Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

c04472a1gw1f5jxkyg6iij20ku0gptbd.jpg


DIUjn-iVoAA0v1a.jpg

Jina Lake Ni Gong Hyo Jin au Kong Hyo Jin, Mara Ya kwanza Kumuona Kwenye Drama Ya It's Okay That's Is Love Nikaja Kumuona Kwenye Movie Ya Missing, Nasasa Namuona Pia Kwenye Master's Sun Ni Drama Ambayo Ndo Naiangalia Kwa Sa Ivi

Huwaga Namfananishaga Na Gianna Wa Kwenye The Legend of the Blue Sea Wako Wanafanana Sana Kwenye Uigizaji Wao Japo Huyu Ni Mkubwa Kwa Gianna Kwa Mwaka Mmoja, Ila Ni Wale Wadada Wanaojua Wanachofanya Kwenye Tasnia Yao,
 
Mkuu damushin ile kiporo yetu ya fortess
ilikuwa ni 17/10./2017.ndipo uliniomba nikuweke link ya historical movie inayoitwa the fortress.
bahati nzuri leo nimetembelea tovuti ya dramanice ndio nimeona wameshaiweka subtitle ya kiingereza.
THE-FORTRESS_Main-Poster-e1521502729925.jpg

kwa ufupi
mnamo mwaka 1636, Qing dynasty ambayo ndio china ya kipindi hiki kama sijakosea waliivamia nchi ya joseon ambayo kwa sasa ni korea japokuwa imegawanyika nchi mbili. mfalme Injo na watumishi wake waliikimbia ikulu na kwenda kujificha kwenye ngome iliopatikana maeneo ya milimani inayoitwa Namhansanseong.

mtumishi mmoja aliyekuwa anaitwa Choi Myung-Kil aliamini njia pekee ya kurudisha hali kama ilivyokuwa mwanzoni ni kuingia makubaliano na QING, kwa tafsiri ya haraka haraka ni kwamba joseon pia wakubali matakwa ya utawala wa Qing.
Pia kulikuwa na mtumishi mwengine aliyeitwa Kim Sang-Hun ambaye aliamini njia pekee ya kurudisha heshima ya serikali ya joseon ni kuendelea kupambana hadi mwisho wa nguvu zao.
je mfalme atachukua maamuzi ya nani?
starring
lee byung hun = choi myung kil
kim yun seok = kim sang hun
park hae il = mfalme Injo​
Awards
  1. 2018 (54th) BaekSang Arts Awards - May 3, 2018 ,"Best Film"
  2. 2017 (38th) Blue Dragon Film Awards - November 25, 2017 ,"Best Screenplay" (Hwang Dong-Hyuk)
nakuomba radhi kutoka ndani ya kiwililiwili changu kilicho hai muda huu, hivyo basi usije ukadhani nilikupotezea kwa kipindi cha miezi 10.
aigoooo lakini mimi sijaiangalia mpaka muda huu.
 
tumblr_pcn5woUjYg1qm5w5wo3_400.gif

Madeepa Type.
hahahahahaaaaa uyo bwege madeepa ( madeera) vurugu lake lote akifika kwa beautiful lady Ae shin anatulia kama bata anapoongozana na mama yake..
ananikumbusha yeom jang kwenye emperor of the sea dhidi ya mwanadada jung hwa.
mhhhhhhhh mapenzi ni zaidi ya ugonjwa wa cancer ndio maana naogopa kuyakaribia.
fighting my brother ambaye hatuna uhusiano wowote mr yoo yeon seok
yoo-yeon-seok.jpg
 
IMG_9822.jpg


Hii Drama Huaga Hainotokagi Na Wala Huwa Siichoki! Labda Sababu Huwa Aipiti Muda Mrefu Bila Kusikiliza Ost Zake!
Natoa Ofa Kwa Wapenzi Wa Korean Entertainment Kesho Twendeni Simba Day!

dah mzuka wako wa simba day umekufanya utuwekee poster lenye maandishi ya kijapani.
au ndio team madeepa?
mungu azidi kumponyesha ugonjwa wa nasopharyngeal cancer na pia awape afya wagonjwa wote wanaohangaika kurudisha afya zao.
Kim-Woo-Bin.jpg
 
11/08/2018
unaikumbuka Voice drama season 1?

season 2 inategemewa kuanza siku ya leo.
muigizaji mkuu wa kike ameendelea kuwa ni lee ha na lakini muigizaji mkuu wa kiume amebadilika kutoka jang hyuk hadi lee jin wook.
daebak, hawa OCN hawanitakii mema kwa sababu haiwezekani wiki iliopita imemaliza drama ya life on mars halafu wiki hii inaanza criminal drama nyengine.
d521db6d087d.jpg
 
Back
Top Bottom