Kwa wenye Uzoefu na Biashara ya Vituo vya Mafuta [Fuel Stations]

0719357919
Fundi Canopy na Matenk. Ukiwa serious mtafute huyo fundi atakusaidia ni Mzuri na mwaminifu. Matenk usipopata fundi mzuri yakawa na vilinkage yatakupa hasara sana kuvuja mafuta na hutaona kwa kuwa yatakuwa yamefukiwa. Sasa kwa kuwa Fedha bado ya kuunga unga Anza kutengeneza matenk huku ukijenga Ofisi mdogo mdogo maana Ofisi haiitaji Fedha nyingi kwa wakati mmoja
 
Mkuu, kuna kitu unakijua zaidi ya ulichoandika, ongezea ongea maneno
najua coz ni biashara nimejihusisha nayo illegal na legal so najua kwa kiasi changu some of my relatives wanamiliki hii biashara so kwa muda niliofanya kazi zangu za mafuta pamoja na kufanya kazi ktika ofisi za ndugu zangu nimejifunza kiasi
Mimi napenda kushauri kiuchumi+ ukwel ni sekta nzuri kuwekeza lakin inahitaji uzoefu,umakini+ nidhamu bila kusahau ubunifu wafanya biashara wengi tu sio mmoja wanaingia na mitaji full na wanashindwa kuindeleza so kwa huu mtaji wa ndugu yetu si mbaya wala si mdogo unaweza ujafanya kitu kizuri lakin tu kimkakati ukikaza sana
 
kaka umeandika kidaftari zaidi hio pesa kwa mutu mwenye nia anafanya kazi ingawa itamchukua muda
 
kaka umeandika kidaftari zaidi hio pesa kwa mutu mwenye nia anafanya kazi ingawa itamchukua muda
Mie nimejenga, BOQ ya injinia ilikuwa mil 350 ila ujenzi imefika mpk mil 500. Ila changu kikubwa kina majengo mengi, Kuna mgahawa, supermarket, ATMashine room mbili, Gym and fitness, car wash, car service na barbershop. Na nimetumia miaka miwili pesa imelala ila kimeanza kufanya kazi, return naona ndani ya miaka mitatu nitakuwa bilionea
 
Kwanza kuna aina mbili ya vituo vya mafuta Filling station na service station. Filling station unapaswa kuwa na eneo lisilopungu 600sq.m. wakati service station unapswa kuwa na eneo lisilopungua 1,150sq.m

KAma ni filling station basi unatakiwa kujenga jengo la ofisi, changing room, toilet. Ambapo kama vifaa vya ujenzi sio ghali hiyo fedha onatosha na kubakia.

Unapaswa kujenga canopy pamoja na kumwaga zege eneo lote la kuingilia kituoni pamoja eneo la canopy zege lisilopungua 9inches.

Matank ya mafuta kama ulivyoshauriwa hapo juu walau 30,000 each. Mafuta hayapaswi kuisha kwemye tank.

Vibali na mtaji wa mafuta.

Mtaji wa Mafuta unaweza kuingia mkataba na wauzaji wakubwa wakakuletea on credit au ukachukua mkopp bank. Hii itawezekana kama utakuwa na hati ya eneo la hiyo station.

Basically ni mradi mzuri sanasana kama utapata sehemu strategic. Kama utataka ufanyie feasibility study tukupe ni actual costs tuwasiliane inbox
 
Shukrani kwa ushauri wako Mkuu, nitazingatia.

Na vipi ishu ya faida, naweza kurejesha gharama zangu baada ya miaka mingapi wastani?

Kuna kituo kimoja nimekiona Dodoma, jamaa wanauza mafuta kwa gharama ya chini kiasi cha kama shilingi 50 - 78 pungufu ya vituo vingine kwa lita moja.

Inawezekana hao jamaa wanaagiza wenyewe nje ya Nchi?
 
Shukrani Chief

Eneo ninalo la kutosha, ekari 5 ni approximately mita za mraba 24,000 kwahiyo linatosha kabisa.

Hofu yangu ilikuwa kwenye huo mtaji na namna hiyo biashara kama ni practical au inaweza kunipotezea hela yangu.

Kama kuna supplies wanaweza kunikopesha mzigo then nikarejesha hela baada ya mauzo kumbe naweza kufanikisha lengo
 
Sio GBP hao?
 
Huenda uliamua kujenga kwa kutumia mafundi wazoefu wa mtaani (Local Fundis).

Njia ya Force account imeonekana ina okoa gharama sana kuliko kutumia Mkandarasi
 
Mimi mwenyewe nipo kwenye construction industry kwa miaka kadhaa sasa, nadhani kuna haja ya kupata mafundi wenye uzoefu na aina hii ya miradi then tuta share knowledge.

Hapo pia nikipata watu wenye uzoefu na hii biashara hope naweza kujifunza mengi na pengine nikaondoa wazo la uoga wa hii biashara
 
Kwamba hiyo 50M siwezi kujenga hizo items chache muhimu hata kama nikitumia mafundi yaani Force Account?
 
Asante kwa mchango wako Mkuu.

Nitafanya mawasiliano na Mdau.

Hata kama itanilazimu kujenga kwa miaka 2 lakini nimeshatia nia lazima niikamilishe hii project
 
kaka umeandika kidaftari zaidi hio pesa kwa mutu mwenye nia anafanya kazi ingawa itamchukua muda
Mkuu amenitisha sana kwa gharama hizo, Ina maana nitahitaji zaidi ya miaka 2 hadi 3 kuianza hadi kuikamilisha project yangu 🙆
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…