Gwanggaeto the Great
JF-Expert Member
- Apr 14, 2018
- 831
- 1,792
Hatimaye nimeimaliza Safari iliyokuwa ndefu sana, Safari ya Episode 200.
Kituo cha Taifa (SK) KBS, iliwaghalimu miezi 24(2000-2002) kuirusha Drama hii.
Daemusin aliyenipa assignment hii, kama siku mnukuu vibaya... alisema, " aliianza 2015 - 2017"
Lakini miye niliianza June 1 ya mwaka 2019 kwahiyo ni kama miezi 11 na siku 26.
Nadhani nadhani yeye afanyae assignment na kuzimaliza kwa wakati humtia moyo mwalimu wake.
Hii Drama kuna baadhi ya washiriki nilikuwa nishawasahau Sura na uhusika wao kwa jinsi Drama ilivyokuwa ndefu.
Nimejifunza mengi sana humo ndani hasa kuhusu U-budha na Sutra zake, na masuala mengine yakawaida kabisa, hasa yaliyowatokea Wababe wetu Gung Ye(Mwanzishi wa Goryeo according to the Drama) na Kyeon Hwon ( Mfalme wa Bakje)
Lakini hii Drama ilikuwa imejawa sana na Watu wenye Vipaji na Ma- Genius; Choi Ung(Minister of Military in Goeyeo, Choi Son woo( Vice Prime minister of Bakje), Choi Jimong( Royal Advisor in Goryeo mzee wa nyota na ndoto), Captain Taepypng ( Military Advisor in Goryeo) na wengine wengi.
Bato ya Waziri mkuu msaidizi wa Bakje na Dogo mwenye akili nyingi( Choi ung), Hawa jamaa walikuwa wanapendana kinoma licha uhasama wa Nchi zao, na walikuwa wanajuana kuwa wote ni wakali .
Lakini Urafiki wa Kyeon Hwon kwa Wang gun n.k
Uovu wa Gung ye ndio unakumbukwa zaidi kuliko Wema wake hapo awali.
Hii kitu lazima nitairudia huko
mbeleni.
inaitwa... Emperor Wang Gun