Hahaha.. Japo inawezekana kiongozi aliweka mchango wake ktk utawala huu kwa mujibu wa katiba, lkn naamini maamuzi hayakuwa ya kwake peke yake. Kwa vile lile lilikuwa jambo linalohusu ulinzi wa katiba yetu isinajisiwe (kama unavyosema kwamb ilitaka kufanyika ndivyo sivyo) basi ni wazi kuwa kulikuwa na majeneral, na viongozi wengine wakubwa wa jeshi waliochangia kufanya hali iwe sawa. Kumbuka hata mw Nyerere ilishindikana kumpindua kwa sababu katika uongozi wa juu kuna wale waliotaka kufanya mapinduzi na kuna wale waliokataa kufanyika mapinduzi. So usifikiri jambo nyeti la namna hiyo linachukuliwa uamuzi na mtu mmoja tu eti kwa sababu ni kiongozi, no kwa mfumo wa jeshi la Tanzania lililoshibishwa damu ya uzalendo kwa nchi yao, kwa raisi wao na kwa katiba yao, kamwe haiwezekani. Ni lazima uwashirikishe na wengine afu wao wakubali au wakatae. Ukifanya jambo ambalo haliendani na viapo vyao kivyako vyako na ukashtukiwa, huenda wale ma general unaowaongoza wakakugeuzia kibao na kuweka mtu wao wenyew anaowafaa. Hii ni Tanzania yenye jeshi na wanajeshi makini ndugu yang, kamwe usiifananishe na Myanmar au Sudan.