Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Hii ni thread niliiandika mwaka 2015, na ni mojawapo ya thread ilisomwa sana humu JF, na hata kuandikwa gazeti la Mwananchi. Kutokana na umuhimu wake, nimeona niihuishe tena nikijua kuna wengine hawakuwahi kuisoma, na inaweza kuokoa uhai wao, hasa kwa wale wanaonunua magari kwa mara ya kwanza, na hawana uzoefu wa kuendesha gari barabara kuu za kwenda mikoani, japo wamekuwa wakiendesha gari mijini.
Ni vema pia hata kama wewe unatarajia kuwa abiria katika gari ya mtu ukaisoma,huenda ukamkumbusha huyo atakaekuwa akiendesha mambo kadhaa ili nyote muwe salama. . Kusoma hii thread liinaweza pia kuwa jambo la kuokoa uhai wa familia yako, kwani mara nyingi tunasafiri na familia zetu mwisho wa mwaka. Hata madereva wa gari za abiria kama mabasi ni vema mkasoma hii thread.
Ndugu zangu, ukiweza kuendesha gari hapa mjini Dar au hata mikoani mijini, haina maana utaweza kuendesha gari pasipo tatizo kwenye barabara kuu. Nimeshuhudia watu wengi sana waliokufa kwa sababu baada ya kununua gari walikuwa na mchecheto wa ku-drive kwenda kijijini kwao.
Kuendesha gari kwenye barabara kuu ni tofauti sana na kuendesha gari mijini. Kwenye barabara kuu challenge zake ni kubwa sana kwa sababu gari zinaenda kwa kasi, na pia kuna mambo mengi ya ghafla yanayoweza kujitokeza ambayo kama huna uamuzi wa haraka kama dereva utakufa tu kabla ya kufika mwisho wa safari yako. Ukifanya kosa hata dogo barabara kuu unaweza kufa, tofauti na mijini.
Kwa mfano, ku-overtake katika barabara kuu ni jambo linatakiwa lifanywe kwa makini sana. Vifo vingi barabarani ni overtake. Na pia kila unapoingia kona kali au blind spot kwenye barabara kuu weka akilini kwamba unaweza kukutana na kitu upande wako, basi linaloenda kasi, lori au trekta liloharibika, mifugo, shimo kubwa, mawe yaliyoporomoka, ajali nk. Pia unaweza kukutana ghafla na dereva mzembe anae-overtake kwenye kona na yuko upande wako.
Usithubutu ku-overtake sehemu ambayo huoni mbali mbele, au gri kadhaa zimefuatana bila nafasi ya kutosha kati ya gari na gari, hasa malori. Subiri wakati muafaka. Na unapo overtake, usikaribie sana gari unayotaka ku-overtake kabla ya kui-overtake. Na unapo-overtake kama una gari manual gear, rudi gia za chini kwanza ili kujenga spidi ya ku-overtake. Ni muhimu sana wakati unapovertake gari iwe gia ambayo inakupa acceleration power unapokanyaga accelerator. Angalia usiovertake ukiwa gia ya juu, kwa mfano gia ya tano, huku spidi ni dogo labda chini ya 80km/hr. Hutapata accelaration power ya kutosha. Kama uko spidi chini ya 100km/hr, rudi hadi gia namba tatu uanze upya acceleration wakati una overtake
Overtake kwa haraka, sehemu ambayo iko salama na unaona mbele zaidi ya mita 100, na ni vizuri gari unayoi-overtake dereva wake ajue unamu-overtake. Unaweza kumpigia honi kidogo ya kuibia kama kuomba - usipige kwa nguvu ukamuudhi. Epuka kuovertake sehemu ya barabara yenye mashimo, maana dereva wa mbele anaweza kurudi upande wako ili akwepe shimo wakati tayari unamu-overtake.
Siri moja ya ku-overtake salama ni kuwa na subira - overtake nzuri haitaki haraka. Be patient, na wait for the right place to overtake - subiri uwe sehemu inayofaa ku-overtake. Usiovertake kwa sababu tu kuna gari mbele yake inaenda spidi ndogo kuliko spidi yako - ambayo ni tabia mbaya ya madereva wengi wa mabasi.
Na pia kosa linaloua watu wengi sana ni ku-overtake kwa kukisia kwamba hakutakuwa na gari inayokuja upande wa pili zile sehemu ambazo huoni vizuri mbele. Hata kama barabara haina magari mengi usithubutu kukisia kwamba hakutakuwa na gari (gambling in overtaking).
