Kila siku mnaambiwa msiwaamini sana wanasiasa, lkn vijana mmekuwa hamuelewi. Mwaka 2008 wanasiasa wa upinzani kina Lisu, Mbowe, Msigwa, Zito na wengineo waliwaambieni kuwa Lowasa ni fisadi papa na kamwe hastahili kushika wadhifa wowote serikalini. Mwaka 2015 wale wale wanasiasa kina Lisu, Mbowe, Msigwa na wengineo wakawaambia tena kwamba Lowasa sio fisadi na kwamba anastahili kushika nafasi ya juu zaidi serikalini ikabidi wawashawishi ili mumchague awe raisi. Miaka kadhaa iliyopita mch Msigwa aliwahi kumtuhumu komredi Kinana na mambo ya ujangili, lkn swala lilipofika mahakamani na Msigwa kutakiwa kwenda kutoa ushahidi, alishindwa kwenda na mwisho ikaamriwa kuwa alipe faini kwa kumchafua Kinana au aombe radhi, Msigwa akaomba radhi kwa uongo aliofanya kumchafua Kinana. Zito aliwahi kudai kule Kigoma kuna wilaya fulani watu walikuwa wanauwawa na kutupwa porini, alipoitwa polisi kutoa ushahidi Zito alikosa ushahidi wa kupeleka polisi na matokeo yake kila mtu akajua kama jamaa ni muongo. So kwa aina hii ya siasa za bongo sitashangaa mwanasiasa kukumezesha uongo mungine kama huu uliyoandika hapa kwa manufaa yake mwenyewe na genge lake. Na ww bila kufikiri uongo wao, ukaamua kukubali na kuamini kila unaloambiwa na wanasiasa. Mh Kikwete aliwahi kusema "akili ya kuaombiwa changanya na yako" sio uwe mtu wa kukubali kila unalomezeshwa na wanasiasa.