Upo kama mimi. Mimi pia naangalia genre za aina zote sichagui genre fulani tu ya kutembea nayo napendezwa na zote mradi story iwe nzuri.
Yaani iwe (sageuk, romance, melodrama, comedy, mystery, action, horror, medical, legal, coming-of-age, fantasy, sports,suspense, thriller, sci-fi ) mimi naangalia tu . Hii imenifanya kufurahia sanaa hii ya wakorea sababu ukiji-limit kuna vitu na ladha fulani unakosa kutoka genre zingine.
Yote kwa yote kila mtu ana taste yake na maamuzi yake katika kuangalia drama lakini tujitahidi tusikosoe genre wanazoangalia watu wengine.
NB: Kuna jamaa yangu yeye akikuomba movie ukampatia kitu cha kwanza anakuuliza "ina mkono hii(mapigano) kama haina mkono basi usinipe"[emoji1787].