Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Ni wazi pesa za wananchi zimetumika kwenye Tume hii ya Mh Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande hivyo wananchi tungetamani kuona matokeo chanya ya utekelezaji. Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makamanda wa Polisi Mikoa na Wilaya na Taasisi zote zinapaswa kuzingatia maelekezo ya Rais ambaye ni Mkuu wa Nchi kuhusu utekelezaji wa mikakati na mbinu iliyoibuliwa kwenye mipango hii.
Lakini kwa masuala haya yaliyotokea ndani ya Jeshi la polisi kwa mwaka 2023/ 24, ni kama vile Jeshi la Polisi linamkwamisha Rais Samia kwa makusudi.
Mifano michache hii hapa:-
1. Kutekwa kwa kijana Sativa na kutupwa mbuga ya Katavi
2. Kushikiliwa kwa kijana Kombo wa Tanga kwa siku 29 bila mashtaka
3. Kubakwa na kulawitiwa kwa binti wa Yombo na wanajeshi 5. Halafu RPC Mallya badala ya kupeleka Mahakamani yeye anadai binti alikuwa anajiuza
Kama Rais Samia hatochukua mabadiliko dhidi ya Jeshi la Polisi basi ametumia fedha za walipa kodi vibaya.