siku kama ya jana ya tarehe 15/03/2008
song il kook mmoja kati ya waigizaji walionifanya nipende kufuatilia maisha ya korean hallyu star alifunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu anayejulikana kwa jina la
Jung seong yeon ambapo ndoa yao ilikuwa ya kitamaduni ilikuwa ni miezi michache kabla ya
song il kook hajaelekea China kwa ajili ya kushoot drama ya
kingdom of the wind ambapo alicheza uhusika wa
prince muhyool (king damushin muhyool), uhusiano wao ulianza 2006 wakati song il kook akiendelea kushoot drama ya jumong ambayo ilikuwa ni maarufu kipindi hicho na mwanadada
jung seong yeon ambaye kitaaluma ni mwanasheria ambaye kwa mujibu wa kituo cha television ya Tvn "the list 2015" alishika nafasi ya pili ya wanawake wenye mafanikio ambao waliofunga ndoa na celebrities wa kiume nchini korea. rekodi zake zinaonesha alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wenye matokeo bora sana katika kitivo cha sheria kwenye chuo kikuu cha Seol National university ambapo alisoma Master na kutunukiwa heshima ya udaktari akiwa na miaka 33. kwa sasa ni jaji wa Incheon District Court.
View attachment 481892View attachment 481893
siku kama ya leo 16/03/2012 wakati akiwa katika majukumu yake ya kazi ya uigizaji wa drama ya Fermentation family (kimchi family) alipata taarifa ya kwamba mke wake amejifungua watoto 3 wa kiume na kuamua kufuata ushauri wa mama yake Kim eul dong akawaita majina ya :
daehan = jamhuri (republic) : ndie wa kwanza kuzaliwa na ni mwajibikaji,ana aibu kama baba yake,ni handsome kama baba yake na ana matatizo ya macho kama baba yake.anapenda kupiga picha kama baba yake
minguk = korea : ni mcheshi sana (cute), ana akili sana kama mama yake na ana penda sana kuimba
manse = long life (hurray) idumu milele : msumbufu sana na ni free spirit,anapenda kula kama baba yake.
leo wametimiza miaka 5 ya kuzaliwa sina budi kuwatakia heri ya kuzaliwa;
pia sina budi kuwatakia wazee wao heri ya kutimiza miaka 9 ya ndoa yao siku ya jana.
View attachment 482007
View attachment 482008
hii ni moja kati ya familia bora kuwahi kuishuhudia.kila siku namuomba Mungu anijaalie nije niwe baba bora kama
Song Il Kook na pia nipate mke bora kama
Jung Seong Yeon.
nilitamani muendelee kuwepo kwenye show ya return of superman ila nitaendelea kuheshimu maamuzi yenu. nilijifunza mambo mengi sana.
mwishoni mwa mwaka 2014 song il kook aliamua kutengeneza calendar za 2015 kwa kutumia picha za watoto wake kwa jinsi walivyokuwa maarufu ndani ya masaa 24 aliuza copy 100000 ambazo ilikuwa ni sawa na (687 million won, au $625,000 USD.) ila aliamua pesa zote kuzipeleka kwenye charity
pia kwa mujibu wa apple daily mnamo mwaka 2015 song triplets waliingia kwenye top 5 ya celebrities wanaotengeneza hela nyingi nchini korea kupitia matangazo ambapo walilipwa takribani (usd$ 4.26million) wakiwa na miaka 3 tu.
Saengil chukahamnida -happy birthday to you
Saengil chukahamnida -happy birthday to you
Saranghaneun (daehan, minguk,manse) happy birthday dear (daehan,minguk,manse)
Saengil chukahamnida