kampeni yangu ya kuzifuatilia drama zilizokuwa zimekamilika itaendelea kama nilivyojipangia.
imenichukua siku tatu kuangalia episode 16 za drama inayoitwa
misty.
sijui nitakuwa mwanamme mvumilivu kama bwana yule?
sidhani kama nitaweza kiukweli.
mchepuko wa zamani :hivi kweli unampenda mume wako
mwanamke: anasita kwa muda halafu anajibu,
namhitaji (nyakati hizo alikuwa anahitaji nafasi ya msemaji mkuu wa ikulu)
halafu jamaa anayehitajiwa ndio anashuhudia kinachoendelea ndani ya gari, siku aliyobahatika kuiona black box yalikuwa ni maumivu makali sana.
kweli kupenda ni zaidi ya utumwa.
ukiondoa
blood, misty, na dong yi kuna drama nyengine nzuri aliyoshiriki
jin jin hee kwa aliyebahatika kuangalia?
nakumbuka mwanadada
Nifah aliwahi kusema ni mshabiki wa
jin jin hee ila sijui amekimbilia seoul baada ya vyuma kukaza
nataka niiangalie
chicago type writer drama ya mwaka 2017
lee seung chul = painful love ost 1