Kwa zama tulizopo ni bora mtu kwenda Ordinary diploma au Advance Education (Form 5 na 6?)

Nomadiq

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2025
Posts
8,572
Reaction score
22,926
HESHIMA MBELE wakuu.

Kama mnavyojua kuwa mwezi wa saba umefika na tayari wale wanafunzi ambao walifaulu kwenye mtihani wa NECTA mwaka, wengine wanaenda kidato cha tano na cha sita huku wengine wakianza mipango ya kuingia chuo kwa maana ya Ordinary Diploma.

Sasa nilitaka kujua iwapi level hizi za elimu hizi zina ubora sawa ama kuna moja ina ubora kuliko nyingine.

Kati ya elimu hizo mbili ipi ni nzuri zaidi kwa mtoto, bora asome chuo cha kati au bora asome kidato cha 5 & 6?

Na kwa zama tulizopo ni bora mwanafunzi aende Diploma baada ya kumaliza kidato cha 4 au aende Advance kwa maana ya Kidato cha 5 na 6?
 
Kwa mm niliepitia advance level na kwenda chuo naona Bora mtu apitie ordinary diploma then atajiendeleza kielimu akiwa kazini na pia kazi zinafanywa na ordinary diploma

But kama tunataka kuwaandaa wanasayansi nguli wa utafiti ni vizuri wakapitia advance coz unachimba mambo kwa undani sana
 
Wengine huchaguliwa kujiunga kidato cha tano(advanced secondary education), elimu hizi zina ubora sawa, ama moja ina ubora kuliko nyingine.
Diploma haifanani na 5&6, moja ina Advantage zaidi kuliko nyingine

5&6 haina issue sasa hivi Diploma ndio inayoangaliwa zaidi labda huko mbele wakibadirisha kete ndio 5&6 itakua na maana

Mtoto wako mpeleke Diploma sio 5&6
 
kwa upande wangu aliyeenda diploma ndiyo ana kitu cha zaidi, yaani alosoma diploma akija kuendelea Degree na yule alotoka Advance wa Diploma anakuwa na maujuzi kibao
Umesema ukweli kabisa Chica, nilitoka fresh from school nikawa naona kabisa wale wa diploma wako nondo zaidi kuzidi sisi wa kidato cha sita, walikuwa wanashuka halafu kuna ile washazoea maisha ya chuo wakati sisi ndio tuaadapt.
 
Kwa mm niliepitia advance level na kwenda chuo naona Bora mtu apitie ordinary diploma then atajiendeleza kielimu akiwa kazini na pia kazi zinafanywa na ordinary diploma

But kama tunataka kuwaandaa wanasayansi nguli wa utafiti ni vizuri wakapitia advance coz unachimba mambo kwa undani sana
Hata mimi nilipitia Advance mkuu, nakubaliana na wewe japo wanasema waliosoma Advance ndio wako vizuri lakini kwa mtazamo wangu naona wale wa diploma wako nondo zaidi. Pia wana uzoefu kama x3 kuzidi sisi wa kidato cha sita.
 
Diploma haifanani na 5&6, moja ina Advantage zaidi kuliko nyingine

5&6 haina issue sasa hivi Diploma ndio inayoangaliwa zaidi labda huko mbele wakibadirisha kete ndio 5&6 itakua na maana

Mtoto wako mpeleke Diploma sio 5&6
Hakika mkuu elimu ya diploma naona ina advantage maana hata akimaliza anaweza kuamua kuishia hio diploma na akapata ka-gap kaajira, wakati wa 6 hana advantage hio.
 
Inategemea na Career kama ni Upande wa Afya nenda 5 and 6 ila Kwa field zingine zote zilizobaki anza na Diploma faida ni nyingi sana. Sana kwanza employer saivi majority Wana ajili watu wa diploma kuliko degree holders ivo nafasi za kazi za Diploma ni nyingi sokoni kuliko degree.
 
KWANINI career za afya aende Advance(form 5 & 6), unaweza kutoa maelezo hapo mkuu.
 
HESHIMA MBELE wakuu.

Kama mnavyojua kuwa mwezi wa saba umefika na tayari wale wanafunzi ambao walifaulu kwenye mtihani wa NECTA mwaka, wengine wanaenda kidato cha tano na cha sita huku wengine wakianza mipango ya kuingia chuo kwa maana ya Ordinary Diploma.

Sasa nilitaka kujua iwapi level hizi za elimu hizi zina ubora sawa ama kuna moja ina ubora kuliko nyingine.

Kati ya elimu hizo mbili ipi ni nzuri zaidi kwa mtoto, bora asome chuo cha kati au bora asome kidato cha 5 & 6?

Na kwa zama tulizopo ni bora mwanafunzi aende Diploma baada ya kumaliza kidato cha 4 au aende Advance kwa maana ya Kidato cha 5 na 6?
japo wapo wengi bora uende ordinary dip
 
Unaweza kwenda Advance ,Diploma na hata degree na master n.k

Kwa sasa soko la Ajira limekuwa gumu kidogo hivyo ajaribu kuangalia mambo mbali mbali kutokana na mahitaji yake.

Mfano anataka kuwa Mwalimu wa secondary itapendeza akipe A level

So aangalie mahitaji yake zaidi .
 
Mfano, ataka kuwa electrical engineer au career inayoendana na hio, aende Advance, ordinary diploma, ama vocational education(VETA)?
 
uzi kama huu ulipostiwa kidogo nyuma, nilishangaa kuona comments nyingi sana zikisema wanaoenda o. diploma ni wale waliofeli, naona dawa imeingia vizuri sasa na watu wamesanuka
SIDHANI KAMA NI DAWA , nadhani ni nyakati zimebadilika, mahitaji ya soko la ajira yamebadilika, watu wameongezeka, na mambo mengi tu yamebadilika.
 
Back
Top Bottom