu character ya Bidam namna ile, lakini kwakuwa ni historical drama huenda mambo ndivyo yalivyokuwa hivyo kweli.
 
Hahaha kumpenda au kumchukia mtu si kunaendana na character aliyocheza au? Ila kwa kweli mwandishi hajakutendea haki kabisa
 
Kama uliwahi kuitazama "THE RETURN OF IL JIMAE"kuna kuna mtu humo ndani anaitwa "Hwang beo" huyo jamaa sura yake ukiitazama tu ni kituko, kwanza alikuwa na mwendo wake utadhani anacheza (Magulu baja) 😀😀 kifupi ni kituko.
 
Miye niliitazama 2011 tena wakati huo nasoma Mafundisho ya Kipaimara.
Kwahiyo sikumbuki vizuri, but 2017 nilijaribu kuirudia nikaishia sehemu ya 10 sababu ya kuwa busy.
I think "ITV tz" wanaionyesha kama nitakuwa sikosei.
 
Haha nisamehe my dongsaeng kiukweli nashukuru kunipa moyo maana nilikuwa naitamani siku nyingi sana ila nilikuwa naziogopa zile episode 62. Lakini bado naona empress Ki bado itabaki kuwa drama bora kabisa kwangu ingawa hii pia ni fire
Hapa ndo na amini kuwa binadamu tunatofautiana kimapenzi.
Drama bora zangu
1 Dong Yi
2 King Gwanggaeto the Great Conqueror
3 Prince of the Legend(Chumo)
4 Seon Deok(Queen)
5 Bridal Mask.
Nipo tayari kuirudia drama ya Kim Suro mara 20, lkn nisiitazame Empress Ki.
Kwa sasa nipo kwenye mtambo mnene kabisa ( Jeong do Jeon na The great King Sejong) hizi drama ni shule.
 
Ukiitazama King's Dream (Dream Empire) na Queen SeonDeok zinaelezea kisa kimoja lakini zina mkanganyiko, sasa sijui kama ni wanahistoria walitofautiana katika utunzaji wa kumbukumbu zao au ni waandaaji walitaka kuonyesha utofauti!!.
All in all Bidam kachorwa kama kama mtu aliye na tamaa ya madaraka kwenye Drama zote 2.
 
Jumong.!!????
 
Alivyo kuwa akipaka ile kitu mdomoni kama mwanamke vile [emoji4][emoji4]
 
Ila Nifah naomba nikuulize, hivi ule upigaji kura mbona sikuuelewa inakuwaje watu wengi wanaunga mkono hoja halafu tunaambiwa proposal imekuwa rejected?
 
Alivyo kuwa akipaka ile kitu mdomoni kama mwanamke vile [emoji4][emoji4]

Ndivyo alivyo bhana, Bidam lips zake ni za pink. Kwani hujawahi kuona watu wa namna hiyo?
Bidam ni handsome kwelikweli.
Kama hujui baada ya hiyo series kuisha wanawake wa Korea walimchamgua kama sexiest man wa Korea [emoji4].
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…