Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hivi siku kuna movie inaitwa tax driver ya kikorea or mi ndo nachanganya mafile??
 
inaitwa a tax driver, imeigizwa na song kang ho wa parasite kama umeiangalia
Oooh oky basi nilishaitazama nikashia njiani....Parasite bonge la picha nimeiona nzuri,alinikosha sana humu.tena nilikua nafatilia movie zake baada ya kumuona kwenye the good the bad
n the weird

Mbona sijawai kuona drama za huyu baba??namuona kwny movie tu
 
Naombeni mnitajie historical drama nzuri ndefu sio hizi za 16 episodes
Wewe waweza kuwa miongoni mwa watazamaji wachache na wa kipekee katika ulimwengu wa tasnia ya drama sababu kuna idadi kubwa ya watu siku hizi wanaopenda kuangalia drama fupifupi. Wakianza kuangalia asubuhi, usiku unasakwa mzigo mpya wa kuangaliwa kesho yake. Kwa wiki moja tu mtu anaweza kumaliza hata drama 10 au zaidi.

Vijana wana msemo wao wanasema "kasi ya 4G".

Drama ndefu hasa historical ambazo ni nzuri mtafute mtu mmoja anayeitwa Lee Byung-hoon. Huyu mzee ame-direct miongoni mwa drama kali za historical ambazo zimepata kukubalika sana katika tasnia.

Miongoni mwa hizo drama alizohusika huyo mzee ambazo kwangu ni nzuri na pia ni ndefu ni hizi hapa tano:

1) Lee San (Yi San) ya mwaka 2007 ambayo ina 77 episodes.
2) Dong Yi ya mwaka 2010 yenye 60 episodes.
3) The Flower in Prison ya mwaka 2016. Ina 51 episodes.
4) Horse Doctor ya mwaka 2013 yenye 50 episodes.

Bila kusahau ya tano; Jewel in the Palace ya mwaka 2003 yenye 54 episodes. Kama ni shule, basi hii ni chekechea maana kupitia drama hii, kuna list ndefu sana ya wadau ulimwenguni walioanza kuwa wapenzi wa Korean historical drama na utamaduni wa Korea kwa ujumla.

Nina imani kuwa hizi tano zitakidhi haja yako!
 
Asante kwa recommendation.
 
Duh! Kwa masharti hayo, drama itakapoisha unaweza kujikuta umehitimu shahada ya sheria bila cheti!
 
Asante..drama fupi za mjini nimeangalia sana zimenichosha..nataka nigeukie upande wa pili kwa muda then ntaendelea na fupi [emoji16]
 
Asante..drama fupi za mjini nimeangalia sana zimenichosha..nataka nigeukie upande wa pili kwa muda then ntaendelea na fupi [emoji16]
missyrose naomba unitajie drama Kali nikaangalie ambazo sitapoteza mb zangu ninaomba muongozo wako maana nimegundua wewe na mimi tuna taste zinazofanana hii vincenzo nimeangalia episode 1 tu nimeona utopolo mtupu masiala ni mengi nimeamua niachane nayo.
 
Usinikumbushe wakat natizama Money Game zile financial terms yani sikuwa naelewa hata Ila ndo nakomaa mpaka mwisho

Humu nimemuona Yule mkaka alikuwepo kwenye itaewon kama financial adviser wa ML, nampendaga si ntakomaa na hicho kisheria tu[emoji23]
 
Hiyo vincenzo jikaze ukifika ep ya 3 uje hapa,
Yani ni nzuri mno mno uyo Song Joo ki so wa mchezo mchezo.

Humo kila mtu star hadi njiwa- INZAGHI
 
money game drama nayo ilikuwa tafrani tupu ila baadae nilikwenda nayo vizuri, hapo ndipo tunapouona ubora wa wenzetu na uandishi wao uliojaaa tafiti za kisomi juu ya jambo fulani wanalotaka kuliwasilisha kwa njia ya sanaa.
Kabisa

Kama za kidaktari mpaka nahis naweza kuwa neuro....hahahha Kwa kutizama tu drama za kikorea
 
Recommendations nimetoa humu humu kwenye huu uzi ngoja nikitulia ntakutajia
 
Hiyo vincenzo jikaze ukifika ep ya 3 uje hapa,
Yani ni nzuri mno mno uyo Song Joo ki so wa mchezo mchezo.

Humo kila mtu star hadi njiwa- INZAGHI
Binafsi nisipoielewa episode ya kwanza siwezi kuangalia Tena hiyo drama bando langu linathamani Sana ina utoto mwingi hata huyo star hajanivutia kiuchezaji kabisa mbona vagabond, Last, innocent defendant, empress ki, Penthouse,Mouse,Jumong,K2 n.k zinaeleweka kuanzia tu episode 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…