Kwa wenye Uzoefu na Biashara ya Vituo vya Mafuta [Fuel Stations]

Kwa wenye Uzoefu na Biashara ya Vituo vya Mafuta [Fuel Stations]

Mzee wa Economics it's a monopolistic market.
Uoga wako ndio UMASIKINI wako.

Kama ndio hivyo kama usemavyo basi vunja bei asingefungua duka la nguo k.koo na bill Nas asingefungua duka la simu.
Maana yapo kibao k.koo

#YNWA
Kwa namna magari yanavyonunuliwa kila siku Bongo, hii biashara seems itakuwa na soko la uhakika.

Ukipita barabarani utaona miaka hii miwili ya hivi karibuni, watu wengi wanajenga vituo kila mahali

This means that, the grasses are greener out there 🤒
 
Habari za Muda huu Wakuu!

Kadri Umri unavyosogea, na majukumu yanapoongezeka ndivyo tunavyozidi kutafuta namna mpya ya kuwekeza ili kupata Uhuru wa Kiuchumi (Financial Freedom) kuelekea kwenye Umri wa Uzee.

Kwa muda mrefu nimekuwa nawiwa kufanya uwekezaji kupitia kujenga na kumiliki Kituo cha Mafuta (Fuel station ).
Nia ninayo, ila wasiwasi wangu ni kwenye mtaji halisi unaohitajika kufanikisha uwekezaji huu.

Binafsi nina milioni 50 ambazo nadhani naweza kuzitumia kwenye shughuli za awali ikiwemo Ujenzi n.k

Nina kiwanja nimenunua mahali ekari 5, na ni barabarani (Barabara ya Dsm - Mbeya).

Kwa kuwa mtaji wenyewe hautoshi, nafikiria kukopa Benki na kuweka dhamana Lodge yangu ya vyumba 8 niliyonayo.

Kuhusu vile vibali vya Nemc na Ewura, nina connection kule ya jamaa tunaofahamiana, kwahiyo nahisi nitatumia gharama kidogo kufacilitate mchakato.

Kutokana na ufinyu wa mtaji, nafikiria kujenga pump station 3 mbili za Petrol na Moja ya Dizeli. Pia ili kuongeza Wigo wa biashara, napanga kufunga compressor kwaajili ya upepo pia kujenga kibanda kwaajili ya kuosha magari (car wash).

Nitaanza na matenki ya kutunza mafuta ya ukubwa wa lita 10,000 kwa petrol na lita 5,000 dizeli.

Kwa kuwa ndiyo naanza biashara nitatumia magari ya kukodi kuniletea mafuta.

Ili kupata kujua gharama halisi za uendeshaji nitatenga shilingi milioni 15 kwaajili ya mishahara (ya miezi 8) ya pump attendants 5, mlinzi na Cashier ambaye nafikiria atafanya na kazi ya uwakala hapo hapo.

Karibuni kwa michango yenu ya mawazo ili kuboresha biashara hii, na pengine kunishauri kuachana na wazo hili la biashara kabla sijatumbukiza hela zangu.

Natanguliza shukrani za dhati 🙏🙏
Check jamaa flani ivii Insta wanajiita Energy Africa wanafanya consultation na kujenga vituo vya mafuta na wanatoa ufafanunuzi mzurii tuu
 
Mil 50 haitoshi na benk hawezi kukupa ela ya kujenga kituo kwa dhamana ya lodge maana kituo size unayotaka roughly lazima uwekeze mil 300 mpaka 350 hapo bila mafuta. Mfumo wa mafuta peke yake yaani canopy, matenk, pump tatu ,stand by generator, VFD system na zege la canopy kwa haraka lazima vile mil 200. Majengo ya iyo filling station na vibali lazima vikule mil 150 to mil 200. Pambana
Kitu kinachongeza gharama kwenye petrol station ni mahengo ya ziada na kiwanja otherwise ukiwa na 100M unajenga vizuri tuu
 
Kwanza kuna aina mbili ya vituo vya mafuta Filling station na service station. Filling station unapaswa kuwa na eneo lisilopungu 600sq.m. wakati service station unapswa kuwa na eneo lisilopungua 1,150sq.m

KAma ni filling station basi unatakiwa kujenga jengo la ofisi, changing room, toilet. Ambapo kama vifaa vya ujenzi sio ghali hiyo fedha onatosha na kubakia.

