Kwaheri TTCL, kila lenye mwanzo halikosi mwisho

I get you.

Zile safari kwa jamaa kati ya hao wawili hazikuwa bure.

Walikuwa wakitoka na mipicha wacheka mbele ya kamera lakini yalokuwa nyuma ya mazungumzo mazito hakuna alieambiwa.
 
Nadhani wamiliki wa makampuni ya simu wanataka kuizika TTCL.
 
Nadhani wamiliki wa makampuni ya simu wanataka kuizika TTCL.
Watanzania waelimishwe wasikae tu kama mazuzu, TTCL si kampuni ya mtu ni mali ya taifa.

Ni sehemu ya mali za taifa TTCL, ATCL, TRC, TPA, TAA, NSSF, NDC, NIDA, TCRA, EWURA, DAWASA, TANESCO, NHC, na mengine mengi tu ni mashirika au kampuni za umma.

Tubadilike tuweke sheria kabisa, mtu akiingia na akiyachezea shere mali hizi twaenda "Chinese Way" ambayo ni..........
 
Mimi nilisema Starlink haiwezi kupewa ruhusa Tz watu wakawa wanabisha, same reason hawafufui mfumo wa reli ambao ungesafirisha mizigo kwa gharama nafuu sababu mabosi ndo wamiliki wa malori.
 
Solution sio kuitoa serikalini bali ni kuuza hisa ili management iwe inaidhinishwa kitaalamu na shareholders kuliko hivi sasa raisi anateua.

Miaka ya Magufuli wakati wa kupokea gawio binafsi nilisema serikali ina mzaha sana kwenye kuendesha biashara; taasisi aina ata net profit hilo gawio linatokea wapi.

Kipindi hiko kwenye financial statement yao shirika lilikuwa linatengeneza gross profit, tatizo ni admin expenses wanatumia sehemu kubwa sana ya mapato yao kwenye kulipa mishahara kushinda ata washindani wao na hapo ndio faida yote inapopotea. Jumlisha na haya mashirika ya serikali kweny overstating ya matumizi mengine ni jambo la kawaida through dodgy tenders.

Hilo shirika mtu yeyote makini akipewa kuliendesha kitu cha kwanza kitakachofanyika hapo ni downsizing of the workforce; inachukua sehemu kubwa ya mapato.

Kwa kifupi huko serikalini wanahitajika financial analysts, matatizo yao ni obvious ukisoma statements zao. Halafu ukiangalia na everyday operation ni wazi faida aiwezikani hapo miaka 800, ajabu shirika linalotengeneza hasara juzi tu limetoa millions in charity hivi unadhani kungekuwa na shareholders wangekubali; mkutano unaofuata mkurugenzi angekuwa voted out yeye na body nzima ya management.

Sidhani kama serikalini kuna watu wengi waliosoma finance kwenye nafasi za ushauri. Otherwise hayo mashirika yanaendeshwa ovyo sana to external observers; yote sio TTCL tu.

Hao wakurugenzi ukiwasikiliza tu unaona ata uelewa wao wa maswala ya biashara unapwaya, sasa wanashangaa kitu gani yanapotengeneza hasara wakati ni vitu obvious kulingana na uongozi wenyewe.
 
Unafidiwa nini mkuu,line!Si unaachana nayo tu.
 

umeandika kitu kikubwa sana..
umehighlight all the major problems leading to the failure.
 
Wanasema wakaguzi (auditors) tu wanatosha.
 
Wanasema wakaguzi (auditors) tu wanatosha.
Hao watu awafanyi maamuzi ya kibiashara, auditor anaweza highlight tu poor efficiency issues za management. Lakini uongozi wa shirika auna obligations za kufuata ushauri wake.

Mtu pekee mwenye nguvu ya kubadili uongozi akiona mambo bado ovyo ni raisi anaeteua na yeye analetewa tu majina na watu wengine ambao they don’t conduct due diligence ya uwezo wa watu wanaopendekeza kuteuliwa.
 
Shida Raisi wetu mpendwa hatoi matamko yeye anatoa suggestions tu. Kama issue ya wale jamaa walio kula hela ya ndege ya mizigo ilibidi awasimamishe palepale
 
I like you MTAZAMO unafikiri very positive na huwa waleta productive thoughts as always.

