Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Km unataka lockdown kaa Ndani Wewe na familia
Hivi vitumishi vyenye uhakika wa mwisho wa mwezi kero kweli
Kumbuka kuna watu lazima watoke Ndio wale
Sent using Jamii Forums mobile app
Kila siku anasema kwenye urais alisukumizwa tu kwamba haikua hiari yake. Unategemea mtu kama huyo ataweza ku deliver kwa standard za kueleweka kweli ?MODs tafadhalini msiufute huu uzi kama mlivyofuta ule wa siku tatu za sala ambao pia ulikuwa wa nia njema mno. Ni wazi kuwa wenye ujasiri wa kuandika nyuzi kama hizi kwa maslahi ya taifa ndani ya vitisho vilivyopo si wengi hivyo tafadhalini msiwe sehemu ya kuwanyamazisha.
Wanasema nani mwenye kumfunga paka kengele? Ni muhimu sasa bila ya kupoteza muda zaidi wala kumung'unya maneno, tumfunge paka huyu kengele vinginevyo twafa tukijiona.
Wenye ujasiri wamejitahidi kuweka jitihada binafsi kuwahami wananchi.
Heko baba askofu Niwemugizi. Pongezi anazoendelea kuzipata baba askofu huyu ni wazi kuwa hatua za namna hii ndiyo zilizokuwa zikihitajika kwa muda sasa.
Mh. Rais tafadhali tuachane na mambo ya uchumi na siasa. Ugonjwa huu utamaliza watu kwa uzembe wenu.
Gharama za kuwaweka watu manyumbani salama wasife kwa njaa (peke yake) tu ni ndogo mno na zitazidi kupanda kadri siku zinavyopita.
Kwa jinsi ambavyo umekuwa ukishughulikia suala hili tangia mwanzoni wewe kama mtendaji mkuu imetugharimu kweli kweli. Hatukuweza kuuzuia ugonjwa
huu kuingia nchini, na bado hatukumwona hata mmoja katika safu zako aliyewajibishwa au kuwajibika.
Umekuwa ukilishughulikia suala hili kuuzuia ugonjwa huu kusambaa na bado ugonjwa unasambaa. Hatujamwona hata mmoja katika safu yenu aliyewajibishwa au hata kuwajibika.
Kwa mwendelezo huu ni wazi kuwa hatunayo nia ya dhati (seriousness) wala hatuchukulii umuhimu wowote mafanikio
au kushindwa katika vita hivi nyeti ambavyo hakuna taifa hata moja duniani lenye watu makini waliojaribu kuidunisha.
Kwa sababu ugonjwa huu unaenda kutuathiri kimaisha moja kwa moja (sisi na wapendwa wetu), kwa vile wawakilishi wetu labda hawakufikishii maoni yetu vilivyo, na kwamba eti wewe huyaoni haya, tunaomba kutumia maneno yako wewe mwenyewe:
"Kwa jinsi ambavyo umekuwa ukiendesha vita vya ugonjwa huu, tafadhali sasa NO!
Tunakupenda sana mheshimiwa. Lakini mheshimiwa kwenye hili la Corona, big No!
Kwa nini angalau Dar na Zanzibar haziko locked down? Mh. rais, Big No! Tumevumilia kweli kweli hadi tumelazimika kukupa ukweli huu. Mkuu big No!"
Cha kufanya kinafahamika. Kenya Rwanda na Uganda walio kama sisi wamefanya nini na sasa wanaudhibiti juu ya ugonjwa huu na karibu wanaanza kurejea kwenye shughuli zao za kawaida?
Please No!
Gazeti nzima lakini mapovu matupu au ni seme pumba tupu! Si ujifungie wewe mwenyewe au kama unaona Watz hawachukui hatua kwanini usihame nchi ili ukaishi milele. USA wako lockdown lakini mbona bado wanaambukizana zaidi ya mwezi sasa?
Hao wakenya walijaribu lockdown ikawashinda wakaamua kubadirisha kuwa curfew ya kuanzia saa moja jionj hadi SAA 11 asubuhi sasa wewe unaona hiyo ni lockdown? Kwani huna akili ya kujilinda wewe na familia yako mpaka usimamiwe na serikali.
