Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Oiii thanks man mzigo upo vzuri
Hiyo ni noma nina masaa 24 ya bure bado ntaongeza mengine acha tuwatie hasara
Screenshot_20220322-151015.jpg
 
The King of Tears Lee Bang Won [emoji1487][emoji1487]
Nimenyoosha mikono juu, kwa miaka mingi nimekuwa nikiitafuta drama ya historical kali ya miaka ya hivi karibuni, naweza sema ndio hii niliyokuwa nikiitafuta!
BhaaaaaaasssssssKatika historical drama ambayo sijaikubaki ni pamoja na hii, mwanzo niliielewa ila kadri inavyoendelea mpaka nimejikuta naichukia juzi nilikuwa naangalia episode za 19 na 20 niilishindwa kumaliza niakaachana nayo kabisa, kama una nyingine nzuri nipe niitafute!!!!
 
ROMANTIC DOCTOR, TEACHER KIM

ROMANTIC DOCTOR, TEACHER KIM 2

INTROVERTED BOSS

THE BRIDE OF HABAEK

THE HEIRS

LOVE IN THE MOONLIGHT

FIGHT FOR MY WAY

CRASH LANDING ON YOU

I’M NOT A ROBOT
umeshakuwa professor, niruhusu nikutunuku hiyo heshima.

hivi maporofesa nao wanafanya graduation, kama ni hivyo ya kwetu sisi itafanyika kwenye mji wa Kyiv.

nimepata 5/9 kwenye list yako.
 
Linapokuja swala la VPN FORCE huku kwangu zinakuja server mbili tu yaani USA na INDIA, nyingine zote zinahitaji malipo. Hiyo sio mbaya, ila tatizo hizi server mbili zina disconnect sana yanu haipiti dk 5 ni lazima uconnect tena.

Hii shida ni kwangu tu ama ni kwa wote? Au labda kuna muda maalumu ambao hii shida haijitokezi??
 
Linapokuja swala la VPN FORCE huku kwangu zinakuja server mbili tu yaani USA na INDIA, nyingine zote zinahitaji malipo. Hiyo sio mbaya, ila tatizo hizi server mbili zina disconnect sana yanu haipiti dk 5 ni lazima uconnect tena.

Hii shida ni kwangu tu ama ni kwa wote? Au labda kuna muda maalumu ambao hii shida haijitokezi??
Nahisi kwako tu ila mimi natumia hata masaa mawili bila kuwa disconnected ila nahisi ukiconnect halafu ukaiacha simu kwa dakika kadhaa bila kutumia inajikata
 
The King of Tears Lee Bang Won
emoji1487.png
emoji1487.png

Nimenyoosha mikono juu, kwa miaka mingi nimekuwa nikiitafuta drama ya historical kali ya miaka ya hivi karibuni, naweza sema ndio hii niliyokuwa nikiitafuta!
Bhaaaaaaasssssss
mwishoni mwa episode 20
lady min (mke wa bang won) na kabila lake(min clan) ni suala la muda tu kabla na wao hawajaingia kwenye mdomo wa mamba, bang won amekuja na mkakati wa kuondoa vikosi binafsi vya ulinzi vinavyomilikiwa na makabila pamoja na familia maalum(tumeona huko nyuma mfalme taejo aliwatunuku wanawe wanajeshi kwa ushauri wa malikia aliyekuwa na lengo la kuwatengenezea mazingira ya kupumbazika na kufanya uhaini). hapo nyuma sambong alikuja na wazo la kufuta wanajeshi binafsi(military disbandment) lakini akapata upinzani mkali kutoka kwa lee bang won, leo hii bang won anataka kupita mule mule alimopitia adui yake sambong ndio maana kabila analotokea mke wake hawamuelewi juu ya mpango wake huo na khofu yao bila ya shaka wanaamini kutokuwa na majeshi ya kulinda kabila lao ni sawa na kuchomolewa maarifa na ufahamu kwenye vichwa vyao na watakuwa chawa wa mfalme milele, wakati baba mkwe dhumuni lake haswa ni kuitawala joseon kupitia sketi ya mwanawe wa kike (wanaume wa scotland nao wanavaa sketi) huku wakipata msaada wa kiulinzi na kifedha zitakazowawezesha kutawala nafasi zote nyeti za kiserikali.wakati yeye anawaza hivyo upande wa pili anaamini kwenye uendeshwaji wa serikali itakayoongozwa na nguvu ya mtu mmoja (hata kuwa kama baba yake aliyetawaliwa zaidi na sambong pamoja na malikia sindeok). lady min anamwambia bang won nyakati za shida tulikuwa pamoja, tulicheka pamoja pale tulipopatwa na jambo la kufurahisha, tulikejeliwa na kudhihakiwa pamoja. leo wachukua maamuzi muhimu ya kuongoza nchi peke yako, kama huwezi kuishawishi familia yangu juu ya mpango wako wa kuondoa majeshi binafsi basi nishawishi mimi, utakaponishawishi mimi ni sawa na kuwa umeishawishi familia yangu. hivi umesahau kuwa nusu ya mafanikio yako yametokanwa na mimi(akiwa na maana ya kabila lake).aigooo marehemu khadija baramia aliwahi kuimba wimbo wake wa taarab asilia..... njoo njoo mpenzi wangu njoo, rudisha yako imani wachochea moto ukija kuwaka mzimaji nani, eti lady min?....umeshasahau kuwa mume wako amewaua ndugu zake, amemfungia baba yake na kumuondoa ndani ya mji kaka yake. mara hii atazitafuta shingo za ndugu zako wawili na baba yako..... nilifikiri naongea na lady min. kumbe naongea na mkorea wa makunduchi. basi naambatanisha na samahani isiyoonyesha kujutia kosa langu.
 
😂😂😂😂😂Dae bana,niliendana na kasi zenu humu enzi naingia kdrama world nilijiona nimechelewa sana.
je kushafika hiyo safari yako, nimemkumbuka yule mchumba wake khantwe aliyesema ameangalia drama zote za wakorea. sikukuu ya karibia, ulininyima wali wa kirisimasi, hasira hazijaisha. hutaonja keki wala sambusa za dae. hata muhogo wa ramadhan hutauonja... bado nimenuna kama putin wa magogoni ikulu
 
Back
Top Bottom