Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Naboreka kwa kweli sioni drama kali zinazotoka recently nimejikuta nimezamia uzunguni
 
Na safari hii wamepika sana nyama. Intern kachapa kazi kubwa japo nipo episode ya pili
Halal food tumepata recipes za kutosha
Ingawa mi hata wakisema pork huwa na assume nyama na kuku tu taste ake
 
Najua wewe upo kwenye mysteries sana hizi soft ni kwa ajili yetu japo mimi kila genre natazama kikubwa maadili tu yawepo
Han Kyul Hata genre ya Romance naangalia sema za Romance sizipendi zile zenye utoto na ucomedi eti unakuta mlikuwa wapenzi utotoni mkapoteza eti mnakuja kukutana ukubwani mnaendeleza mahusiano zenu au unakuta main characters ukomedy mwingi mtu anafanya vitu vyakujitoa akili kwa kweli hizi kwangu hapana, Me napenda zile ambazo kwanza main characters wapo seriously, story nzuri na yenye matukio mengi yanayosisimua kumfanya mtazamaji uwe na shauku ya kutazama next episode pindi tu inapoisha mfano mzuri wa hizo Romance genre Fates & furious, VIP, dangerous wife, Secret love, The empress ki, bad guy,Vengeance of the bride n.k kitu pekee sipendi pia genre za fantasy
 
kwa upande wa legal dramas nafikiri kituo cha SBS wapo katika dunia ya peke yao. Wamekuwa na muendelezo bora sana wa uzalishaji wa dramas zenye maudhui hayo ndani yake.
  1. Good partner
  2. one dollar lawyer
  3. Innocent defendant
  4. judge vs judge
  5. While you were sleeping
  6. Hyena
  7. Why Her
  8. Remember
  9. Your Honor
  10. Whisper
  11. N.K
Najikongoja nayo Good Partner drama,
uvivu na uchovu mwingi, majukumu ya watu nayo yanakula muda.
hakukosea yule aliyesema ukitaka kula sharti nawe uliwe.

Jang Nara amegoma kuzeeka hata akiwa kwenye muonekano wa makeup

Wivu wa kijinga
View attachment 3092651
Apa umesahau Lawless Lawyer
 
Back
Top Bottom