Kwa yaliyomkuta rafiki yangu sitajaribu kuoa

Kwa yaliyomkuta rafiki yangu sitajaribu kuoa

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
2,932
Reaction score
4,544
Mke wake alianza kubadilika tabia akanifuata na kuniomba ushauri,nikamuuliza kulikoni? akasema ni mara ya pili sasa mkewe anambwagia mtoto na kwenda misele isiyo na kichwa wala miguu,akimwambia aondoke na mtoto mwanamke anakuwa kiburi,anakaidi na kuondoka akimwacha mtoto analia,tena ndo first born huyo mtoto,jamaa akaamua kufuatilia ili ajue kulikoni,amefanya u spy kwa miezi 6.

Jana tena mwanamke akaondoka kama kawaida yake na kumuacha mtoto akilia,jamaa akanipigia simu kuwa niende haraka kumpa kampani ya kumfuatilia wife wake,ilikuwa saa 3 usiku, kwa kawaida mke wa jamaa huaga kuwa anakwenda kwenye hisa(michezo wachezayo wanawake wengi mjini) tulipofika kwenye ile nyumba ambayo ndo mara nyingi hupenda kwenda katika hisa,tukakuta hayupo,jasusi wa jamaa aliyemuweka kwa kazi ya kum spy.

Mkewe,akatuelekeza aliko shem,jamaa akashindwa ku drive, ikabidi nishike sterling, looh kufika tukavamia nyumba ya mgoni na kumkuta shemeji yupo uchi kama alivyozaliwa, jamaa kazirai, nimekesha hospital, shemeji kakimbia sijui aliko.

SITAKI KUOA.
 
Yaani unajifunza uongo kwa stori kubwa sana. Kama mlikuwa na baunsa wa kumfuatilia, kwenye hisa mlifuata nini? Halafu mlipomkuta uchi, walikuwa kichakani ama nyumba haina hata mlango?

Tupe hadithi zenye akili bwana. Kwanza huyo rafiki yako ana gari model gani? Ina cc ngapi? Consumption yake ikoje? Maximum speed? Tuanzie hapo
 
Kiboko! sasa ukishajua type ya gari na cc ndo itakuwaje au unataka kujua Ana drive gari gani
Lmfao....!
 
Sitaki kujua kama stori hii ni ya kweli ama la. Ila mimi nnachokijua ni kwamba mwanamke akishahamua kuhamisha akili yake huwa anakua kama chizi na hakuna utakachomuambia akuelewe. Ni hayo tuu.

True that
 
Kama mliweka spy kwa nini mhusika asizimie akiwa kwake hadi kwenye hisa ? Ina maana alikuwa anaspy fake asiyejua kutoa taarifa??? Mlipataje uwezo wa kuingia sehemu pasipo vikwazo kama milango , na watu waliozunguka wahusika
 
Sioi Leo, Sioi Kesho, Keahokutwa wala Mtondogoo,

Sioi Mchana, Sioi Usiku wala Majogoo.

~FA
 
Kama mliweka spy kwa nini mhusika asizimie akiwa kwake hadi kwenye hisa ? Ina maana alikuwa anaspy fake asiyejua kutoa taarifa??? Mlipataje uwezo wa kuingia sehemu pasipo vikwazo kama milango , na watu waliozunguka wahusika

Jamaa kasema wamevamia,
Ni juavyo uvamivi sio rahisi kama kuchuku juice kwenye jokofu. Ila kwenye hoja ya spy, mmh!!?
 
Back
Top Bottom