Kuhusu kupata watoto wenye mahitaji maalumu:Katika mpango wa Mungu wa kupata watoto wakati mngine familia hupokea watoto wenye ulemavu wa ngozi,wasiiona,wenye ulemavu wa viungo nk mara nyingi hili jambo huleta maswali,maumivu,hofu ,kukataaa na hata kukata tamaa ukweli unabaki kuwa ndiye mtoto tuliyempokea na ni muhimu muhudumu aliyetoa huduma atoe taarifa mapema ili wazazi wafahamu na waendelee kukubaliana na hali hiyo, ulemavu mngine huchukua muda kujulikana ni vizuri wazazi baada ya kujifungua tujitahidi kuwachunguza watoto wetu wakati wa kuwaogesha ,kuwavalisha na kuwa nao ili kuweza kufahamu miili ya watoto wetu kuna vitu vingine vikipata uangalizi wa daktari mapema vinarekebishika na yale ambayo hayawezekane tunapata nafasi ya kuwaona wataalamu mapema na hakika watatuelekeza namna nzuri ya kuwapokea kuwapenda na kuwatunza watoto wenye hali hizo na kuendelea kumshukuru Mungu kwa zawadi ya watoto anazotupatia