Kwahiyo tumewahamishia Shule nyingine Walimu waliokuwa wakichekelea kupigwa Mwanafunzi ili wakacheke zaidi huko?

Katika kupitia pitia nyuzi mbalimbali kuhusu sakata hili sijaona aliyetoa sababu za kitaalam za kwanini ni hatari kumchapa mtoto kwwnye nyayo ni hatari kuliko mkononi na matakoni. Na kwanini imfanye mwalimu afukuzwe kazi kwa jambo hilo. Si kama naunga mkono jambo lile hapana. Nahitaji sababu za kitaalam tu. Povu ruksa.
Suala sio tu kupiga kwenye unyayo, suala ni kiasi cha nguvu alichotumia kana kwamba anataka kumuua mtoto wa watu
 
Katika kupitia pitia nyuzi mbalimbali kuhusu sakata hili sijaona aliyetoa sababu za kitaalam za kwanini ni hatari kumchapa mtoto kwwnye nyayo ni hatari kuliko mkononi na matakoni. Na kwanini imfanye mwalimu afukuzwe kazi kwa jambo hilo. Si kama naunga mkono jambo lile hapana. Nahitaji sababu za kitaalam tu. Povu ruksa.
Inaonekana wewe ni mwalimu. Maelezo yako yanaashiria kutetea tendo hilo; haiyumkini na wewe unawapa wanafunzi wako adhabu za namna hii au zinazofanana na hizi! Waliopendekeza adhabu kwa watoto mashuleni hawakuamua adhabu hizo pasipo kufanyia utafiti jambo hilo. Ilithibitika maeneo salama ya kuchapa fimbo mwanafunzi (mtoto) ni mikononi na matakoni. Kuna mtaalam mmoja wa reflexology kutoka huko Mbezi (DSM), anasema mishipa yote ya fahamu ya binadamu imeweka mizizi yake kwenye nyayo. Hivyo ni wazi kumchapa mtoto kwenye nyayo kunaweza kuleta madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kuharibu mishipa hiyo! Mtoto anaweza kupooza (permanent paralysis) kutokana na kuathirika kwa mishipa hiyo. Nasikitika yule mama mwenye mtoto aliyeadhibiwa kujitokeza na kusema kuwa mtoto wake anaendelea vizuri; athari zingine huwa zinachukua muda kujitokeza!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa kimya sana kwenye swala hili ebu niongee kidogo.Mimi ni mzazi pia kwa hiyo awali nimpe pole mzazi wa mtoto na pia mwalimu na mtoto mwenye.Siitaji kulaumu Yeyote nachojua ni kuwa katika hii Africa haya malezi ya viboko yanaanzia nyumbani kwa ajili ya kumshape mtoto(na hii inafanyika mpka sasa) Tatizo ni idadi na umri wa mtoto na Ndo maana wizara inatambua na imeweka utaratibu wa hii adhabu ya viboko na mhusika ni mwalimu kiongozi Ndo wa kulitimiza hili la utaratibu au amteue anayeona anafaa kuadhibu kwa kufata kanuni ya Sera ya elimu.Kwa nini mwl analaumiwa naisi ni kutofata pengine utaratibu huu.Lakini adhabu ya viboko ni mhimu sana kwa mtoto ili afanye kile anachoelekezwa kwa utashi zaidi iwe shuleni au nyumbani vinginevyo ikifutwa kizazi kitaalibika zaidi.
 
Huwa najiuliza mwalimu usipochapa anapungukiwa nini?, hapo ndipo ninapowashauri walimu waache kuchapa hakika wataishi vema.

Ninajua kuacha kabisa kuchapa kwa shule zetu hizi kuna athari lakini ni bora kuliko wewe mwalimu kujikuta uko mikonini mwa vyombo vya dola huku ukivuta pumzi ya moto au ukiwindwa na wazazi wa watoto mithili ya pakashume mitaani.

