Kwa upande wa historical dramas nilijaribu kufuatulia sehemu wanazoigizia nikakuta, kumbe MBC na SBD wanamiliki maeneo ya kutosha (Km squares za maana), zenye majengo ya kizamani kwaajili ya kuigizia pamoja na misitu na mapori.
Mwanzo nilidhani zile nyumba huwa zinajengwa na kubomolewa, wenzetu wamewekeza vizuri kwenye sanaa na kuichukulia kama kazi seriously. Hata ukiangalia budgets zao ni billions of money.
Sijui kuhusu location ya hizi drama za mijini (kama hiyo doctor romantic) ila nadhani pesa huwa inamwaga haswa, pamoja na kuwapiga wahisika course maalumu juu ya namna ya ku-act kama watu wa afya, ikiwa ni sambamba na kuwa kuwaelekeza misamiati ya kitababu.