Kwahiyo vijijini mtu anaweza kuuliwa kwa kuiba laptop ya laki mbili !?

Kwahiyo vijijini mtu anaweza kuuliwa kwa kuiba laptop ya laki mbili !?

Mjini ndio zaidi, watu wanauliwa kwa kuiba Simu, Radio,TV, gunia la Mkaa, Kuku, Kutembea na Mke/Mume wa mtu,

Arabuni anakatwa kiganja,

Wizi mbaya, mapori yapo mengi tukalime au tufuge
Huyo hajaiba. Ila kahisiwa kuiba. Na waliomuua ndo hawa wanaofanya madudu ya ufisadi wa ardhi ya vijiji. Kama adhabu ya mwiz ji kummua walitakiwa wao waanze kuuawa
 
Huyo hajaiba. Ila kahisiwa kuiba. Na waliomuua ndo hawa wanaofanya madudu ya ufisadi wa ardhi ya vijiji. Kama adhabu ya mwiz ji kummua walitakiwa wao waanze kuuawa
Ni kweli story ya huyo kijana ipo tofauti lakini tukirudi kwenye suala la wizi sio mzuri tuwakanye vijana wetu waache hiyo tabia, unayemuibia na yeye kavurugwa vile vile
 
Kwa nn Asipelekwe Jela kuliko Kumuua?
Kuua unaondoa uhai wa mtu (Pumzi ya Mungu)
Mungu mwenye uwezo wa kuchukua uhai wa mtu bado anahuruma anakupa nafasi ubadilike

Ila watu wanajikuta wao ndio wanahukumu

Mathayo 7;1
Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.

2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.

Kutoka 20:23 Usiue
Wakipelekwa jela wanatoka baada ya wiki tu na wakirudi wanakuja kulipa kisasi, mwizi sio wa kumtetea akikukuta kwenye 18 anakuibia na kukuua vile vile,

Tuletee na andiko la hukumu ya mwizi
 
Ningekuwa na Uwezo
Walioba na Walioua Nakuja na Defender 🚓 Wekaaaa Ndaniii
Woteee Wanamakosaaaa😎
Watajua Hawajui🤏 No more Explanation
 
Nimeshangaa kusikia wananchi wanamuua MTU kwa kosa la kuiba lap top ya lakimbili .

Na najiuliza hawa jamaa ni kweli hawana akili .Ila hata kufikiria hawawezi?.
kwan mjin hawaui kwa kitu kidogo mnamchoma moto kaiba laki mbili binadamu hamna upendo watu wangeju kumfuata Olumba tungejua nini maana ya Upendo
 
Nimeshangaa kusikia wananchi wanamuua MTU kwa kosa la kuiba lap top ya lakimbili .

Na najiuliza hawa jamaa ni kweli hawana akili .Ila hata kufikiria hawawezi?.
Mbona mjini kuku tu wanakuuwa!...nchi yakimasikini sana hii
 
Akili Vijijini ni jamii duni Sana ambazo zimetofautia kidongo na hao kuku
Mbona kariakoo mtu anaiba yebo yebo anachomwa moto live sembuse kijijini kijijin watu Wana Upendo na akili kubwa we mwenyew angalia laki mbili mjini mtu anakufa kwa 1000, 2000 au 750
 
Nimeshangaa kusikia wananchi wanamuua MTU kwa kosa la kuiba lap top ya lakimbili .

Na najiuliza hawa jamaa ni kweli hawana akili .Ila hata kufikiria hawawezi?
Matumizi ya laptop si kama udhania yo wewe, wanaojua umuhimu wake hiyo ndiyo maisha yake ya kila siku.
 
Akili Vijijini ni jamii duni Sana ambazo zimetofautia kidongo na hao kuku
Ndugu yangu, Dar siku moja nilikuwa napita nikaona kundi la watu. Kusogea nikakuta ni kibaka alikuwa ameuawa kwa kuiba ndoo inayowekea mnazi. likuwa pembeni, ni ndoo chafu na nina uhakika wewe ungekuwa nayo nyumbani ungeshaitupa jalalani. Makuzi yetu Tanzania yanatufanya tuwe watu makatili. Hivi zile fimbo alizokuwa yule mzee anampiga yule kijana na watu wengine wako pembeni wanasubiri ''zamu'' yao ya kupiga unaona ni jambo la kawaida? Wale wanaonyesha kabisa brain zao haziko sawa na zimeharibiwa tangu utoto.
 
Siwez tetea mwizi,hata ukiiba mihogo unatakiwa ufe
Vipi mafisadi wanao iba mabilioni na c.a.g kila mwaka ana tumia ghalama kubwa kubaini wapi kuna upotevu wa pesa ya mlipa Kodi hakuna mtu yeyote ana ajibishwa?
 
Mbona kariakoo mtu anaiba yebo yebo anachomwa moto live sembuse kijijini kijijin watu Wana Upendo na akili kubwa we mwenyew angalia laki mbili mjini mtu anakufa kwa 1000, 2000 au 750
Tanzania mtu naweza kuuawa hata kwa kutoiba kitu. Ni jamii ambayo watu wanaanza kufundishwa ukatili tangu utotoni. Unakuta shule au nyumbani watoto wanaanza kupigwa tangu wakiwa watoto eti ndiyo kufundisha nidhamu. Madhara yake yanaenda mbali.
 
Back
Top Bottom