KILA MMOJA ASHINDE MECHI ZAKE
Swali zuri na pia umetoa ushauri mzuri Sana ila uharisia mgumu Sana

Ni hivi inabidi ujue mwalimu ni muajitiwa na pale shuleni yupo chini ya serilaki na shule ka taasisi pia katika majukumu anayopewa ni pamoja na TAALUMA na NIDHAMU kwa wanafunzi sasa utata unaanza kwenye haya majukumu mawili maana yanaenda kwa kutegemeana nikupe mfano wewe mwanao alivyokiwa anaanza chekechea dhumuni lako sililikuwa yeye aende apate elimu(taalum) hii lakini 99.9% ya wazazi kipindi hiki hujikuta wanawachapa fimbo watoto maana watoto wanakuwa hawataki shule kabisa YOU SEE aim yako ni elimu ila unashangaa unafanya jukumu lingine ambalo hukupanga la adhambu hili kumfanya mtoto aende shule hili atimie jukumu kuu....So unaona HAKUNA TAALUMA BILA NIDHAMU (NATURAL ALOGARITHIM) hii ALOGARITHIM ndio inayomtesa mwalimu Leo hii hasa kwenye hizi shule za kimaskini ambazo mazingira yake yalivyo magumu hii ALOGARITHIM ndio imekuwa ngumi zaidi kwa mwalimu.

Unasema mwalimu ajari kusomesha tu Basi lakini NATURE haikubaro Hilo kitu watoto wetu wakimaskini kutimiza Hilo suala super impossible bila kurekebisha nidhamu zao na hao watoto hakuna nji nyengine yoyote hapa Duniani unaweza rekebieha nidhamu zao instant NI FIMBO TU.

Mimi nishawai fundisha shule miezi kadhaa na Ni katika wale walimu HUMBLE sana hila nakuambia kazi ya uwalimu kuwa humble Kuna wanafunzi wanaweza kukutia hata kidole ukiwa unafundisha inagika wakati unajari kifundisha tu watoto wakorofi wanasumbua nyuma kelele inayotengeneza DHARAU kwako unaona inafika point wale wanafunzi wazuri wanawakemea wanafunzi wenzao kwa namna unaona Kama wanakuonea huruma

“Simunyamaze jamani hamuoni mwalimu yupo darsani"

Kuna mifano mingi ila uwalimu kazi fulani sio kazi kwa kifuoi hasa kwa hapa Tz kifupi mwalimu ni mtu anayebebesha zigo la miba.

Hii taaluma inaingiliwa na kuchezewa Sana na baadhi ya makundi ya watu ikiwemo jamii nk proffessional yoyote ile inabidi iheshimishe kwasababu wale walio na hio proffessional ndii wanajua ni Nini na Nini kinafanya kitimiza nini...ningeshauri walimu wajielewe wawe na misimamo Kama professional nyengine Kama madktari nk kwasabu nauhakiki mwalimu hata akimuadhibu mwanafunzi kisheria then yule mwanafunzi akapata madhara yoyote wazazi wa mwanafunzi, jamii, mitandaoni nk itakuwa against na huyo mwalimu yaani mwalimu halindwi akiwa natimiza majukumu yake...WHAT THIS

Jamii inaona mwalimu kuadhibu mtoto Ni Kama ni anapata burudani instead kuona ana rekebisha mtoto.
 
Kipi kizuri, usichape uwe salama au uchape uwe hatiani?
 
