Kwako Rais Magufuli sasa pasipo na kupepesa maneno: Kwa unavyoshughulika na Corona sasa - NO!

"Eti gharama ya kuwalisha watu wakiwa majumbani mwao ni ndogo mno".
Hivi wewe unajua gharama za kuwalisha watu milioni 60.
Asubuhi, mchana na usiku?
Unajua lockdown down itakaa siku ngapi?.
JE corona isipo isha Ina maana watu watakaa ndani mwaka mzima.
Utaweza kuwalisha?

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"

Unapenda kula sana eeh?

Soma bandiko kuelewa. Umesoma vizuri kilicho andikwa? Kama hukuona pako hivi:

"Gharama za kuwaweka watu manyumbani salama wasife kwa njaa (peke yake) tu ni ndogo mno na zitazidi kupanda kadri siku zinavyopita."

Ni kuonyesha umbumbu kuliko pitiliza kujaribu kunukuu andiko aliloandika mtu kindivyo sivyo kwa malengo au maslahi yako binafsi.

Nukuu yako ya kimbumbumbu uliitoa wapi mkuu?
 
Uzuri wake muh Rais hajamuzuia mtu yeyote kujiweka karantini, wanaoamini kuwa maamuzi yaliyofanywa na muhe Rais hayako sahihi wanahaki ya kujiweka karantini wenyewe kwa uhuru wao.

Na sisi wengine tunaokubaliana na maamuzi ya Rais ya kumtegemea Mungu katika janga hili la corona tuachwe tuendelee na uhuru wetu na haki yetu ya kuamini kuwa muhe Rais yuko sahihi katika hili.

Nakama Mungu atatuacha tuangamie kwa corona kwa sababu ya kumtegemea yeye tutakuwa na hoja ya kumuhoji ni kwa nini alituacha tuangamizwe na corona wakati ametuahidi kutuponya na kutulinda tutakapo mugeukia na kumulilia yeye?.
 
Mr. Wakati unayazungumza hayo uneangalia na upande wako ambao unaweza kukaa ndani miezi kadhaa ukitumia kile ulichonacho ndani.Wakati unayazungumza haya,kuna watu wanaomba hii lock down isitokee ili watu wasave familia zao kwa kurudi na chochote kitu.

Mhe.Raisi atasikiliza nani aache nani?.hata kenya watu walilazimika kutoka kwasababu kuliko kufia ndani akiwa na nguvu anaona bora atoke kutafuta chochote.Msipende kulaumu tu bila kufikiri.unadhani yeye haoni hali ilivyo?shida ni kuwa anaangalia pia ni familia ngapi zitakuwa hatarini kwa kukosa chakula kwasababu ya lockdown.

Acheni hizo lawama za kijinga jaribuni kufikiria familia ambazo pia zipo hatarini kwa kupato.Kuanzia bodaboda na wale wote waliojiajiri ambao wanategemea kipato kinachotokana na nguvu zao za siku.Hiyo NO yako iambie familia yako wajifungia hujalazimishwa kutoka.

Mkijifungia familia nzima ndani mtakuwa salama hivyo deal na familia yako ijifungie.Si ajabu unazungumza NO zako kumbe kwenu mna fensi mlishaamua kujitenga na majirani hata kabla ugonjwa haujaingia

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu tatizo letu watanzania ikiwamo wewe ni kutokusoma kujua nini tayari kimeshaongelewa. Matokeo yake yanakuwa mtu unakuja sasa kama umetokea sayari nyingine.

Mkuu uliwahi kuyaona haya:

IMG_20200416_125352_093.jpg

Hoja za wanaoona lockdown haifai ni zipi? Tuelimishane - JamiiForums

Au ndiyo unayaona leo mkuu?

Hatuwezi kujipanga kama taifa watu wasife njaa tuutokomeze huu ugonjwa?

Mbona Kenya, Uganda na Rwanda wanaweza hali hapo wengine hohehahe kuliko sisi?
 
Mkuu hata kama imeenea nchi nzima haijaenea kwa watu wote.

Uzembe wa viongozi wetu ulituletea Corona. Uzembe wao unaacha ugonjwa huu kusambaa. Kadri watu watakavyoambukizwa ndivyo hivyo hivyo na idadi ya vifo vitaongezeka.

Ugonjwa huu hautaondoka wenyewe:

Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu - JamiiForums
Dunia nzima wanazungumzia corona na kuita janga na tunaona huko ulaya wakipukutika ila wewe unasema Tanzania ugonjwa umeingia kwa sababu ya uzembe! Wakati nasikia Russia aliwahi mapema kufunga mipaka yake ila hadi sasa washapukutika watu mia tatu na hali inazidi. Sioni tofauti ya aliyefanya uzembe na siyefanya uzembe. Na kama ni uzembe basi huoni kuwa tulitakiwa afrika tuwe tumepukutika zaidi ya Marekani au Italy hadi sasa?
 
