jana nchini korea kusini kulifanyika press conference kwa ajili ya utambulisho wa Historical movie inayojulikana kwa jina la
THE FORTRESS.
the fortress ni movies ambayo inazungumzia tukio lililotokezea 1636 nchini
joseon wakati wa utawala wa mfalme
Injo baada ya utawala wa china unaojulikana kwa jina la qing dynasty kuivamia kijeshi taifa la joseon jambo ambalo lilimpelekea mfalme Injo pamoja na watumishi wake kukimbilia Namhan Mountain Fortress eneo ambalo lipo umbali wa km 24 kutoka kusini mashariki mwa mji wa SEOUL. Vita hiyo ilisababisha taifa la joseon kukubali (surrendered) kuwa koloni la china katika mwaka 1636.
kwa mujibu wa rekodi mbali mbali za kihistoria inasemekana mfalme alikaa sehemu hiyo pamoja na jeshi la joseon kwa siku 47 tukio hilo linachukuliwa kama ni miongoni mwa matukio ya fedheha kuwahi kuikumba tawala ya korea.
directoctor hwang dong hyuk jana (23/08/2017)alisema maneno yafuatayo wakati wa mkutano
"
imenifanya nikumbuke uvamizi wa taifa la Qing 1636 tukio ambalo nimelifahamu zaidi kwa kusoma riwaya mbali mbali zinazozungumzia tukio hilo, kiukweli nimefurahishwa na kushangazwa sana baada ya kujifunza mambo mengi na ya kushangaza yaliyotokezea ndani ya ngome, ukweli ni kwamba mambo yaliyotokezea wakati ule yanashabihiana sana na yanayotokezea wakati huu ndio maana niliamua kutengeneza movie ili kuwawezesha watizamaji kujifunza na kulinganisha yaliyopita na yanayoendelea kutokezea wakati huu katika taifa letu.
aliendelea kusema
"
leo hii taifa letu la korea linapitia kipindi kigumu kwa sababu taifa letu lipo chini ya kivuli cha nchi mbili zenye nguvu duniani za Marekani na China jambo ambalo linashabihiana na yaliyotokezea kwenye karne ya 17 wakati tulipokuwa chini ya kivuli cha taifa la Ming dynasty na baadae Qing Dynasty yote kutoka china.
pia director amefurahishwa zaidi na ushirikiano mkubwa ulioneshwa na waigizaji wakuu wa movie hii akiwemo lee byung hun, kim yoon seok, go soo, park hae il, jo woo jin.
movie hii inatarajiwa kuonekana september 27