Unapaswa kujenga canopy pamoja na kumwaga zege eneo lote la kuingilia kituoni pamoja eneo la canopy zege lisilopungua 9inches.

Matank ya mafuta kama ulivyoshauriwa hapo juu walau 30,000 each. Mafuta hayapaswi kuisha kwemye tank.

Vibali na mtaji wa mafuta.

Mtaji wa Mafuta unaweza kuingia mkataba na wauzaji wakubwa wakakuletea on credit au ukachukua mkopp bank. Hii itawezekana kama utakuwa na hati ya eneo la hiyo station.

Basically ni mradi mzuri sanasana kama utapata sehemu strategic. Kama utataka ufanyie feasibility study tukupe ni actual costs tuwasiliane inbox
nilifikiria kumshauri afanye hivi au atafute kituo akodi pia itamsaidi
 
Shukrani kwa ushauri wako Mkuu, nitazingatia.

Na vipi ishu ya faida, naweza kurejesha gharama zangu baada ya miaka mingapi wastani?

Kuna kituo kimoja nimekiona Dodoma, jamaa wanauza mafuta kwa gharama ya chini kiasi cha kama shilingi 50 - 78 pungufu ya vituo vingine kwa lita moja.

Inawezekana hao jamaa wanaagiza wenyewe nje ya Nchi?
technique za kibiashara kk ni aproach inayotumiwa na wafanyaji biashara waliojikamilisha yeye ukute kalenga kupata faida labda ya usafiri tu yaani anapiga hela kwa mzunguko wa gari zake kibiashara maana yake ni nn sehemu aliopo huyo jamaa yawezekana kuna vituo vingi vya mafuta ko anaweza akawa kabaki na faida labda ya tsh30 tu kwenye mafuta lakin gari zake I mean truck zinazunguka sana yaani zinapiga trip nyingi kwenda depot so yeye pesa anapata kwwnye gari zake and sometimes namna ya manunuzi retailers wananunua cash so wanapewa discount meanwhile wengine wananunua kwa mkopo
 
Shukrani kwa ushauri wako Mkuu, nitazingatia.

Na vipi ishu ya faida, naweza kurejesha gharama zangu baada ya miaka mingapi wastani?

Kuna kituo kimoja nimekiona Dodoma, jamaa wanauza mafuta kwa gharama ya chini kiasi cha kama shilingi 50 - 78 pungufu ya vituo vingine kwa lita moja.

Inawezekana hao jamaa wanaagiza wenyewe nje ya Nchi?
ukumbuke lakin bei ya mafuta inakuwa influenced na umbali kutoka depot na some time kuna sheria ya petroleum industry kuhusu bei za mafuta na zina madhara kama usipofuata mind this is oligopoly market so single seller hawezi Fanya maamuzi sahihi bila kufuata maamuzi ya mwenzake( Kuna kitu kinaitwa kinked demand curve ) hii inaeleza nature ya hili soko
 
Shukrani Chief

Eneo ninalo la kutosha, ekari 5 ni approximately mita za mraba 24,000 kwahiyo linatosha kabisa.

Hofu yangu ilikuwa kwenye huo mtaji na namna hiyo biashara kama ni practical au inaweza kunipotezea hela yangu.

Kama kuna supplies wanaweza kunikopesha mzigo then nikarejesha hela baada ya mauzo kumbe naweza kufanikisha lengo
inawezekana but kuna million ways wewe kufanya hii biashara ni vile utavokuwa unajibidisha kujaribu kuielewa hii biashara
 
Mie nimejenga, BOQ ya injinia ilikuwa mil 350 ila ujenzi imefika mpk mil 500. Ila changu kikubwa kina majengo mengi, Kuna mgahawa, supermarket, ATMashine room mbili, Gym and fitness, car wash, car service na barbershop. Na nimetumia miaka miwili pesa imelala ila kimeanza kufanya kazi, return naona ndani ya miaka mitatu nitakuwa bilionea
Ndani ya miaka mitatu ntakua billionaire........#tukumbukane boss
 

Attachments

  • Screenshot_20230209-185751.png
    Screenshot_20230209-185751.png
    47.9 KB · Views: 45
Back
Top Bottom