Kwa wenye Uzoefu na Biashara ya Vituo vya Mafuta [Fuel Stations]

Kwa wenye Uzoefu na Biashara ya Vituo vya Mafuta [Fuel Stations]

so far biashara ya mafuta sio monopoly in oligopoly kwenye hii biashara kuna ewura ambao hupanga bei ya ukomo kwa wauuzaji wakubwa na ma retailer meanwhile monopoly bei anaipanga yeye monopoly
Sahihi kabisa, ingawa ule utaratibu wa mwenye uwezo kuagiza mafuta mwenyewe huenda ingepunguza sana gharama kwa walaji na wafanyabiashara wangepata faida maradufu
 
Habari za Muda huu Wakuu!

Kadri Umri unavyosogea, na majukumu yanapoongezeka ndivyo tunavyozidi kutafuta namna mpya ya kuwekeza ili kupata Uhuru wa Kiuchumi (Financial Freedom) kuelekea kwenye Umri wa Uzee.

Kwa muda mrefu nimekuwa nawiwa kufanya uwekezaji kupitia kujenga na kumiliki Kituo cha Mafuta (Fuel station ).
Nia ninayo, ila wasiwasi wangu ni kwenye mtaji halisi unaohitajika kufanikisha uwekezaji huu.

Binafsi nina milioni 50 ambazo nadhani naweza kuzitumia kwenye shughuli za awali ikiwemo Ujenzi n.k

Nina kiwanja nimenunua mahali ekari 5, na ni barabarani (Barabara ya Dsm - Mbeya).

Kwa kuwa mtaji wenyewe hautoshi, nafikiria kukopa Benki na kuweka dhamana Lodge yangu ya vyumba 8 niliyonayo.

Kuhusu vile vibali vya Nemc na Ewura, nina connection kule ya jamaa tunaofahamiana, kwahiyo nahisi nitatumia gharama kidogo kufacilitate mchakato.

Kutokana na ufinyu wa mtaji, nafikiria kujenga pump station 3 mbili za Petrol na Moja ya Dizeli. Pia ili kuongeza Wigo wa biashara, napanga kufunga compressor kwaajili ya upepo pia kujenga kibanda kwaajili ya kuosha magari (car wash).

Nitaanza na matenki ya kutunza mafuta ya ukubwa wa lita 10,000 kwa petrol na lita 5,000 dizeli.

Kwa kuwa ndiyo naanza biashara nitatumia magari ya kukodi kuniletea mafuta.

Ili kupata kujua gharama halisi za uendeshaji nitatenga shilingi milioni 15 kwaajili ya mishahara (ya miezi 8) ya pump attendants 5, mlinzi na Cashier ambaye nafikiria atafanya na kazi ya uwakala hapo hapo.

Karibuni kwa michango yenu ya mawazo ili kuboresha biashara hii, na pengine kunishauri kuachana na wazo hili la biashara kabla sijatumbukiza hela zangu.

Natanguliza shukrani za dhati [emoji120][emoji120]
Petrol station inatakiwa uangalie vitu vingi sana maana unaweza kujenga na usipate wateja kama kituo kitakuwa mbali na wateja
 
kwa nyoongeza tu hakuna hela rahisi broo nao wanakabiliwa na ushindani ukiangalia wanauza bidhaa tofauti tofaouti though ni hio hio dizel na ni hio hio petrol lakn zimetofautiana ubora mafuta wanayouza total,puma,Bp na gapco sio sawa na mafuta ya wauzaji wengine ingawa yote ni mafuta hapo nakuelekeza kwamba sio monopoly.yaani ni kama mapishi mwengine ataweka Nazi mwingine hataweka
Lakini si kuna agent mmoja anayeagiza mafuta kwa niaba ya Serikali, sasa huo utofauti wa ubora unatokeaje?
 
Mwenye ufahamu, je Ewura wanatoa vibali vya kuzalisha mafuta, KWA wanaotaka kutengeneza mafuta ya kuendeshea magari, mitambo na mashine mbalimbali
 
I have some experience ktk hio biashara nimefanya ktk petrol station kwa muda nimepata kufahamu biashara hii .
1. kitu cha kwanza sikushauri utengeneze storage tank ndogo kwa sababu tofauti tofauti umesema unaanza biashara kwa gari ya kukodi ni sawa unatakiwa uangalie namna ambavo utaongeza tija zaidi kwa mfano kama utakodi kipisi kufanyia delivery mind vipisi Vingi ni approximately 22000ltr sasa in case ukaagiza 10000ltrs za PMS na 5000 kulingana na storage facilities kibiashara unatakiwa uagize litre 1500 tu sasa hio space unayotaka kuicha huoni kama itakuongezea gharama za usafiri ?
2.ukijenga storage tanks za 10000 Ltrs kwa PMS(petrol) na 5000ltr kwa ajili ya PMS bado itafikia wakati itabidi uongeze ili kupunguza gharama na kuchukua faida zile za ghafla kulingana na trend ya biashara
Zipo gari za kukodi ndogo zina hadi lita 1500 sio lazima kuchukua kipisi.
 
Mil 50 haitoshi na benk hawezi kukupa ela ya kujenga kituo kwa dhamana ya lodge maana kituo size unayotaka roughly lazima uwekeze mil 300 mpaka 350 hapo bila mafuta. Mfumo wa mafuta peke yake yaani canopy, matenk, pump tatu ,stand by generator, VFD system na zege la canopy kwa haraka lazima vile mil 200. Majengo ya iyo filling station na vibali lazima vikule mil 150 to mil 200. Pambana
Labda aanze local kwa pump mbili moja ya diesel moja ya petrol.
Sio lazima ajenge tank chini atumie tank za lita elf moja za kusimamisha juu.
Kama zile za kuuzia mafuta ya taa vijijini.
 
Ni shihihi mkuu ila eneo langu lipo barabarani kabisa, Barabara ya Dsm - Mbeya.
acha mawazo mgando unaweza ukajikwamisha ukishililia wazo la kusema unakiwanja mind that unaweza ukawa nacho na bado usikitumie au bwana Grahams aww huenda unafell biashara hii haitaki mawazo kama yako umefenya utafiti mara ngapi mpaka umejiridhisha kuwa hilo eneo lipo shwari
 
Back
Top Bottom