Kwa Watanzania walio na malengo ya kuishi kutafuta kazi au kusoma nchini Ubelgiji au Uswisi someni hapa

Visa hakuna upigaji...labda unachanganya na passport
Kwann hakuna,sa'bu si inayo tumika si pesa na wapigaji wana taka pesa,kwamm naona passport ni very simple kuipata na nime ipata hii mpya,Visa km ya Canada na nchi za Scandinavia ndio balaa labda za UAE na China lkn kwingine kume kua na wajuaji wengi sana,Mm hua naishia kusilikiza baada ya hapo naona bora niendelee kupambana SADEC ambapo sasahv hakuna fursa km zamani,Lkn nahitaji sana niingie Nordic Sweden au hata Canada lkn duh kichwa kunauma
 
Sio upigaji mkuu ndo sera zao za immigration.Wengine ndo hivyo kama unaenda kuishi na kufanya kazi,kukupa Visa ni hadi uwe umepata kampuni ya kukuajiri huko,na kama kampuni hiyo inakudhamini na upande wa kupata Visa basi kuipata ni kugusa tu.Usisahau kuna charges mbalimbali pia throughout the process.Kuna nchi mfano Australia huwa zinatoa kabisa list ya occupation wanazohitaji kwao.Kama una nia ya kutafuta maisha na fani yako haipo miongoni mwa zilizolistiwa,nakuhakikishia huingii na kule hakuna mambo ya rushwa au cha juu.Nadhani yote haya ni kukufanya wewe usiende kubangaiza kule,kuhakikisha husumbui raia wao na vyombo vyao vya usalama.
Hata kama unaenda for vacation nadhani huwa wanacheki uwezo wako wa kiuchumi kujirizisha.Hii hata nchi za Scandinavia wanafanya.Na kama una ndugu au rafiki huko,watahakikisha kama yupo vizuri kiuchumi kuweza kukuhudumia wewe ndo wakuruhusu.Nadhani hii vijana ndo hupendelea kuitumia.Ukitimiza vigezo vyao,basi utapata Visa yako bila shida.
Kwa hiyo mkuu sanasana ni immigration policies za nchi husika na sio kubania kama baadhi wanavyodai.
 
Shukurani Nyingi sana kwako Bro
Nimeweza kuelewa vizuri na kwa undani zaidi maisha , vitu kikubwa na mambo mengi mazurli kuhusu Ubeligiji na uswizi umeshaelezea

Issue kubwa nilikuwa najiuliza kuhusu TUNDU LISSU walivyomuhudumia pia issue ingine ni jinsi dereva wake alivyowezakupata chance hadi akaanza masomo huko huko Ubeligiji . Kwa yale yote uliyoyaelezea nimeweza kukonect dot na dot na kupata picha kubwa sana sana
Pia unaweza kufànya mazoezi humo humo ndani yanasaidia kutoa stress .
Stay positive in every situation bro

THIS TOO SHALL PASS

My Kind regards to bro
Mkuu Mayor Slum pitia hapa hili lilikuwa moja la hitaji lako majuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeeleza vizuri kaka
 
Ahsante kaka na karibu pia
 
Passport ni rahisi sana kuipata na pia unaweza kutoa hongo wakaharakisha mchakato tofauti na Visa mataifa mengi huwa makini sana kutoa mpaka wajiridhishe kwenye vigezo vyao
 
Nyie mliopata fursa za kutangulia huko toeni miongozo mahususi kuwasaidia waafrika wenzenu conection za vyuo cheap,zenye course ambazo zinaweza kuwafanya Watanzania wanyonge ku afford,na wakifika huko wajilipue na fursa zilizopo huko na mwisho wa siku wa win.Ni rahisi kwa wazazi wengi kuwasupport watoto wao huko kwa masomo kwa vyuo ambavyo ni vya gharama nafuu.
Nikupe kisa kimoja hapa Singida,kuna mrombo alikuwa na shoeshine toka miaka ya tisini mwanzoni,aliajiri vijana wa kirombo kadha,kila baada ya mda flani alikuwa akiwatoa vijana hao wakiwa na akiba zao na wanafungua biashara kubwa.Hadi leo huyo jamaa ni tajiri,na kawatoa vijana kibao,na hiyo shoeshine inapiga kazi.
Nchi za wenzetu walitumia mianya hii kitambo na sasa wanalisha familia zao wakiwa huko.Watanzania uwe ndio mda wetu huu japo tumechelewa.
 
Hata Mimi niliwaza Kama wewe nadhani ndio maana TUNDU LISU waliamua kumpeleka huko na ona huduma aliyopewa na maisha anayoishi huko inaonekana kweli huko watu ni wakarimu na wanaupendo sana
Mtu Kama Mimi ninaependa kujichanganya nadhani huko kunanifaa zaidi
 
bandiko zuri kk na yote nayafatilia...kwa sisi km mwenye ki degree ka sheria kwa huko mchongo naona ni mgumu labda kufundisha kiswahili labda kwa jinsi uonavyo ebu tupe mazingira ya uzoefu kwa mtu kuja kufanya icho kitu huko na kufanya ilo zoezi km taasisi au wasemaje Parabora

HOT
 
Sina uzoefu na mfumo wa elimu wa huko nyumbani lakini nadhani kwa sheria mtakuwa mnasoma kwenda na mazingira ya huko nyumbani kitu ambacho ni tofauti na huku sheria imebeba mambo mengi ikiwemo ya kimataifa na kwa fani Kama hizo huku ni ngumu mno kupata kazi moja kwa moja.

Waafrica wengi hata waliosoma sayansi wakifika huku huanza kufanya kazi ndogondogo then wanajiendeleza kwenye fani zao au fani nyingine tofauti ili wakubalike kuajiriwa na mifumo rasmi ya kimataifa. ni ukweli kabisa hawa watu hawaipi uzito elimu inayotolewa katika baadhi ya nchi za Africa katika soko lao la ajira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…