Waafrika tunadhani kuwa kupiga ndio kufunza la hasha
Hii ni tabia walizonazo wengi sana
Nidhamu inahitajika na kwa mafunzo na adabu mtoto atajifunza kama utamsaidia na kumfundisha vizuri

Hii tabia ya kupiga ipo mpaka kwa wanyama
Unampiga mbuzi fimbo kisa amekula mahindi anakimbia baada ya mda anarudi tena na wewe unapiga tu ulivyokuwa zuzu badala ya kutafuta njia zingine

Punda kabeba mzigo umemuelemea unapiga tu ili aende kwa matakwa yako
Hajala siku nzima hata maji hujampa kabeba mzigo ambao ukiuza ndio umpeleke mtoto shule au hospitali ila umuhimu wa Punda huuoni

Kuna jamaa nilimuambia huyo punda ndio anakulisha halafu unamchapa hivyo hebu niambie hata majani umemkatia ? Au maji umempa
Anabaki kuniangalia

Wasaidieni watoto na ushauri kwa waalimu
Kama mtoto haelewi labda ana autistic wewe unapiga tu
Waite wazazi mjadili kuliko kumpiga kila siku

Kwani watoto wote wana ufaulu mmoja au wana uelewa wote
Wengine hawaelewi mpaka urudie mara Tatu

Poleni sana wanaodhani kupiga ndio suluhu
 
Watanzia acheni unafki.. mbon hamuwasem Askari wavyo chapa watuhumiwa vituon wakiwa wanapeleleza kesi... ?
Yule kachapia fimbo pale askari anatumia nondo tena kukukandamiza ukubali kosa na ikitokea umeshinda kesi unaenda jiuguza nyumban kwenu...
Kuna kosa na kosa. Sio kila kosa litapelekea physical torturing ukiwa police... umewahi kuona kwa mfano watu wamekamatwa kwa kosa labda la kujisaidia au kutupa taka, kutukana, kupigana au kupiga, kuvuta bangi au madawa akapigwa kituoni?! Ataguswaguswa kutishwa

Ole wako upelekwe kwa kosa la kigaidi au kujaribu kufanya ugaidi, kuua, kubaka au uhaini uone... utaomba ardhi itoboke utumbukie ndani
 
mpwayungu village

Binafsi ninawashauri walimu wote nchini waachane na suala la kuchapa wala kufuatilia kwa kina watoto wa watu.

Mwalimu jikite kufundisha tu, mtoto wa mtu akizingua achana naye, hakikisha masuala yote ya kinidhamu unamwachia mzazi wake atajuana naye huko kwao, hata wakifeli wote wewe hautanyimwa mshahara.

Pia walimu tafuteni kazi nyingine binafsi za kuwawazisha zaidi ili ukose muda wa kutosha wa kumuwaza mtoto wa mwingine, ili ujiepushe na matatizo.

Mchuma janga hula na wakwao.
Waache kuchuma majanga yasiyokuwa yao kwa kumtoa mtu ujinga utakaohatarisha mshahara yao..km haelekei kuelekezwa muache avune ujinga wake maisha yake yote we mwl kula mshahara wako kila mwezi .ya nn kuhangaika na mtt wa mtu akikufia je
 
mpwayungu village

Binafsi ninawashauri walimu wote nchini waachane na suala la kuchapa wala kufuatilia kwa kina watoto wa watu.

Mwalimu jikite kufundisha tu, mtoto wa mtu akizingua achana naye, hakikisha masuala yote ya kinidhamu unamwachia mzazi wake atajuana naye huko kwao, hata wakifeli wote wewe hautanyimwa mshahara.

Pia walimu tafuteni kazi nyingine binafsi za kuwawazisha zaidi ili ukose muda wa kutosha wa kumuwaza mtoto wa mwingine, ili ujiepushe na matatizo.

Mchuma janga hula na wakwao.
Kwa mfano akatokea mwanafunzi wa darasa la sita/saba anawalawiti watoto wa darasa lapili/tatu na nne waalimu wampotezee tu???
 