Lakini analysts kama Ernst Young, PWC si wapo?

Serikali iamue kama wenzetu India ambao shirika la reli lamilikiwa na serikali lakini laongozwa na wizara ya reli kabisa no problem.

Baada ya hapo ndipo yaibuka makampuni ya reli ambayo hukodi njia za reli hivyo hulipia huduma hiyo ya kutumia reli.

Mwisho kuna kampuni inoshughulika na matengenezo na uboreshaji wa njia zote za reli yaani railway network.

Hivyo utaiona kwamba shirika la reli lipo chuini ya wizara lakini inasimia shughuli zaote za reli ila uendeshaji ni makampuni ya reli ambayo asilimia kubwa ni makampuni binafsi.

Hii kwanza yaleta ufanisi katika uzimamizi na pia yapanua soko la ajira kwani kampuni hizi zitaajiri watu wao wataofanya kazi katika reli hizo.

Pia kampuni inoshughulika na matengenezo na uboreshaji wa njia za reli nayo inakuwa na wale sub-contractors ambao wote wanapata ajira hivyo kupanua zaidi soko la ajira.

Huduma za reli tu Tanzania yaweza kuinua uchumi na sko la ajira maana watu wataarijiwa katika sehemu mbalimbali ukatishaji tiketi, usafi, huduma ndani ya garimoshi, udereva uongozaji na mengine lukuki.

Sasa hata kama kuna watu wahitaji kuendesha biashara ya mabasio waweza kufanya hivyo bila shida maana huduma ni usafiri ni huria na watu wana uchaguzi aina ipi ya usafiri watumie.

Air India CEO wake ni raia wa New Zealand na jana alitetea kwanini Air India yailipa Russoa kutumia anga lake ili kupunguza gharama za kuzunguruka mamaili kibao kutafuta viwanja vya ndege Ulaya.

Huyu CEO na Managing Director (Campbell Wilson) amesimamia mashirika ya ndege ya Singapore, Canada, Hong Kong na Japan hivyo ana uzoefu mkubwa.

Wenzetu India sasa hivi wapiga hatua kubwa sana kiuchumi na kwa kila sekta.

Eeeh Mola wetu, tusikie kilio chetu wana wa nchi ya Tanzania.
 
Sasa huoni wapi twaonyesha ujinga wetu?

Weye una ndege 6, mfano wa marubani 147 wa nini?

Huo si ndo upigaji tunozungumzia?
 
Nini hasa kinafanya TTCL isiendeshwe kwa faida kulinganisha na makampuni mengine ya simu!? Ni kukosa uongozi, kushindwa kufanya maamuzi ya kibiashara kwa wakati, wafanyakazi wasio na weledi au!?
Acha lifungwe hawa jamaa awajui biashara tuliomba huduma ya internet kwa njia ya fibre cable dah iyo bei taasisi ikaona twende kwa kampuni binafsi na wanapoteza mteja kwa kauli yao bila wasiwasi
 
Na si tu workforce kuna matawi na ofisi kila wilaya na vitongoji, idadi kubwa ya magari, idara ya huduma kwa wateja na shughuli zingine za uendeshaji.

Kwa mfano TTCL wana Telephone House, ile yaweza kuwa ni centre yake kwa Dar-es-Salaam na HQs.

Kisha baadae wafungua kidogokidogo kila Wilaya kulingana na kukua kwa mapato, soko na mahitaji.

ATCL wana ofisi kuu Pale Ohio St hivyo ofisi ile yaweza kuboreshwa na kukodishwa kisha HQs yake ihamishiwe uwanja wa ndege.

Hivyohivyo kwa mashirika mengine makubwa ni lazima kitu cha kwanza kuangalia pesa yapotelea wapi.

Tatizo jingine umeligusia kuhusu Analysts hawa uhaba upo hivyo itabdi uwe na analysts kutoka nje na si Ulaya bali hapahapa barani Afrika wapo analysts walosomea biashara na wana uwezo wa kufanya analysis ya threats kwa organisations na masuala mengine kama masoko na kusaidia kuleta resilience katika kampuni wakati wa shida.
 
Matatizo yao wote yanafanana admin costs, higher costs of sales and poor management competence.
 
Akili ndogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…