Kwako Mzee Wangu Mohammed Said

Kwako Mzee Wangu Mohammed Said

Mimi nafikiri chaguzi hizo zinafanyika random tu bila kuaangalia udini , ukianza kufanya chaguzi kwa kubalance mambo ya udini apo ndipo tatzo litakapo anzia .serikali haina dini mkuu.
Min ...
Ikiwa serikali inahodhiwa 80% na waumini wa dini moja bado serikali hiyo itakuwa haina dini?
 
Loth...
Unaijua historia ya chama cha TANU kuanzia African Association 1929 hadi TANU 1954?

Ungeweza kuiweka TANU Dar-es-Salaam mbali na Waislam na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam waTanganyika)?

Hujui kwa nini ilikuwa vile?
nadhani unaelewa ilifika wakati siasa za kidini hazikukubaliwa tena katika tanzania. Viongozi wakuu walikemea udini usimee na kushamiri tanganyika/tanzania
 
Min...
Kipaumbele cha Waislam baada ya uhuru kupatikana ilikuwa elimu.

Mwaka wa 1962 kukaitishwa Muslim Congress agenda kuu kujenga shule na Chuo Kikuu kupitia EAMWS.

Shule zikaanza kujengwa na ilipofika mwaka wa 1968 EAMWS ikaanza ujenzi wa Chuo Kikuu.

Serikali ikapiga marufuku EAMWS na kuunda BAKWATA.

Huijui historia hii?
Najifunza🙏
 
nadhani unaelewa ilifika wakati siasa za kidini hazikukubaliwa tena katika tanzania. Viongozi wakuu walikemea udini usimee na kushamiri tanganyika/tanzania
Loth...
Soma historia ya uhuru ndiyo uje hapa ufanye mjadala.

Hawa ndiyo waasisi wa African Association: Kleist Abdallah Sykes, Mzee bin Sudi, Suleiman Majisu, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Cecil Matola, Raikes Kusi na Rawson.

Ushapata hata siku moja kuyasikia majina haya katika historia ya uhuru wa Tanganyika?
 
Peaky...
Ukiwa "mdini" unakusudia Uislam umesema kweli kabisa.

Naupenda sana Uislam.

Ukiwa kuniita "activist wa Islamic," unakusudia kushughulika na Waislam na Uislam hakika umesema kweli.

Kwani haya hayaruhisiwi mtu kufanya?

Hili la kupewa nafasi BAKWATA nakuomba unifafanulie nafasi ya BAKWATA nikafanye kazi gani?
Kama msemaji wa waislam.
Maana kila unachoandika lazima useme kuwa uislam unaonewa hapa Tanzania. Una faa kupewa nafasi ya kuwa Islamic defender pale bakwata.
 
Kama msemaji wa waislam.
Maana kila unachoandika lazima useme kuwa uislam unaonewa hapa Tanzania. Una faa kupewa nafasi ya kuwa Islamic defender pale bakwata.
Peaky...
Naandika Uislam unaonewa?

Hebu niwekee hapa hayo niliyoandika Uislam unaonewa.
 
Min...
Kipaumbele cha Waislam baada ya uhuru kupatikana ilikuwa elimu.

Mwaka wa 1962 kukaitishwa Muslim Congress agenda kuu kujenga shule na Chuo Kikuu kupitia EAMWS.

Shule zikaanza kujengwa na ilipofika mwaka wa 1968 EAMWS ikaanza ujenzi wa Chuo Kikuu.

Serikali ikapiga marufuku EAMWS na kuunda BAKWATA.

Huijui historia hii?
Hoja dhaifu sana hii. Kama serikali ilipiga marufuku mwaka 1968, ndio iliwaambia wasipate elimu?
Je wewe ulizaliwa na hiyo elimu yako au uliends shule?
 
Loth...
Soma historia ya uhuru ndiyo uje hapa ufanye mjadala.

Hawa ndiyo waasisi wa African Association: Kleist Abdallah Sykes, Mzee bin Sudi, Suleiman Majisu, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Cecil Matola, Raikes Kusi na Rawson.

Ushapata hata siku moja kuyasikia majina haya katika historia ya uhuru wa Tanganyika?
Hawakuwa na impact yoyote ndio maana hawapo.
 
20240515_084138.jpg
 
Hawakuwa na impact yoyote ndio maana hawapo.
Peaky...
Umewaona waliounda AA.
Je unawajua waliounda TAA Political Subcommittee 1950?:

Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Abdul Sykes, Dr. Vedasto Kyaruzi, Steven Mhando na John Rupia.
 
Nimekujibu hawakuwa na impact.
Walitoa tu mchango wao.
 
Mdukuzi,
Sijapatapo kuacha kuandika wakati wowote.

Sijapatapo kushikwa na hofu nikaacha kuandika.

Angalia hapa niko katika jina langu kwa sura na sauti.

Wewe ndiye muoga uliyeficha jina lako.

Niandikayo yote yako hapa yapitie na lete ushahidi kuwa mimi muoga.
Nakumbuka nimeanza kusoma nakala zako mwanzoni mwa 1990's. Hata ktk zile zilizo zikirudufiwa na typewriter mwisho ukiandika jina lako.
Naikumbuka "Mwinyi's Dilemma" nadhani ulikuwa ukimjibu Christopher Mtikila.
Nakushukuru si haba umetufungua macho si haba
 
Back
Top Bottom