Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Samahani hapo nilijua mama ndio kapost nikasema mama mtoto kama nimekosea nisamehe
 
Anapata choo vizuri?akila unamtoa gesi vizuri chunguza kwa makini na fanya marekebisho kwa kuhakikisha anashiba angalia kama nawe unakula vya kutosha ili utoe maziwa ya kutosha ashibe mtoe gesi na mpunguzie nguo pia maombi kwa mtoto ni muhimu muombee
Choo anapata vizur tuu, ngoja tuangalie suala la nguo na maombi kwasababu nimpeleka hospital zaidi ya mbilI wanasema mtoto hana tatizo. Asante kwa ushauri.
 
Mtoto wa wangu ananisumbua tangia juzi ameanza kulia yaan analia mpaka anageuza macho, nimempeleka hospital wamemchekI wanasema hana tatizo lolote, kiukwelI napata wakat mgumu sana hasa mama ake. Yaani siku nzima analia anaweza kuacha kulia mda flan tuu na hataki umlaZe kitandani, anataka abebwe mikononi mda wote.
Ni mtoto ambae ametimiza mwezi mmoja tuu, naombeni mnisaidie wenye uzoefu na hali hii.
 
Maadam nakusoma hapo ujue sijaelewa.....wa kwanza na wa pili lol haya mamito........ni kweli hata mie wangu nilimwogesha baada ya siku 3 niliporudi home lakini inaogopesha jinsi mdogo unakuwa unaogopa kumwangusha au kumkwarua na kitu

Haahahha, mkweee. . . .

Nimeshaongezaga namba 2. Yani ukimshindwa W unamrudisha tu nakupa mwingine. LOLZZZZZ
 
Haahahha, mkweee. . . .

Nimeshaongezaga namba 2. Yani ukimshindwa W unamrudisha tu nakupa mwingine. LOLZZZZZ


Aiseee hongera sana mie sijajua hiyo habari njema...........na uzee huu najichagulia mpaka nishindwe mwenyewe nimefurahi sana kusikia hayo mpe salamu yangu nyingi
 
Maziwa ya ng'ombe kwa mtoto mdogo si mazuri sana humletea mtoto gesi na kuvimbiwa[/QUOTE]

sio hilo tu kubwa zaidi n kwamba mfumo wa kumengenya virutubisho ndani ya maziwa inakuwa haijakomaa kias ambacho unaipa kazi ya ziada iyo mifumo ili kufanya iyo kazi ya kumengenya, inashauriwa walau mtoto afikishe mwaka mmoja, au ukiamua kumpa bas hakikisha una dilute sana hayo maziwa
 
Maziwa ya ng'ombe kwa mtoto mdogo si mazuri sana humletea mtoto gesi na kuvimbiwa

sio hilo tu kubwa zaidi n kwamba mfumo wa kumengenya virutubisho ndani ya maziwa inakuwa haijakomaa kias ambacho unaipa kazi ya ziada iyo mifumo ili kufanya iyo kazi ya kumengenya, inashauriwa walau mtoto afikishe mwaka mmoja, au ukiamua kumpa bas hakikisha una dilute sana hayo maziwa[/QUOTE]

Kwa watu wazima ipo condition inaitwa "lactose intolerance". Inafika mahali mtu mzima hawezi kunywa maziwa mengi bila kupata side effects...
 
huyo mwenye lactose intorelance anakuwa na upungufu wa kimengenya kiitwacho lactase.

Kwenye maziwa kirutubisho kisicho rafiki kwa mtoto ni protein, maziwa ya ngombe yana kiwango cha juu zaidi. Ndo maana product zote za maziwa kwa mtoto alie na umri wowote angali ameanza kula anaweza tumia, ispokuwa maziwa yenyewe, na tatizo hasa ni kiwango cha juu zaid cha protein
 
huyo mwenye lactose intorelance anakuwa na upungufu wa kimengenya kiitwacho lactase.

Kwenye maziwa kirutubisho kisicho rafiki kwa mtoto ni protein, maziwa ya ngombe yana kiwango cha juu zaidi. Ndo maana product zote za maziwa kwa mtoto alie na umri wowote angali ameanza kula anaweza tumia, ispokuwa maziwa yenyewe, na tatizo hasa ni kiwango cha juu zaid cha protein
Tiba yake ninini kwenye hili?
 
Haina tiba. Zipo baadhi ya njia za kuishi na hili tatizo mojawapo ni kupunguza matumizi ya maziwa na vitu vyote vitokanavyo na maziwa sababu ndani ya maziwa na vitu vtokanavyo na maziwa mna sukari inayosababisha ilo tatizo. Unashauriwa pia kuonana na daktari kwa maelezo zaid
 
Kwakuwa hii ni mada ya watoto ningeomba kuongelea kitu tofauti kidogo lakini kinachohusu watoto
Ni hili jambo la kuwavulia watoto nguo zetu za ndani mbele yao na kuziweka hovyo
Jana tulikuwa kwenye shughuli ya kutoa posa mahali fulani, tukiwa tuko tayari pale kwa wenyeji wetu shughuli inaendelea ghafla alitoka mtoto chumbani na chupi ya mamaake kaivaa kichwani....kwakweli haikuwa siku nzuri kabisa kwa sisi wageni na wale wenyeji wetu
 
Back
Top Bottom