Mara nyingi trafiki wanapiga fine ku-overtake sehemu zenye solid line( mstari wa katikati ya barabara ambao haujatenganishwa umechorwa moja kwa moja), japo mara nyingine ni kweli unaona uko salama ku-ovetake kwenye solid line. Kwa ujumla, sehemu zenye solid line sheria inasema usiovertake, na kama unaona unaweza kufanya hivyo uwe mwangalifu sana.
Jambo jingine la kuzingatia barabarani ni uchovu, - fatigue. Hili ni jambo jingine linaua sana watu wasio na uzoefu wa kuwa katika barabara kuu. Ukianza safari kati ya saa kumi na moja na saa moja asubuhi, masaa matatu ya kuanza safari ni magumu sana, usingizi utakuwa unakuja mara kwa mara. Simama, nawa uso, tembea, ruka ruka nk. Usijilazimishe na usifikiri kukodoa macho kutaondoa usingizi. Ukiona unapiga miayo kila baada ya dakika moja au mbili huo ni usingizi. Unaweza kutumia vitu kama kahawa au pipi kijiti (lollipop) zinasaidia sana
Utakaposimama mahali kwa chakula ukanywa bia - hata moja tu, ni mbaya sana, kwa sababu itakuletea sana usingizi. Epuka kula vyakula vizito kama ugali na maharage, au kula hadi ukashiba sana! Ukisikia usingizi simama upumzike, toka ndani ya gari, tembea kidogo, kabla ya kuendelea na safari. Kama ikibidi tumia Redbull (sio zaidi ya mbili kwa siku). Unapoendesha gari, ukiwa unasinzia unaweza kulala ghafla bila kujitambua, huwezi kuzuia!
Na jambo jingine muhimu sana la kukumbuka ni kwamba ukiingia barabara kuu, ukaendesha kwa muda fulani, akili yako inazoea spidi kali kiasi kwamba huoni tena kama unaenda spidi kali. Unaweza ukawa unaenda 140km/hr ukaona kama unaenda 80km/hr. Hili huwa mara nyingi linasababisha kuacha njia na kupinduka, au kuingia kona ukiwa na spidi kubwa na gari kupinduka. Nadhani umesikia sana ajali zinazosemwa zilitokea kwa sababu dereva alishindwa kumiliki gari - ni kwa sababu akilini dereva aliona haendi spidi sana,hadi alipojaribu kupunguza mwendo.
Na pia jambo jingine muhimu sana kukumbuka ni kwamba, unapoenda safari yoyote ya mbali ambayo utaendesha gari mfululizo kwa zaidi ya masaa manne, au kwa spidi zaidi ya 100km/hr, hakikisha tairi zako hazina umri zaidi ya miaka mitano, la sivyo utapata basti hata kama tairi inaonekana bado mpya kwa kuitazama. Tairi ikizidi miaka mitano haifai kusafiria safari ya mbali, japo unaweza ukaendelea kuitumia kwa safari za mijini. Kutumia tairi ya miaka sita kwenda mikoan labda gari isiwe na mzigo na usikimbie zaidi ya 100km/hr.
Kutokana na matukio mengi ya gari kusombwa na maji wakati wa mafuriko, ni muhimu sana kukumbuka kwamba kitu chochote chenye hewa iliyofungwa ndani kama matairi ya gari kitaelea majini. Hivyo, mara nyingi sana, hata kwenye maji yanayoonekana kuwa na kina kidogo, gari zinakuwa na mwelekeo wa kuelea kwenye maji mengi. Hii ni kwa gari zote, kubwa na ndogo. Hivyo ni muhimu sana kutojaribu kukatisha au kupita barabara ambayo imefurika maji, hasa maji yanayotembea. Suala muhimu la kukumbuka ni kwamba tairi zimejazwa upepo, hivyo ukipitisha gari kwenye maji gari itakuwa ina mwelekeo wa kuelea, na itahitaji nguvu kidogo sana kuisomba na kuipeleka nje ya barabara. Kama ikibidi kuvuka, basi toa upepo kwenye tairi, lakini unaweza kuharibu tairi.
