Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Umesomeka mkuu....kila mtu afanye kinachomfurahisha bila kumtingisha jirani [emoji3577][emoji3577]
 
Upo kama mimi. Mimi pia naangalia genre za aina zote sichagui genre fulani tu ya kutembea nayo napendezwa na zote mradi story iwe nzuri.

Yaani iwe (sageuk, romance, melodrama, comedy, mystery, action, horror, medical, legal, coming-of-age, fantasy, sports,suspense, thriller, sci-fi ) mimi naangalia tu . Hii imenifanya kufurahia sanaa hii ya wakorea sababu ukiji-limit kuna vitu na ladha fulani unakosa kutoka genre zingine.

Yote kwa yote kila mtu ana taste yake na maamuzi yake katika kuangalia drama lakini tujitahidi tusikosoe genre wanazoangalia watu wengine.

NB: Kuna jamaa yangu yeye akikuomba movie ukampatia kitu cha kwanza anakuuliza "ina mkono hii(mapigano) kama haina mkono basi usinipe"🤣.
 
Vile Ninavyolifuatilia pambano la wazee wa tastes humu ndani huku nikiendelea na mitafuno yangu ya chakula cha wakorea
Your browser is not able to display this video.
 
Umenena vema mkuu mimi pia huangalia kila kitu kasoro horror (zile za mazombie ) ndio hazinivutii zingine zote napeleka. Kama mtu anajilimit ajilimit yeye sio kulimit na wengine pia
 
Wataachana tu. Lee Seung gi simuamini hata [emoji1787][emoji1787]
Watadumu sana kwa sababu mwanamke sio staa sana japo anatoka familia ya sanaa Mama yake na Dada yake pia ni waigizaji.

Lee Seung Gi sio mzinguaji kama unavyodhani,hadi kamuoa Da In kuna baadhi ya changamoto zilitokea kama vile mashabiki kumtisha jjamaa aachane nae la sivyo wanamcancel,Baba yao Da In na Yubi(ni wa kambo ila ndio wamechukua jina la ukoo kwake) alikuwa na history za kihalifu kiasi kwamba Korean netizens wakakazia jamaa asioe kwenye hiyo familia na kipindi kile mara nyingi alikuwa anapenda kukutana na familia ya Da In.


Angekuwa hana nia ya dhati nae kwa walivyo Wakorea wangekuwa washaachana.


 
Nimetania tu [emoji16][emoji16] ila nashukuru kwa info
 
Kuna series moja aliuliza mdau, nami natamani kuifahamu au kupata jina lake.

Inaanza kwa kuonesha jamaa mmoja anapitia changamoto kweny kulea wadogo zake baada ya baba (wazazi wake) kufia kweny Mines za makaa ya mawe.

Baadae alikuja kukua na kutafta namna ya kupata haki au fidia ya mzee wake. (NI DRAMA MOJA INA MAJONZI SANA) nakumbuka enzi hizo ililiza wengi.
Kama unaikumbuka naomba jina lake.

Sina hakika sana na mtiriko wa matukio nlioelezea hapo juu bt kama umeilewa msaada tafadhal.

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…