Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kwa wale mlio wakazi wa Arusha na Manyara huko, nadhani mmeona kwamba hivi karibuni kumekuwa na shughuli nyingi zinazohusu wale wanaosemwa kuwa wawekezaji nchini toka mataifa ya Uarabuni.
Mara kadhaa Makonda ameonekana kushiriki kikamilifu katika shughuli wa "Wawekezaji" hawa. Madege makubwa ya mizigo yameonekana kutua na kuruka toka sehemu za Arusha. Ninavyoelewa ni kwamba kanuni za usalama/ulinzi na TRA haziruhusu ndege kubwa toka nje kutua viwanja visivyo rasmi nchini, na zaidi ikiwa zinamilikiwa na jeshi au sekta binafsi toka nje.
Hili limefanya nijiulize sana. Je, inawezekana kwamba Makonda aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha kwa kusudi maalumu, na hili la kusaidia wananchi na kero zao, ni igizo tu la kufunika ukweli halisi?
Kufikiri kwangu kunatokana na ukweli kwamba kama kuna shughuli zinazoendelea Arusha ambazo "Serikali ya juu" isingependa ziwe wazi kwa wananchi, basi mkuu wa mkoa mwenye kuaminika kusimamia hili na kutunza siri lazima angeonwa kuwa Makonda na ile kuteuliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM labda ilikuwa ni njia tu ya kupitia kuelekea kumweka Arusha kwa sababu maalum, na ndio maana japo kulikuwa na pingamizi kali katika kumrudisha katika utumishi wa umma, msimamo uliwekwa kwamba lazima Makonda arudi.
Sasa je, kweli Makonda yupo Arusha kwa manufaa ya wananchi au ya "Wawekezaji" toka Uarabuni? Najiuliza tu, kwa sababu ninapenda ku-synthesize mambo.