Kama huoni kosa kucheka kwa mtu mzima wakati mtoto mdogo akifanyiwa unyama basi hakika una walakini ndugu na pengine una tofauti ndogo sana na yule mwalimu mpigaji.
Ila watanzania tumekuwa wakatili sana, kitoto cha miaka 9 mtu mzima anamkanyagia miguu chini huku anampiga nyayo za miguu na bado wengine wanacheka na ni wanawake waliozaa sijui tumefikaje hapa. Mi mnyama tu kupigwa naumia, siigizi mi siwezi kumchapa eti mbwa au paka sembuse mtoto binadamu kwa style ile. Hapana tumepotoka mno. Babake yule kijana akiona adhabu ile anaweza kumakizana na mwalimu mitaani. Jamani walimu wanawake kwanini mna roho mbaya hivyo? Why? Stress za maisha? Badilikeni nenda nyumba za ibada muombewe
 
Watanzia acheni unafki.. mbon hamuwasem Askari wavyo chapa watuhumiwa vituon wakiwa wanapeleleza kesi... ?
Yule kachapia fimbo pale askari anatumia nondo tena kukukandamiza ukubali kosa na ikitokea umeshinda kesi unaenda jiuguza nyumban kwenu...
vile vitoto na watu wazima ni vitu tofauti kabisa. Tena umesema wahalifu, wahalifu lazima wapashwe ktk mchakato wa kutafuta ukweli. Na we ni yale yale makatili km lile tukio halijakugusa eti unafiki. Badilika ndugu.
 
Mwisho wa yote namsifu mno mzazi wa yule kijana. Ingetokea kwa mwanangu nina yakini pasi na shaka huyo mwalimu angekuwa anafaya shopping ya wheel chair na magongo saa hizi.
Acha kujiapiza kitu kama hiki na kwa namna hii. Hujui huyo mtoto alifanya kosa gani kwa ufupi hujasikia kilichosababisha kupelekea kadhia ile, hujasikia toka upande wowote ule.

Acha kujivisha ushujaa uchwara.
 
Swali zuri na pia umetoa ushauri mzuri Sana ila uharisia mgumu Sana

Ni hivi inabidi ujue mwalimu ni muajitiwa na pale shuleni yupo chini ya serilaki na shule ka taasisi pia katika majukumu anayopewa ni pamoja na TAALUMA na NIDHAMU kwa wanafunzi sasa utata unaanza kwenye haya majukumu mawili maana yanaenda kwa kutegemeana nikupe mfano wewe mwanao alivyokiwa anaanza chekechea dhumuni lako sililikuwa yeye aende apate elimu(taalum) hii lakini 99.9% ya wazazi kipindi hiki hujikuta wanawachapa fimbo watoto maana watoto wanakuwa hawataki shule kabisa YOU SEE aim yako ni elimu ila unashangaa unafanya jukumu lingine ambalo hukupanga la adhambu hili kumfanya mtoto aende shule hili atimie jukumu kuu....So unaona HAKUNA TAALUMA BILA NIDHAMU (NATURAL ALOGARITHIM) hii ALOGARITHIM ndio inayomtesa mwalimu Leo hii hasa kwenye hizi shule za kimaskini ambazo mazingira yake yalivyo magumu hii ALOGARITHIM ndio imekuwa ngumi zaidi kwa mwalimu.

Unasema mwalimu ajari kusomesha tu Basi lakini NATURE haikubaro Hilo kitu watoto wetu wakimaskini kutimiza Hilo suala super impossible bila kurekebisha nidhamu zao na hao watoto hakuna nji nyengine yoyote hapa Duniani unaweza rekebieha nidhamu zao instant NI FIMBO TU.

Mimi nishawai fundisha shule miezi kadhaa na Ni katika wale walimu HUMBLE sana hila nakuambia kazi ya uwalimu kuwa humble Kuna wanafunzi wanaweza kukutia hata kidole ukiwa unafundisha inagika wakati unajari kifundisha tu watoto wakorofi wanasumbua nyuma kelele inayotengeneza DHARAU kwako unaona inafika point wale wanafunzi wazuri wanawakemea wanafunzi wenzao kwa namna unaona Kama wanakuonea huruma

“Simunyamaze jamani hamuoni mwalimu yupo darsani"

Kuna mifano mingi ila uwalimu kazi fulani sio kazi kwa kifuoi hasa kwa hapa Tz kifupi mwalimu ni mtu anayebebesha zigo la miba.

