ni jambo la kufurahisha pale unapoona veteran actors and actress bado wanapewa nafasi ya kuwa lead actor and actress kwenye drama.
ji jin hee amezaliwa miaka 45 iliopita na kwa yeyote anayefuatilia korean drama basi atakubaliana na mawazo yangu ya kwamba jamaa yupo vizuri sana kwenye kuigiza na timu nzima ya misty drama naamini hawajafanya makosa kumpa ofa,huyu ahjussi nilimpenda sana kwenye drama ya dong yi, blood drama alipoigiza uhusika wa daktari vampire na hata kwenye jewel in the palace.
niwe mkweli sijawahi kuangalia drama yeyote aliyoigiza mwanamama kim nam joo ambaye amezaliwa miaka 46 iliopita, kwa jinsi tasnia ya uigizaji nchini korea ilivyovamiwa na kpop idols ni ngumu sana kwa mwanamama mwenye umri wa miaka 46 kuwa lead actress hivyo basi bila shaka yupo vizuri ukizingatia drama yake ya mwisho kushiriki ni miaka 6 iliopita.
nimejaribu kupitia baadhi ya tovuti hii drama ya Misty asilimia kubwa ya walioanza kuiangalia wameipenda sana mtiririko wa hadithi yake.
ila mimi sidanganyiki kwa kipindi hiki ngoja niendelee kupumzika nitakuja kuitafuta siku za mbeleni hukoo.
kwa mujibu wa nielsen korea
episode ya 1 rating yake ni asilimia 3.47, hii ni rating kubwa sana kwa cable tv drama
episode ya 2 rating yake ni asilimia 5.07
hizi cable tv project zao nyingi zimefanya vizuri na zinaendelea kufanya vizuri sana jambo ambalo linazidisha ushindani dhidi ya public broadcasting kama KBS, MBC na SBS.