Kwakuwa umefurahi ngoja nikupe hiyo sura inavyo sema.
Katika Qurani ukiona Neno "Sema" jua kuwa hapo anaongea Muhamadi.
Kama hapa.
قُلْ مَا كُنتُ بِدْعًا مِّنَ الرُّسُلِ وَمَا أَدْرِي مَا يُفْعَلُ بِي وَلَا بِكُمْ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ وَمَا أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ
[ AL - AH'QAAF - 9 ]
Sema: Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi.
........
Ukiona hakuna neno Sema ujue kuwa hayo ni maneno ya Allah watabarak au Majini.
Kama hapa
وَأَنَّا مِنَّا الْمُسْلِمُونَ وَمِنَّا الْقَاسِطُونَ ۖ فَمَنْ أَسْلَمَ فَأُولَـٰئِكَ تَحَرَّوْا رَشَدًا
(AL - JINN - 14)
Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanao acha haki. Basi walio silimu, hao ndio walio tafuta uwongofu. (hapa yanaongea Majini na hayaambiwi "Sema"
Hiyo sura yote yanaongea Majini tu. Na hayaongei popote pengine ila katika Sura yao ya Majini.)
Sura ya Fatiha ndio hii
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
(AL-FAATIH'A - 1)
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ
(AL-FAATIH'A - 2)
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;
الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
(AL-FAATIH'A - 3)
Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu;
مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ
(AL-FAATIH'A - 4)
Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo.
إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ
(AL-FAATIH'A - 5)
Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.
اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ
(AL-FAATIH'A - 6)
Tuongoe njia iliyo nyooka,
صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ
(AL-FAATIH'A - 7)
Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.
...............
Katika Qurani ni Allah na Majini tu ndio wanaongea kwa kutumia nafsi ya uwingi kama (sisi) (tuna)
Muhammadi ni mmoja na Jibrili ni mmoja hawawezi kusema (sisi)
..........
Hapa anaongea Allah
فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ إِنَّا لَقَادِرُونَ
(AL - MAA'RIJ - 40)
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza
.............
Ukiwauliza Waislamu hiyo Surat Fatiha na hapo kwenye hiyo Aya moja ya Surat ya AL-MAA'RIJ kuwa
Ni nani anaongea hutajibiwa hadi kiyama.
Ukiyauliza hayo maswali huko Somalia utaishia kukatwa kichwa kwa kuikashifu Dini na Qurani.
......
Ukiwauliza hapa anayeongea ni nani katu huwezi kujibiwa.
مَّا أَصَابَكَ مِنْ حَسَنَةٍ فَمِنَ اللَّهِ ۖ وَمَا أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٍ فَمِن نَّفْسِكَ ۚ وَأَرْسَلْنَاكَ لِلنَّاسِ رَسُولًا ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّهِ شَهِيدًا
[ AN-NISAAI - 79 ]
Jema lilio kufikia limetokana na Mwenyezi Mungu. Na ovu lilio kusibu linatokana na nafsi yako. Nasi tumekutuma kwa watu uwe ni Mtume. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kutosha.
....
Hao akina "nasi" ni nani waliomtuma Mtume huku Mungu akishuhudia?