Wahenga wakishasema wamesema na ukipuuzia waliyoyaonya utakiona cha mtema kuni hapahapa duniani.
Baada ya Rais wa awamu ya tano Magufuli kufariki dunia Chadema wakiongozwa na Mbowe, Lissu na Kigogo walishangilia sana hadharani bila kuona aibu kabisa.
Walisema sasa watakuwa huru na watatajirika na kula raha sana hapa Tanzania.
Leo Magufuli hayupo lakini Mbowe yuko jela kwa siku 35 sasa.
Leo Magufuli hayupo lakini mbowe tayari ameshapoteza ndugu zake kadhaa kwa ugonjwa Corona.
Leo Magufuli hayupo lakini chadema imeendelea kupoteza mvuto kwa wananchi, kila wanapoitisha maandamano hamna anayetokea.
Leo Magufuli hayupo lakini sasa Chadema na Kigogo hawaelewani tena. Kwa mjibu wa kigogo chadema ya sasa ni intarahamwe( kikundi cha magaidi na wauaji wakubwa).
Shida ya watu wa ccm akili finyuuuu, yaani hadi huruma. Hivi inakuwaje mtu akiwa ccm anakuwa hana hoja? Mwangalie Bashiru Ali. Kuna uzi humu anaonekana akijenga hoja kali sana kuhusu Katiba Mpya. Lakini baada tu ya kuwa kiongozi ccm, akili zooote zilimtokea masikioni na puani. Hizoooo zikayeyuka. Leo hii Bashiru ni kama debe tupu. Naweza kusema hayo pia kwa Kabudi, na wengine wengi tu.
Habari ya CHADEMA, siyo kudorora tu, bali kufa kabisa, imetabiriwa mara nyingi sana na watu wengi tu, kina Steven Wassira, na wengine. Leo Wassira hata hajulikani aliko.
Mzee Meko mwenyewe alijitwisha jukumu la kuiua kabisa siyo CHADEMA tu, bali vyama vyoooote vya upinzani, lakini aliilenga zaidi CHADEMA, maana si ndio baba lao?
Na Meko Magufuli alitumiagharama, nguvu, muda, mbinu na mikakati mbalimbali , aliyoijua yeye, na aliyofunzwa na akina Museveni, Kagame na wengineo. Ilifikia wakati watu tukaamini kweli Magu kafaulu.
Alipokuja Lissu, Meko alimwacha azungumze atakavyo, akijua baada ya pini ya miaka 5, viongozi wakipishana mahakamani na magerezani. Wengi wao wakichomolewa na kuingizwa ccm kwa ahadi za fedha na vyeo. Viburi wakipotezwa, kuuwawa. Yote hayo yakitokea, TV zote, magazeti yote yakimpamba mzee Meko na "maajabu" aliyoifanyia Tanzania, akajua Lissu wala hafiki popote. Na kwa kibri, Meko alidiriki kuahidi jwa Mabalozi UCHAGUZI HURU NA WA HAKI. Weee, moto wa Lissu ulipoanza kuchanganya, ikabidi waanze kumpiga pini. Uchaguzi ukavurugwa kupita viwango vyoote.
Moto wa CHADEMA kuhusu Katiba Mpya unewafanya serikali ya ccm wampige kesi la ugaidi, ili akae gerezani. Hawana hoja za kumjibu. Huo ndio upofu wa ccm. Hawajui kujibu hoja, wao ni kufunga watu tu. Wasichojua ccm ni kwamba jinsi Mbowe atakavyozidi kukaa gerezani, ndivyo atazidi kuwa kaa la moto, hadi watamtema. Itakuwa hadithi ya:
Uchimeje, Uchimung'unye, uchiteme. Ukitema Nchale. Ukimung'unya Nchale, Ukimeja Nchale.
Karma? Itawaachaje ccm? Wezi, wala rushwa, watekaji, wauaji? Na kwa kweli Karma ilianza naMeko mwenyewe, aliyeitangazia CHADEMA kiama. Na sasa tunaona serikali ya ccm vipande vipande. Mara gazeti la Uhuru liandike hivi. Mara Gwajima Askofu aseme vile, mara aibuke Gwajima waziri anadai mumewe katesti mitambo ya mkewe, kama siyo Karma, ni nini hiyo?