Na kama itatokea umepita kwenye maji na gari ikitumbukia majini mara nyingi milango inakuwa migumu kufunguka kutokana na pressure ya maji kwenye milango. Ni vigumu sana watu kujiokoa kwa sababu ya kupanic. Ili uweze kufungua mlango ni vema usubiri maji yaingine ndani ya gari kwa kiasi fulani ili kubalance pressure ndani ya gari na nje, na milango itafunguka kirahisi. Kama vioo vilikuwa vimefungwa ni vizuri hata zaidi kwa sababu maji hayatajaa ghafla ndani ya gari, na kukupa muda wa kupanga jinsi ya kutoka na kujiokoa. Hivyo usipoteze nguvu nyingi kujaribu kufungua milango ikiwa pressure ya maji inakuzuia kufanya hivyo, kwa sababu utatoka nje ya gari wakati huna nguvu na pumzi ya kutosha. Ikiwa una kitu cha kuvunjia vioo, vunja vioo ili utokee dirishani badala ya kusubiri maji yajae ndani ya gari ili uweze kufungua milango. Unaweza pia kujaribu kufungua madirisha kwa kutumia power window au kidude cha kufungulia kioo. Kumbuka sio rahisi kufungua mlango wa gari iliyozama majini.
Gari ikizama majini jitahidi kuto-panic, jipe kama sekunde thelathini kutuliza akili na kupanga jinsi ya kutoka na kujiokoa, badala ya kutumia nguvu nyingi ambazo zitakuchosha kabla hata hujajaribu kutoka ndani ya gari na kuogelea kwenda juu. Pia watu hupoteza mwelekeo wa wapi ni juu na wapi ni chini wakizama na gari. Hivyo unaweza kufa kwa kuwa tu hujui uogelee kwenda wapi, hasa ikiwa gari ilitumbukia na kupinduka. Jambo la msingi ukizama na gari ndani ya maji, kabla maji hayajajaa ndani, ni kujipa muda kidogo wa kutulia, na kujua mwelekeo wa kwenda juu ni upi, kutegemea kama gari imegota chini au bado inaelea. Kama maji sio machafu na sio usiku, angalia mwelekeo wa mwanga uko wapi, huko ndio juu. Pia unaweza kuzifuata povu (bubbles) kwa sababu huwa zinaelekea juu. Ni muhimu sana ujue wapi ndio juu kabla ya kuanza kuogelea. Kabla hujatoka ndani ya gari ambako kuna hewa, vuta hewa nyingi, bana pumzi na kuanza kuogelea kwa kasi kwenda juu au kufuata mkondo wa maji.
Ikiwa unasafiri wakati wa mvua sehemu zenye kufurika kirahisi, huenda ni vizuri kuwa na na maboya ya kuogelea ndani ya gari, hasa kwa ajili ya watoto. Ni rahisi kumuokoa mtoto ikiwa amevaa boya la kuogelea. Haya yanapatikana kirahisi sana siku hizi. Kama una watoto nunua uwe nayo kwenye gari wakati wa kusafiri kipindi cha mvua.
Tahadhali nyingine kubwa juu ya kusafiri na watoto ni kwamba hata siku moja usithubutu kuwafungia watoto ndani ya gari lililofungwa vioo ili ukimbie mara moja kufanya shughuli fulani. Hii huwa inasababisha vifo kwa watoto au hata kiumbe chochote kilichofungiwa ndani ya gari, hasa sehemu za joto kama Dar ambapo kifo kinaweza kutokea baada ya dakika 20. Na pia kumbuka huwezi kujua nini kitakupata huko uendako; labda utapata mshituko wa moyo ukimbizwe hospitali au tukio lolote litakalokufanya ushindwe kurudi kwenye gari yako ambayo umefungia watoto ndani yake. Ikibidi kuwaacha watoto ndani ya gari basi acha vioo wazi na usi-lock gari - lakini kwa ujumla epuka kuacha watoto peke yao au mtoto peke yake ndani ya gari.
Kwa jumuia kwa ujumla, ikiwa mtu utakuta watoto wamefungiwa ndani ya gari, ita walinzi na watu wengine kama mashahidi, au polisi kama wapo karibu na vunjeni kioo cha gari ili kuokoa watoto. Siku hizi unaweza kupiga simu kuita Polisi kirahisi sana; piga namba 111 au 112 kutumia simu yako ya mkononi. Lakini msisubiri hadi Polisi wafike ili kuvunja vioo - mnaweza kuchelewa kuokoa watoto au mtoto.
Nimeona niseme haya kwa sababu nawapenda ndugu zangu. Sitaki mufe barabarani au mniue mie na familia yangu. Wapeni taarifa wengine ili tuzidi kuepuka vifo hivi vya barabarani ambavyo vingi vinazuilika.
Neno langu la mwisho, ili uendeleee kuwa salama barabarani ni kwa lugha ya kiingereza; BE PATIENT kwa lolote unalotaka kufanya ukiwa unaendesha gari. Wakati wowote ukikalia usukani, uwe safari za mjini au kwenda mikoani, kuna siri moja tu ya kufika salama, kuwa na subira, be patient. Zingaitia hilo, utakuwa salama.