Hii taaluma inaingiliwa na kuchezewa Sana na baadhi ya makundi ya watu ikiwemo jamii nk proffessional yoyote ile inabidi iheshimishe kwasababu wale walio na hio proffessional ndii wanajua ni Nini na Nini kinafanya kitimiza nini...ningeshauri walimu wajielewe wawe na misimamo Kama professional nyengine Kama madktari nk kwasabu nauhakiki mwalimu hata akimuadhibu mwanafunzi kisheria then yule mwanafunzi akapata madhara yoyote wazazi wa mwanafunzi, jamii, mitandaoni nk itakuwa against na huyo mwalimu yaani mwalimu halindwi akiwa natimiza majukumu yake...WHAT THIS

Jamii inaona mwalimu kuadhibu mtoto Ni Kama ni anapata burudani instead kuona ana rekebisha mtoto.
Acha arrogance za kjinga kuziita shule za serikali za kimaskini. We umesomea shule gani. Kinachotoa elimu siyo pesa. Tuheshimu shule za serikali ndiyo mali yetu zinajengwa kwa kutumia kodi na tozo mbalimbali. Acheni huu utamaduni wa kipuuzi, viongozi wote unaowaona madarakani wamesoma shule za serikali we umepata kijkibarua mjini waita shule za serikali za kimaskini, acha arrogance za kipuuzi kijana
 
mpwayungu village

Binafsi ninawashauri walimu wote nchini waachane na suala la kuchapa wala kufuatilia kwa kina watoto wa watu.

Mwalimu jikite kufundisha tu, mtoto wa mtu akizingua achana naye, hakikisha masuala yote ya kinidhamu unamwachia mzazi wake atajuana naye huko kwao, hata wakifeli wote wewe hautanyimwa mshahara.

Pia walimu tafuteni kazi nyingine binafsi za kuwawazisha zaidi ili ukose muda wa kutosha wa kumuwaza mtoto wa mwingine, ili ujiepushe na matatizo.

Mchuma janga hula na wakwao.
Tatizo waalimu wana upeo mdogo sana, wana stresa za maisha na wana hasira za maish ambazo wanaangusha kwa watoto

Kwa sasa kilichobaki ni kudeal nao perpendicular hadi washike adabu
 
Sio stress tu bali hawajui ku deal na mtoto
Yaani mwanafunzi na mwalimu hawaongei zaidi ya masomo na fimbo

Mtoto anaogopa hata kuomba ruhusa akajisaidie
Mwalimu hana akili za kuuliza kwa nini huyu mtoto analala tu kila siku masikini kumbe mama yake ni mgonjwa sana (kwa mfano) na anamuandalia uji kabla hakuja shule na usiku anamuangalia

Sasa kwa upumbavu wao hawajui au kuwaza tu kwanini mtoto anakuwa hivi badala yake linapiga tu

Ni lazima Waalimu wajue matatizo ya watoto kabla ya kupiga tu hapo wangewasaidia sana

Sio mashuleni tu hata mahospitalini wana roho mbaya utafikiri mjerumani na myahudi
 
Kwa mfano akatokea mwanafunzi wa darasa la sita/saba anawalawiti watoto wa darasa lapili/tatu na nne waalimu wampotezee tu???
Wakipotezea wako salama wao na familia zao ila wakijifanya wanashughulikia hilo ndo matatizo yanawaandama wao na ndugu zao.
Hii dunia ya kibepari kila mtu anajiangalia yeye tu, hivyo ukihangaika na mambo ya wengine mwisho wa siku unajitia matatizoni.

Kuna walimu kibao wako busy na mambo yao hawachapi wala hawahangaiki na mtoto wa mtu, wao ni kufundisha tu uelewe usielewe haiwahusu, hao wako salama na kamwe hautasikia wakilaumiwa popote hata kama hawatimizi majukumu yao ipasavyo.
 
Back
Top Bottom