Mimi pia sikubaliani na virutubisho vya kuongeza kwenye vyakula vya mtoto wala sikubaliani na kumpa mtoto vitamins unless kapimwa kakutwa na upungufu mkubwa wa madini fulani basi ndio mtoto apewe hayo madini/vitamin kama matibabu. naamini kabisa mtoto akilishwa mboga mboga, matunda, maziwa asilia ya mama au asilia ya ng'ombe (siyo ya kopo yaliyochanganywa na kemikali kadha wa kadha ) wanga bora (whole grains) na protini ya kutosha hasa ya mimea kama maharage, mbaazi, dengu nk lazima atapata virutubisho vyote vinavyotakiwa mwilini, mboga organic na matunda yanapatikana kwa urahisi sana Tanzania, wakulima wengi hata majirani zetu wanalima mboga kwa kiasi kidogo hazipuliziwi madawa. Matunda mengi ya msimu huwa hayahitaji kupuliziwa madawa au mbolea za sumu.
Menu hii simple lakini inaweza kumpa mtoto wa miaka 4 na kuendelea karibu mahitaji karibu yote ya virutubisho kwa siku:
Asubuhi :uji wa ulezi uliopikiwa kwenye maziwa kikombe kimoja,
Snack ya asubuhi: embe au tunda lolote la msimu kwa snack
Mchana: ugali wa dona mchicha, na dengu zilizoungwa na nyanya kitunguu na nazi
Snack ya mchana: salad ya tango kitunguu na hoho
Usiku: ugali wa dona, dagaa aliyeungwa kwa nyanya, vitunguu, mchicha; na juisi ya nanasi au ya tunda la msimu isiyoongezwa sukari
kwenya protini tunaweza kubadilisha dengu na dagaa kwa maharage, nyama, mayai, mbaazi, etc
kwa wanga asubuhi tunaweza kubadilisha uji wa ulezi na na viazi vitamu vya kuchemsha, majimbi, uji wa dona, etc na kikombe cha maziwa
mboga za majani na matunda zipo aina nyingi tu.