Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

yeon gaesomun alikuwa ni
  1. shujaa wa goguryeo
  2. dikteta wa goguryeo
historia ya bwana yeon gaesomun itaendelea kuleta mgawanyiko wa kifikra mpaka ulimwengu utakapokwisha
Huyu jamaa Yeon Gaesumn maisha yake si yameguswa kwenye King's Dream Drama.au ni Bange kutoka Pyeongyang zishaanza kuniathili
 
Age Of Warriors.. Hawa wahuni ni nyoko. Nimejikuta kama " Emperor Wang Gun" naitazama mara mbili mbili, mara ghafla nikajikuta Naikumbuka "King Gwanggaeto the Great Conqueror", 'Dae Joyoung',. "Jeong Do Jeon" 'Great King Sejong' n.k
Hawa wahuni wanajua kucheza Historical Drama, sio hawa ndugu zake Daemusin mabishoo Seoul, kaZi kuuza sura. Hehehhe na Jinsi nionavyo Hizi Sura usitegemee scene ya mapenzi.
 
humo ndani wakitongozana ni full kituko.
mwanamke na mwanamme wanakaa umbali wa mita 100 kama GK wa team A na B.

mwanamke: nakupendaaa
mwanamme: unasemaje sijasikia
mwanamke: nimesema nakupenda general
mwanamme: aaaahhhhh kumbe nije na panga huko uliko.
 
Wewe jamaa bhana
 

Haha! Hayo malavidavi ni ya ukuryani huko Mara.
 
Daemusin!
Mimi sina uelewa sana na siasa, ustaarabu na uchumi wa nchi za Korea. Ila nimetokea kuvutiwa sana na huu mfumu ulioko kwenye makampuni kama Samsung,Hyundai etc..
Chaebol
naomba ukipata muda unieleze nielewe vizuri huu mfumo maana nimeusoma toka 2017 ila nimeelewa juu juu. Mimi hua ni mtupu kwenye masuala ya hesabu za fedha
 
Ahsante mkuu kwa masahihisho.

Nilidhani ndugu muuliza swali alihitaji ushiriki mwingine wa Yeong-po, yule wa kwenye Prince of Legend (Jumong) ama kwa jina lake halisi la Won Ki-jun ambaye ameshiriki pia katika hiyo Gu Am Heo Joon 'Remake' ya mwaka 2013. Ila kama ni mzee Jeong Gwang-leol, Yeah! upo sahihi kuwa ameigiza 'Orijino' Gu Am Heo Joon ama Heo Joon ya mwaka 1999.
 
Hiyo series ya the empress ki Togon au mfalme wa yuan atakufa? Maana me bado sijaimaliza
Pengine mpaka sasa hivi utakuwa umekwisha kuimaliza hiyo 'Empress Ki' na kwa maana hiyo utakuwa umepata jibu la swali lako ndugu.

Kama bado hujaimaliza basi nakushauri uimalizie ili upate jibu la swali lako maana kwa kitendo cha kulijibu swali hilo kunaweza kumuondolea hamu ya kuitazama Drama hiyo mdau ambaye bado hajapata kuitazama na kuimaliza.

Ila katika historia ni kweli alikufa.
 
Duh! kukutajia Comedies 5 nzuri ndani ya kipindi hicho kifupi cha 2018/2019 ni 'Limited' kimtindo maana nzuri nyingi zipo ila katika miaka tofauti tofauti kuendana na mitazamo ya kila mdau katika tasnia.

Mfano, kuna hiyo uliyoitaja hapo, 'Come Back Mister' ni Comedy nzuri sana ila ni ya mwaka 2016. Pia kuna 'Kill Me Heal Me' ya mwaka 2015 ambayo pia ni moja ya Comedies nzuri "kwa maoni yangu".

Nyinginezo ni;
  • Legend Of The Blue Sea (2016-2017)
  • Suspicious Partner (2017)
  • Introverted Boss (My Shy Boss) (2017)
  • Welcome To Waikiki (2018)
  • Strong Woman Do Bong Soon (2017)
  • I'm Not A Robot (2017-2018)
Na kuna nyingine ya kitambo kidogo, 'Master's Sun' ya mwaka 2013.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…