The king and I drama
- Hutokuwa mwanaume wala hutokuwa mwanamke
- Hutoiona ladha ya kuwa karibu na mwanamke kimwili
- Hutokuwa na ukaribu dhidi ya familia yako.
- Hutokuwa na kizazi kinachotokanwa na damu yako
Bado tu wahitaji kuwa eunuch?
Ndio.
Hutojutia uamuzi wako?
Ndio sitojutia.
Aigoo.
Hii drama nimeiangalia episodes 5, nikajitia ujinga wa kwenda youtube kuangalia OST.
Nilichokutana nacho ni clip za tragic ending.
Nimebaki na swali, je niendelee nayo haliyakuwa hii drama ina episode 60 na kitu.
=======
drama inazungumzia zaidi maisha ya eunuch, kuanzia recruitments zao, kuajiriwa kwao royal palace, mamlaka yao, nguvu zao kwenye kuta za siasa, nguvu zao za kucontrol rasilimali za nchi, vita ya madaraka kati yao.
Hawa mabwana hawazai ila wanaruhusika kusajili watoto wa kuendeleza kizazi chao.
Kwa mujibu wa hii drama hawa mabwana walikuwa wanaoa lakini ndio hivyo masikini mabwana hawa walikuwa wanakatwa korodani (castration)
Ukatili wa hali ya juu sana.
Bwana huyu alitokea kwenye familia ya baba aliyehusika na uhaini wa kutaka kumpindua mfalme sejo, huyu sejo alikuwa mtoto wa sejong the great....
tofauti na baba yake huyu sejo alikuwa kama babu yake taejong.
Bwana yule udogoni kwake akapendana na binti, bwana yule prince naye akavutiwa na binti. Wote wawili walikuwa ni nobles ila yule alikuwa ni peasant.
Inaonekana mbeleni ilifungwa ndoa ya siasa kati ya binti na huyu prince ambaye baadae alitawazwa kuwa mfalme.
Uamuzi huo ulimuumiza sana bwana peasant, nadhani katika kuwa karibu na mwanamke akachukua uamuzi wa kuwa eunuch ili awe karibu na mwanamke ampendaye huko ikulu.
Sijui kimetokezea nini huko mbele, mfalme akatoa hukumu ya kifo kwa huyo mwanamke ambaye ni mke wake....mambo ya siasa hayoo.
Na aliyepewa amri ya kupeleka sumu kwa huyo mwanamke ni huyooo bwana eunuch.
Hatimaye binti akanywa sumu.
======
Unrequited love is love that is not openly reciprocated or understood as such by the beloved. The beloved may not be aware of the admirer's deep and pure affection, or may consciously reject it.