Mkuu haipo sababu sana ya kutafuta mchawi na kuacha jambo nyeti kwa sasa la.kuzuia kusambaa zaidi kwa maambukizi. Hata hivyo, historia ya ugonjwa kuingia inajulikana na hata mwendelezo wa unavyosambaa sasa hivi ninavyoandika hapa inajulikana.

Miito mingapi kutaka ndege zisije kwetu kabla ya ugonjwa kuingia ilikuwapo? Hujasikia waliokuwa wamekataa kufunga anga au kuuzuia ndege tokea china kuja? Hukusikia waliokuwa wakiongelea utalii?

Mada kama hizi je nazo hukuziona?

Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu - JamiiForums

Kwamba ulaya au marekani ugonjwa uliingia hakuhalalishi kutokuwepo uzembe uliopelekea ugonjwa huu kuingia kwetu.

Kumbuka tulisikia na kuona ugonjwa ukiingia mataifa mengine baada ya China yakiwamo ulaya na marekani mapema mno kabla ya ugonjwa kutufikia. Tulikuwa na muda wote wa kujifunza na kuchukua hatua na bado hatukufanya hivyo.

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi. Tumejifunza nini au kwa nani kuhusu huu ugonjwa? Nini tumefanya kufuatia kujifunza huko?

Labda niwe wazi zaidi hili la sala tumejifunza kwa nani?

Tumeshindwa kujifunza hili la hata tokea kwa baba askofu wetu Niwemugizi hapa hapa nchini.

Kama haya yote ndiyo unayasikia sasa utakuwa umewasili tokea sayari nyingine. Haitakuwa bure mkuu.
 
Uzuri wake muh Rais hajamuzuia mtu yeyote kujiweka karantini, wanaoamini kuwa maamuzi yaliyofanywa na muhe Rais hayako sahihi wanahaki ya kujiweka karantini wenyewe kwa uhuru wao.

Na sisi wengine tunaokubaliana na maamuzi ya Rais ya kumtegemea Mungu katika janga hili la corona tuachwe tuendelee na uhuru wetu na haki yetu ya kuamini kuwa muhe Rais yuko sahihi katika hili.

Nakama Mungu atatuacha tuangamie kwa corona kwa sababu ya kumtegemea yeye tutakuwa na hoja ya kumuhoji ni kwa nini alituacha tuangamizwe na corona wakati ametuahidi kutuponya na kutulinda tutakapo mugeukia na kumulilia yeye?.

Mkuu uliwahi kuyaona haya:

IMG_20200419_155725_378.jpg

Uhuru upi usiokuwapo unaouongelea ambao mh. rais kautoa wa kujiweka karantini isiyokuwapo?

Ni kweli hatuelewi au ni mzaha?

Hoja za wanaoona lockdown haifai ni zipi? Tuelimishane - JamiiForums

Hoja zenu ziko wapi?
 
MODs tafadhalini msiufute huu uzi kama mlivyofuta ule wa siku tatu za sala ambao pia ulikuwa wa nia njema mno. Ni wazi kuwa wenye ujasiri wa kuandika nyuzi kama hizi kwa maslahi ya taifa ndani ya vitisho vilivyopo si wengi hivyo tafadhalini msiwe sehemu ya kuwanyamazisha.

Wanasema nani mwenye kumfunga paka kengele? Ni muhimu sasa bila ya kupoteza muda zaidi wala kumung'unya maneno, tumfunge paka huyu kengele vinginevyo twafa tukijiona.

Wenye ujasiri wamejitahidi kuweka jitihada binafsi kuwahami wananchi.

Heko baba askofu Niwemugizi. Pongezi anazoendelea kuzipata baba askofu huyu ni wazi kuwa hatua za namna hii ndizo zilizokuwa zikihitajika kwa muda sasa.

Mh. Rais tafadhali tuachane na mambo ya uchumi na siasa. Ugonjwa huu utamaliza watu kwa uzembe wenu.

Gharama za kuwaweka watu manyumbani salama wasife kwa njaa (peke yake) tu ni ndogo mno na zitazidi kupanda kadri siku zinavyopita.

Kwa jinsi ambavyo umekuwa ukishughulikia suala hili tangia mwanzoni wewe kama mtendaji mkuu imetugharimu kweli kweli. Hatukuweza kuuzuia ugonjwa
huu kuingia nchini, na bado hatukumwona hata mmoja katika safu zako aliyewajibishwa au kuwajibika.