Kwa taarifa yako USA sasa wametoka barabarani hawataki tena lockdown. Namalizia kwa kukueleza tuondolee umbumbumbu wako hapa!
Unapoamua kuchukua hatua zako usianze kujilinganisha na watu wengine, ikiwa china na ulaya wana ubora katika kila kitu iweje vifo viwe vingi kwao kuliko Africa ambako huduma ni duni. Ulishajiuliza kwa nini maskini anaweza asikanyage hospitali kwa miaka kumi, lakini tajiri kila wiki yupo kwa daktari...Ulaya na China walikuwa hawana hivi vitu tena vyenye quality ya juu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mleta uzi unapodai lockdowns vile vile dai na mikakati ya kiuchumi kuwasaidia hao mnaotaka wafungiwe ndani!!
Msipokuwa makini njaa, sonona n.k vitaua watu wengi zaidi ya #Covid-19
Kwan mmesahau kauli ya Mh Ummy Mwalimu kabla hata ugonjw hujaingia alivyosema?
" Huu ugonjwa ni hatar sana laiti ukiingia ktk nchi yetu hatuna uwezo wa kukabliana nao" mwisho wa kunukuu.
Tujiandae kwa lolote.
Sent using Jamii Forums mobile app
Pole pole na PaulNikikumbuka kejeli za mkuu fulani na Sema bora nikae kimyA
Mkuu naona akili na zimeanza kukujia na wewe.Nikikumbuka kejeli za mkuu fulani na Sema bora nikae kimyA
Akili mbovu kama hizi ndio chanzo cha usambaaji wa huu ugonjwa. Uchumi na maisha ya Warundi ni ya chini kuliko sisi,lakini wameimpose lockdown!Km unataka lockdown kaa Ndani Wewe na familia
Hivi vitumishi vyenye uhakika wa mwisho wa mwezi kero kweli
Kumbuka kuna watu lazima watoke Ndio wale
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tutakapofikia hatua ya lockdown usisahau kuja na bandiko jingine kusifia... na ndiko tunakoelekea maana hakuna namna hata hao Uganda na Rwanda hawakupenda ila ilibidi...
Mkuu sisi siyo wa kwanza. Wenzetu wapo hapa hapa si mbali wala.
Kenya, Uganda na Rwanda - wenzetu katika East Africa. Wengi uchumi na raslimali zao mbovu kuliko sisi.
Huu ugonjwa unaouwa. Kulikuwa na uzi huu muda:
Hoja za wanaoona lockdown haifai ni zipi? Tuelimishane - JamiiForums
Hakukuwa na hoja yoyote nzito ya kupinga hili. Kama unayo tupe.
Kwani huko USA unadhani hakuna wajinga kama wew ? Kwahiyo U.S.A wajinga wakiandamana basi na hapo Lumumba uvccm buku7 mnawafuata nyumbu wenzenu kutoka nje kuwa Corona haiuwi.Gazeti nzima lakini mapovu matupu au ni seme pumba tupu! Si ujifungie wewe mwenyewe au kama unaona Watz hawachukui hatua kwanini usihame nchi ili ukaishi milele. USA wako lockdown lakini mbona bado wanaambukizana zaidi ya mwezi sasa?
Hao wakenya walijaribu lockdown ikawashinda wakaamua kubadirisha kuwa curfew ya kuanzia saa moja jionj hadi SAA 11 asubuhi sasa wewe unaona hiyo ni lockdown? Kwani huna akili ya kujilinda wewe na familia yako mpaka usimamiwe na serikali.
Kwa taarifa yako USA sasa wametoka barabarani hawataki tena lockdown. Namalizia kwa kukueleza tuondolee umbumbumbu wako hapa!
Mimi amenikera sitaki hata kusikia akiongeaBaada ya Janga la Corona JPM atadharauliwa sana na Marais wenzie wa Africa ambao walikua wanamuona JEMBE kumbe ni Kijiko.
Sent using Jamii Forums mobile app