Naheshimu ukisemacho, lakini Sidhani kama kuna mtu alikuuliza ndugu, na pia hii ni thread kwa Wapenzi wa Korean Drama. Nadhani kama hawakuvutii huna haja ya kuingia mahala ambapo huvutiwi napo. Mfano mie si mpenzi wa series au single za kimagharibi, bali navutiwa zaidi na Series na single toka Asia ya mbali, kwa kujua hilo wala sijawahi kwenda kuandika kwenye thread au kufungua thread yao sababu najua sipo interested na movie toka huko. Kwahiyo naheshimu mawazo na mapenzo yao. Anyway karibu kama utaanza kuvutiwa nao, nasi bila hiana tutakupa list.