naendelea kujifunza taaluma ya biashara kwa njia ya maigizo, kuna project inaitwa
the great merchant kim man deok ndio naangalia kiuvivu (stori yake si nzuri sana).
Inakupa hadithi ya mwanamama
kim man deok aliyepata kuishi ndani ya tawala ya Joseon kuanzia mwaka 1739 hadi 1812, akiwa na miaka 12 ndani ya visiwa vya Jeju alilelewa na mkuu wa gisaeng (wanawake waburudishaji) na hatimaye akasajiliwa kama ni gisaeng anayetambuliwa na serikali mpaka hapo alipojitambua ya kwamba kumbe ana kipaji kikubwa sana cha kufanya biashara kuwahi kutokezea ndani ya korea.
tukio kubwa na la kukumbukwa alilolifanya nyakati za uhai wake na kuacha taathira njema na ya kukumbukwa kati ya kizazi kimoja hadi chengine mpaka anatengenezewa drama ni hili:
mwaka 1795 ambao ulikuwa ni mwaka wa 19 wa kiutawala wa mfalme jeongjo (Yi San), visiwa vya jeju vilikumbwa na tatizo la ukame uliopelekea jamii kubwa ya raia kudumbukia kwenye umasikini wa njaa, huyu mama aliamua kuziuza asilimia 90 ya asset zake na hatimaye kiwango hicho cha mali akawazadia wananchi.
kwa mujibu wa wikipedia wanasema hicho kiwango cha mali alichokigawa kama utapiga thamani ya fedha za muda huu unapata won billioni 70 au $60 million dollars (takribani billioni 138 za kitanzania kama nitakuwa sahihi).
... at Dramanice
dramanice.sh