mimi nadhani alimpenda zaidi Taek kuliko Jung-Hwan na upendo dhidi ya taek ulianza tokea siku ya kwanza walipokutana (udogoni kwao), si hivyo tu hata ukiangalia mwenendo wa matendo yake dhidi ya Taek yalionyesha heshima, utulivu pindi anapozungumza naye na ule unyenyekevu wa kisichana wenye aibu ndani yake kuliko anapokuwa na Jung Hwan (iwe kimazungumzo, kimatembezi au kimahitaji)
kwa kuangalia mlolongo wa makuaji yao naweza kusema kwa ufupi
Duk-Sun alimchukulia jung hwan kama ni rafiki jirani wa kiume kwa maisha yake yote ya utoto na mwanzo wa puberty stage kuliko mwanaume.
msamiati wa timing utumike baada ya kubaleghe kwake na hapo pia deok sun bado aliendelea kumpendelea Taek kuliko jung hwan aliyekuwa na kila kitu (kazi ya uhakika, familia yenye kipato, elimu, muonekano).
mfano angalia zawadi ya gloves, ni nani kati ya hao wawili aliyempelekea gloves sahihi alizozipenda (nafikiri mmoja wao alichelewa lakini bado alimpelekea zawadi sahihi), cha ajabu ikaheshimiwa na kuthaminiwa ya bwana yule
- kama nitakuwa sahihi deok sun aliogopa hata kumwambia taek ambebe mgongoni kwa kukhofia kumuumiza (khofu juu ya kile ukipendacho kishije kuharibika) lakini kwa jung hwan ilikuwa ni tofauti
- hakupenda kumuona Taek akinywa vinywaji vikali mfano wa pombe lakini kwa jung hwan ilikuwa ni tofauti