Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa upande wa historical list yao ni hii ,hapo vilevile sina hata moja niliyowahi kutazama kwa ujumla sijafikisha hata 25 idadi ya Korean drama nilizowahi kuangalia na kumaliza zote wakongwe wakina Daemushin(Mzanzibar ) na wengine heshima yao.View attachment 2620836
View attachment 2620839
Nyingi za kawaida, isipokuwa hiyo Dae Jang Geum( Jewel in the Palace), Six flying dragon kidogo na hiyo Empress Ki.
 
Wakuu kuna njia yeyote ya kupata kimagendo single movies za netflix ? maana nahitajia Godfather of harlem na hizi hapa..
MV5BM2ZmYjUxZDYtMmZlMi00YjlkLTkwNTItMjcxZDRlOTI3ZTNmXkEyXkFqcGdeQXVyMTkxNjUyNQ@@._V1_FMjpg_UX1...jpg


IMG_20230515_115446.jpg
 
Nipe feedback juu ya hiyo Joseon Attorney.
Hiyo inahusu sheria kuna mwanasheria flani alisomea talanta hiyo ili alipe kisasi kwa waliosababisha wazazi wake wafariki.

Lakini katika harakati za kulipa kisasi anakuja kugundua aliofanikisha kuwaangusha walilkuwa vidagaa tu kuna mtu mkubwa alikuwa nyuma yao.

Kipindi chote hicho alitengana na Dada ake ambaye aliolewa wakiwa bado wadogo na hawakuonana tena.


Anyway hii drama sio kila mtu anaweza kuipenda haina action ni watchable kwa wapenda historical dramas.
 
Missing the other sides season 2 nimeipenda. Napenda drama zinazohusu mizimu(ghosts)hasa wasiotisha. Humu inaelezea watu walifariki kwa kuuliwa ama ajali kisha miili yao ikazikwa kwa kificho hivyo wanajikuta kwenye kijiji wasichokifahamu. Mwili ukigundulika anapotea kule kijijini.

Nianze safari ya kuivuta season 1 nayo nione yaliyomo
season 1 nilibahatika kuiangalia,
season 2 imenipita.
thanks kwa taarifa
 
Hiyo inahusu sheria kuna mwanasheria flani alisomea talanta hiyo ili alipe kisasi kwa waliosababisha wazazi wake wafariki.

Lakini katika harakati za kulipa kisasi anakuja kugundua aliofanikisha kuwaangusha walilkuwa vidagaa tu kuna mtu mkubwa alikuwa nyuma yao.

Kipindi chote hicho alitengana na Dada ake ambaye aliolewa wakiwa bado wadogo na hawakuonana tena.


Anyway hii drama sio kila mtu anaweza kuipenda haina action ni watchable kwa wapenda historical dramas.
Story ni nzuri inafaa kwa matumizi nitaitafuta nilicheki mzee wa taste nimeipitisha
 
Dae ni wa kipekee
Mimi nilikua natizama dizain ukiomba movie unakutana nazo enzi za chuo na za itv
Nilivyokutana na huu uzi humu, nikamfuata pm eti naomba movie
imenibidi nirudi PM nithibitishe hiki ulichokiandika.
kumbe ilikuwa July 2017, nimebaki kucheka peke yangu mfano wa kichaa kwa hayo majibu yangu.
yaani nilikuwa kama nalazimishwa kuchati nawe,
siku zinakimbia sana mfano wa kombora la kinzhal
😛😛😛

nimeyapokea maua yako.
shukrani,
ahsante sana,
Mungu azidi kutubariki kwa sote mpaka dakika ya mwisho ya upumuaji wetu.
tulipokoseana tusameheane.
 
Mwaka 2018 nilipojiunga Jf nilijua hakuna mtu anajua mambo ya kuhusu Korea kunishinda, pia nilikuwa nimejifunza kusoma na kuandika kikorea, kuhusu kuelewa nilikuwa bado kwenye amateur level. Lakini nilipofika humu ndani, niliona andiko lake, na kuna vitu nilikuwa nadhani navielewa sana lakini Jamaa alikuwa anavielewa zaidi. Nami sikutaka battle nae bali nilijinyenyekeza na kumwambia kuanzia leo nitajifunza mengi toka kwako. Wapo wengine wapo vizuri mno pia wanafanya vizuri, k Hata hawa dada zetu wakuu wakuu(Numbisa n.k). Wewe nimekuona recently.
Anyway watu nilowakuta humu walinifanya niwe humble nakujifunza zaidi.
Huyu Daemusin aliwahi kunipa kitabu cha grammar za kikorea.
shukrani sana brother tusiejuana kisura.
tumekuwa pamoja kwa takribani miaka mitano na bado tutaendelea kuwa pamoja kwa kheri na fanaka telee.
Inshaallah

unajua mdogo wangu binadamu katu hatuwezi kufanana, cha umuhimu ni kuifahamu mipaka yako ya kiroho, tamaa na kikhulka. hiyo ndio kanuni yangu kubwa niliyoibeba katika maisha na hata shughuli zangu za kila siku.
be humble.
usiogope kutoa mawazo yako,
kubali kujifunza
 
Mwaka 2018 nilipojiunga Jf nilijua hakuna mtu anajua mambo ya kuhusu Korea kunishinda, pia nilikuwa nimejifunza kusoma na kuandika kikorea, kuhusu kuelewa nilikuwa bado kwenye amateur level. Lakini nilipofika humu ndani, niliona andiko lake, na kuna vitu nilikuwa nadhani navielewa sana lakini Jamaa alikuwa anavielewa zaidi.
mwaka 2015 (disemba)nilipojiunga humu JF hata mimi nilikuwa na fikra kama za kwako ila siku ya kwanza tu kuandika comment ndani ya thread hii nikagundua ya kwamba napaswa kujifunza zaidi upande wa historical.
nilikutana na gwiji anaitwa juan moses, mwenyewe alijipa cheo cha balozi wa goguryeo.

baada ya hapo nikaamua kwenda deep zaidi na zaidi kwa lengo la kujifunza.
jifunze uelimike, usipende tu kuandika au kuzungumza hata kama jambo huna ufahamu nalo
 
Back
Top Bottom