Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hii nadhani nimeitazama zaid ya mara tatu hadi Pc ilopozingua

Hadi ost yake ipogo kichwani

Ingawa nliipenda ile ambayo ingekua coupl ya wazazi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] yaani mimi sikuipenda ile couple ilikuwa imechacha balaa. Ya watoto ndio ilikuwa nzuri sijui ni vile napenda characters waliochangamka...
 
The king and I drama
  1. Hutokuwa mwanaume wala hutokuwa mwanamke
  2. Hutoiona ladha ya kuwa karibu na mwanamke kimwili
  3. Hutokuwa na ukaribu dhidi ya familia yako.
  4. Hutokuwa na kizazi kinachotokanwa na damu yako
Bado tu wahitaji kuwa eunuch?
Ndio.

Hutojutia uamuzi wako?
Ndio sitojutia.

Aigoo.
Hii drama nimeiangalia episodes 5, nikajitia ujinga wa kwenda youtube kuangalia OST.

Nilichokutana nacho ni clip za tragic ending.

Nimebaki na swali, je niendelee nayo haliyakuwa hii drama ina episode 60 na kitu.
=======

drama inazungumzia zaidi maisha ya eunuch, kuanzia recruitments zao, kuajiriwa kwao royal palace, mamlaka yao, nguvu zao kwenye kuta za siasa, nguvu zao za kucontrol rasilimali za nchi, vita ya madaraka kati yao.

Hawa mabwana hawazai ila wanaruhusika kusajili watoto wa kuendeleza kizazi chao.

Kwa mujibu wa hii drama hawa mabwana walikuwa wanaoa lakini ndio hivyo masikini mabwana hawa walikuwa wanakatwa korodani (castration)

Ukatili wa hali ya juu sana.

Bwana huyu alitokea kwenye familia ya baba aliyehusika na uhaini wa kutaka kumpindua mfalme sejo, huyu sejo alikuwa mtoto wa sejong the great....

tofauti na baba yake huyu sejo alikuwa kama babu yake taejong.

Bwana yule udogoni kwake akapendana na binti, bwana yule prince naye akavutiwa na binti. Wote wawili walikuwa ni nobles ila yule alikuwa ni peasant.

Inaonekana mbeleni ilifungwa ndoa ya siasa kati ya binti na huyu prince ambaye baadae alitawazwa kuwa mfalme.

Uamuzi huo ulimuumiza sana bwana peasant, nadhani katika kuwa karibu na mwanamke akachukua uamuzi wa kuwa eunuch ili awe karibu na mwanamke ampendaye huko ikulu.

Sijui kimetokezea nini huko mbele, mfalme akatoa hukumu ya kifo kwa huyo mwanamke ambaye ni mke wake....mambo ya siasa hayoo.

Na aliyepewa amri ya kupeleka sumu kwa huyo mwanamke ni huyooo bwana eunuch.

Hatimaye binti akanywa sumu.


======

Unrequited love is love that is not openly reciprocated or understood as such by the beloved. The beloved may not be aware of the admirer's deep and pure affection, or may consciously reject it.
 
Hivi Park Eun Bin kumbe alianza kama child actor..sikubahatika kumuona au niseme sijamtambua.
Wa kitambo huyo kaanza kuigiza na miaka 7/8 ukiangalia The Legend wapo kama Young Versions za Damdeok na Kiha.

Kwenye Queen Seondeok pia walikuwa pamoja kama couple na kuna drama nyingine inaitwa Operation Proposal wapo pamoja.

Anyway Eunbin ana experience ndio maana anaweza cheza role yoyote akahit ukiangalia Secret Door,Father I'll Take Care Of You,Hello My Twenties na Judge vs Judge utaelewa
 
Kwani hiyo rain ikoje tupe short story
Ni drama inayonyesha tofauti ya romantic relationships za zamani za kipindi hiki, hivyo imechezwa kwenye eras tofauti. Inahusu wanafunzi (wanaojielewa) wa chuo ambao kila mmoja alimpenda mwenzie siku ya kwanza tu kuonana (love at first sight), lakini wote walikuwa na aibu kuonyesha hisia to each other. Mbaya zaidi walikuwa destiny yao ilikuwa kwenda different paths hivyo mpaka jamaa anatongoza rasmi muda wa kuondoka eneo walilokuwepo ulikuwa umefika..........
 
View attachment 2570197
Huyu msichana ni nani?
Kwa sasa ana miaka 33.

Mshindi atazawadiwa tenda ya kuwasha majenereta kwenye uwanja mkapa.
teh teh teh
Scene za historical dramas huwa zina utamu wake bwana, ila zile classes zao zilikuwa ni mbaya sana.

Fukiria high class walikuwa na mamlaka hadi juu ya uhai wa low class, yani kama kuku na mfugaji wake tu.
 
Hivi Park Eun Bin kumbe alianza kama child actor..sikubahatika kumuona au niseme sijamtambua.
Hatika wasanii walioanza kama child actors nawakubali sana hawa, na sijui wapo wengine waliowahi kuingia vizuri kama hawa.
The-Moon-Embracing-The-Sun-Kim-Yoo-Jung-Heo-Yeon-Woo-041221.gif
kim-yoo-jung-26012022-1-1.jpg
Yeo-Jin-Goo-260222.jpg
Screenshot_20230330-101953.jpg
 
Kweli nimeamini kila mtu na taste zake, kuna drama moja 'THE GLORY" ilipendekezwa humu na Inno nikacheki ratings zake nikaona zipo juu, nikaingia NKIRI nikakuta comments kibao za kuisifu, bwanaweeh mpaka sasa nipo episode ya pili ila sielewi kabisa kinachoendelea.

Sijua napata wapi tu drama ya moto kwaajili ya hii weekend.
 
Vipi Kim soo hyun humkubali? Yoo seung ho je?
Daaah huyo Yoo Seung Ho nilikuwa nimemsahau, namkubali pia na nadhani alikuwemo hata kwenye QUEEN SEONDEOK.

Kim Soo Hyun namkubali katika ukubwa wake kutona drama alizocheza hasa 'My love from another star" , sijawahi kuona drama yake ya utotoni.
 
Kweli nimeamini kila mtu na taste zake, kuna drama moja 'THE GLORY" ilipendekezwa humu na Inno nikacheki ratings zake nikaona zipo juu, nikaingia NKIRI nikakuta comments kibao za kuisifu, bwanaweeh mpaka sasa nipo episode ya pili ila sielewi kabisa kinachoendelea.

Sijua napata wapi tu drama ya moto kwaajili ya hii weekend.


The Glory kali
Hao villain wa humo balaa
Usi mzingatie sana FL usoni
Namna tu anavyoisuka revenge

Nipo hapa kuisifu[emoji1787]
 
Back
Top Bottom