Kwahiyo vijijini mtu anaweza kuuliwa kwa kuiba laptop ya laki mbili !?

Kwahiyo vijijini mtu anaweza kuuliwa kwa kuiba laptop ya laki mbili !?

We ni mjinga Sana Dr pori

Sim
Gunia la mkaa vina thamani na uhai
Utaniitaje mjinga wakati nimekupa clear picture ya mambo yanavyoenda? umeshangaa mtu kuuliwa kwa wizi wa laptop wakati watu wanauliwa kwa wizi wa gunia la mkaa tena mjini,

Kama unathamini uhai wako acha WIZI, ukibananishwa watu wanakupiga kiberiti,

Kasikilize Maisha ya Bongo ya 20%
 
Nimeshangaa kusikia wananchi wanamuua MTU kwa kosa la kuiba lap top ya lakimbili .

Na najiuliza hawa jamaa ni kweli hawana akili .Ila hata kufikiria hawawezi?.
Hata huku mjini watu wanauawa kwa kuiba nguo zilizoandikwa kwenye kamba zenye thaman isiyozidi elfu hamsin kwaiyo popote mtu anaweza uawa kwa kpsa la wizi tofauti ya yule dogo kauawa na watu wawili tena viongozi serikali
 
Nimeshangaa kusikia wananchi wanamuua MTU kwa kosa la kuiba lap top ya lakimbili .

Na najiuliza hawa jamaa ni kweli hawana akili .Ila hata kufikiria hawawezi?.

Ameandika Edo Kumwembe.

Ameuwawa Kijana Enock kizembe tu. Unadhani wauaji walipanga kumuua? Hapana. Uzembe wa fikra unatutawala. Watu wachache wanapanga kumuua mtu kama wale Polisi waliohukumiwa kunyongwa.

Huku mtaani kuna uzembe wa kumkomesha mtu. Unampiga mtu sana. Haujui kama zamu yako ya kuua imefika. Unaona unamkomesha tu. Haujui uimara wake wa kimwili wa kuvumilia kipigo.

Unaposikia 'amuua mwanae kwa kuiba sh mia'. Sio kwamba alitaka kumpiga amuue. Hapana alitaka kumkomesha. Hata ugomvi wa baa haukusudii kifo. Unakusudia kukomeshana halafu unaleta kifo.

Mtanzania mwenzangu hata mimi na wewe tunaweza kupata kesi ya kuua tusipokuwa makini. KITU CHA MSINGI epuka ugomvi. Epuka kupiga. Epuka kupigwa. Epuka shari. Enock angepelekwa polisi angekuwa hai na wapigaji wangekuwa nyumbani sio polisi. Sijui nimeeleweka?
 
Yote haya yamechangiwa na watekaji wa Samia kuteka teka hovyo hadi imezoeleka na Kwa watendaji wengine kuona Jambo la kuteka na kuua ni la kawaida.
Hujawahi kuishi vijijini - mauaji na watu kujichukulia sheria mkononj kwa ajili ya vitu vidogo in the name of wizi ni mengi mno. Inasikitisha sana. Jamii inapaswa kubadilika. Wapo waliosingiziwa na waliuawa na kuchomwa moto...

Kuhusisha kila kitu na Samia sio busara... na kuifanya jamii isiwajibike. Tubadilike - mauaji ya namna hiyo ya enock vijijini ni mengi mno. Mjini yamepungua. Mfano leo usingiziwe umeiba pale kariakoo - sidhani kama utapona.
 
Ameandika Edo Kumwembe.

Ameuwawa Kijana Enock kizembe tu. Unadhani wauaji walipanga kumuua? Hapana. Uzembe wa fikra unatutawala. Watu wachache wanapanga kumuua mtu kama wale Polisi waliohukumiwa kunyongwa.

Huku mtaani kuna uzembe wa kumkomesha mtu. Unampiga mtu sana. Haujui kama zamu yako ya kuua imefika. Unaona unamkomesha tu. Haujui uimara wake wa kimwili wa kuvumilia kipigo.

Unaposikia 'amuua mwanae kwa kuiba sh mia'. Sio kwamba alitaka kumpiga amuue. Hapana alitaka kumkomesha. Hata ugomvi wa baa haukusudii kifo. Unakusudia kukomeshana halafu unaleta kifo.

Mtanzania mwenzangu hata mimi na wewe tunaweza kupata kesi ya kuua tusipokuwa makini. KITU CHA MSINGI epuka ugomvi. Epuka kupiga. Epuka kupigwa. Epuka shari. Enock angepelekwa polisi angekuwa hai na wapigaji wangekuwa nyumbani sio polisi. Sijui nimeeleweka?
Edo kumwembe Akili kubwa Sana . Elimu inamjenga.
 
Sio kijijini tu hata mjini hiyo hali ipo kwenye jamii ya mtanzania isiyojitambua,ambapo haohao wanaomuua mwenzao kikatili sio tu kwa laptop ya lakimbili bali hata kuku wa elfu kumi,wakisikia gari la mizigo au mafuta limepata ajali watakimbilia kwenda kuiba na vidumu vyao ila wakisikia kelele za "mwizi" watatoka na mawe kwenda kuponda na kuchoma moto kikatili mwanadamu mwenzao pasipokujali ameiba nn,ndipo hapo mm husema watanzania ni viumbe wasiojitambua
 
Kwa nn Asipelekwe Jela kuliko Kumuua?
Kuua unaondoa uhai wa mtu (Pumzi ya Mungu)
Mungu mwenye uwezo wa kuchukua uhai wa mtu bado anahuruma anakupa nafasi ubadilike

Ila watu wanajikuta wao ndio wanahukumu

Mathayo 7;1
Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.

2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.

Kutoka 20:23 Usiue
 
Back
Top Bottom