Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kim soo hyun ndo wa kwenye a man from another star,Doctor stranger na hiyo aliyomaliza kuangalia. Yupo kwenye series nyingi Sana na sahivi ndo msanii wa korea anayelipwa pesa nyingi kwa kucheza movie.
hapana mkuu kim soo hyun hakucheza drama ya doctor stranger yule bwana mdogo anaitwa lee jong suk ambaye kwa mujibu wa stori na yeye binafsi amethibitisha ya kwamba ana mahusiano ya kimapenzi na park shin hee ambaye ameigiza drama kama THE HEIRS
Pia ameigiza drama kama vile
MR W
PINOCCIO, ICAN HEAR YOUR VOICE
 
Hao wazee hapo juu ni nomaaaaaaa!
Hasa waziri mkuu (huyo Mzee wa pili) ni shida aiseeeee.
Yupogo serious hadi nachukia,na usiombe aigize adui utalia maana ana mipango kinoma.
Kila mambo yanapotaka kuwa mazuri anatibua
Hahahahahaaaaa

Kweli Wakorea wamejaliwa sana vipaji vya kuigiza,yani wanaigiza hadi unajisahau kwamba wanaigiza.
 
Asante kwa kutuondolea utata huu. Sasa tunaomba kama hutojali utuandalie historia ya yule jamaa aliyecheza My love from another star,The moon that embraces the sun na nyinginezo.
Pia tungependa kujua mahusiano yake ya kimapenzi yakoje na anatoka na nani?
Asante.
 
nimeamua kumaliza kiporo changu
kbs drama awards 2016 part 1. boyeza cc button for english
 
Bridal mask kwangu nahisi ndio best series, nyingne nilizo angalia nikazipenda ni Kingdom of the wind, tree with hidden roots(kwakweli hii si ya kukosa kwa wapenzi wa historical ), the heirs,
 
Bridal mask kwangu nahisi ndio best series, nyingne nilizo angalia nikazipenda ni Kingdom of the wind, tree with hidden roots(kwakweli hii si ya kukosa kwa wapenzi wa historical ), the heirs,
Jamani mimi pamoja na ubobezi wangu uliotukuka ktk Korean series sijatokea kuipenda bridal mask kabisa.
Yani ktk series zangu kali ile haisogei hata kwenye 20 bora [emoji13]
 
Jamani mimi pamoja na ubobezi wangu uliotukuka ktk Korean series sijatokea kuipenda bridal mask kabisa.
Yani ktk series zangu kali ile haisogei hata kwenye 20 bora [emoji13]
Labda kwa sababu ni manish movie, ndio series pekee iliyonitoa chozi pale joo won amefika nyumban anajua leo anaenda kumkamataa bridal mask anafika pale anakuta ni kaka ake ile analia kumuita mama ake anakuta mama ake nae kafa, sasa kale kamtiririko had anafikia kumuua kaka ake kalikua kanasikitisha sanaa
 
Sijui kwa nini genre zangu hamzizungumziagi kabisa humu, napenda sana zile za kipelelezi na action kama city hunter, 3days, n.K hzi za historical naweza sinzia kwa kweli. mkuu Damushinmuhyool please note down series za aina hyo nichek ambayo sijaziona, karibu pia Nifah mkinitajia top 5 5 itakuwa poa zaidi
 
ahsante mkuu kwa taarifa muhimu, nimeshaimaliza THE JING BI ROK THE MEMORY OF IMJIN WAR kiukweli nimetumia siku 5 mfululizo....
Hiyo ni siyo drama kamili. Laiti ungeangalia drama yake halisi ya "The Immortal Lee Soon-shin"
 
Usijali,nitakuandalia list yangu bora.
Pia jitahidi kuzipenda historical maana ndio utamu wa korean series ulipo.
Huko mjini hamna la maana.
 
Usijali,nitakuandalia list yangu bora.
Pia jitahidi kuzipenda historical maana ndio utamu wa korean series ulipo.
Huko mjini hamna la maana.
Za mjini ni "copy & paste" za magharibi. 'Historical' zina maudhui mengi ya maisha kati ya mtawala na mtawaliwa. Ukizitizama kwa umakini, zinatoa picha kuhusu watawala na watawaliwa duniani kote, km kuchaguliwa kwa Trump Marekani.
 
humu kwenye jing bi rok nimempenda sana ushirikiano wake na ryu seong ryeong ulimfanya mfalme seonjo awe na kazi rahisi sana ila walishindwa kumsikiliza bwana ryu seong ryeong alipowataka waimarishe ulinzi
 
Wakati unaandaa hyo list andaa pia na hizo historical ambazo ni bora kiasi kwamba nikichek tu nahamia mazima
Mbona hostoria ya Korea imeandikwa sana humu na orodha ya hizo drama zikatajwa! Kwa kifupi:
1) Goguryeo: Jumong; Kingdom of the Wind; Princess Ja Myung Go na King Gwanggaeto the great.

2) Baekje: King Geunchogo; Gye Baej; na King's Daughter.

3) Shilla: King's Dream na Queen Seon Duk

4) Goryeo: Age of Warriors; Emperor Wang Gun; Empress Chun Chun; The Great Seer; Empress Ki na Six Flying Dragon.

5) Balhae: Dae Jo Yeong

Na kadhalika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…