Umekuwa ukilishughulikia suala hili kuuzuia ugonjwa huu kusambaa na bado ugonjwa unasambaa. Hatujamwona hata mmoja katika safu yenu aliyewajibishwa au hata kuwajibika.

Kwa mwendelezo huu ni wazi kuwa hatunayo nia ya dhati (seriousness) wala hatuchukulii umuhimu wowote mafanikio
au kushindwa katika vita hivi nyeti ambavyo hakuna taifa hata moja duniani lenye watu makini waliojaribu kuidunisha.

Kwa sababu ugonjwa huu unaenda kutuathiri kimaisha moja kwa moja (sisi na wapendwa wetu), kwa vile wawakilishi wetu labda hawakufikishii maoni yetu vilivyo, na kwamba eti wewe huyaoni haya, tunaomba kutumia maneno yako wewe mwenyewe:

"Kwa jinsi ambavyo umekuwa ukiendesha vita vya ugonjwa huu, tafadhali sasa NO!

Tunakupenda sana mheshimiwa. Lakini mheshimiwa kwenye hili la Corona, big No!

Kwa nini angalau Dar na Zanzibar haziko locked down? Mh. rais, Big No! Tumevumilia kweli kweli hadi tumelazimika kukupa ukweli huu. Mkuu big No!"

Cha kufanya kinafahamika. Kenya Rwanda na Uganda walio kama sisi wamefanya nini na sasa wanaudhibiti juu ya ugonjwa huu na karibu wanaanza kurejea kwenye shughuli zao za kawaida?

Please, Big NO!

Unakosea kumlaumu Rais kwa hili. Mpaka sasa msimamo na maamuzi yake ni sahihi kabisa na ni ya ki - Mungu

Hakuna mambo ya Lockdown hapa nchini kwetu.

å Kwa kazi ambazo hazihusishi kusanyiko la watu kuanzia 10 na kuendelea, ziendelee kufanyika kama kawaida bila kukosa. Watu wachape kazi!!

å Kila mtu achukue tahadhari zote za kiafya kama zinavyotolewa na wataalamu was afya i.e kunawa mikono, kivaa barakoa, kutotoka ndani na kuepuka safari zisizokuwa na ulazima

å Above all, 2Mambo ya Nyakati.7:14 inatuhusu sote. Suluhu ya haya mambo ni kuacha Dhambi, kujinyenyekesha mbele za Mungu na kuomba toba kwa ajili ya taifa na nchi yetu

Chanzo cha haya yote i.e tauni (corona), mikosi, laana, umasikini, magonjwa ni DHAMBI ama kumuasi Mungu

Tunapoghairi njia zetu ovu na kmgeukia Mungu, atatuponya na kuiponya nchi yetu

Soma pia ISAYA 59:1-2. Hii ndiyo ahadi ya Mungu. Tukimuona hawezi kutusaidia na kukakamaza shingo zetu, hakika tutakufa wote
 
Mkuu haipo hata nchi moja yenye mtazamo kama huu. Hilo tu halitoshi kukupa homa? Mbona majambazi hatuyakabidhi kwa Mungu?

Zipo nchi zilizofanikiwa kuudhibiti ugonjwa huu kwa jitihada thabiti wakitumia raslimali zao na wengine wao hao wala hawana raslimali nyingi kama sisi. Hili nalo halikupi matumaini? Mbona majambazi tunapambana nayo kwa kutumia raslimali zetu?

Umemsikia au kumfuatilia au kumwelewa baba askofu Niwemugizi?

Mkuu tupo tunaompenda sana mtukufu rais lakini kwa hili aah aaah, kwa hakika hawezi kukwepa lawama za moja kwa moja kwa kutokuwajibika.

Nchi hii haina dini. Wananchi wanazao na wengine hawana. Kimsingi hatuna hata haja ya kujuzana dini hizo. Kumbuka dini hizo bado zinakinzana zenyewe. Twalikabidhi hili kwa Mungu kwa dini ipi?

Mkuu huoni kuwa suala hili la msingi mno tunalifanyia mzaha mkubwa?
 
Hii issue kheri upambane wewe na familia yako tu. Kama una uwezo wa chakula na vitu vingine fanya hivyo, protect your family tu.
Wengine washaelimishwa na bado wanasubiri masia atakaeiponya nchi baada ya siku tatu za maombi, then waache waamini hivyo.

Mkuu ingekuwa TB au ukimwi self protection ingewezekana. Lakini huu, kwa kasi ya maambukizi yake, ugeni wake (nani ajuaye 100%?), kasi yake ya kuuwa, kwamba siyo airborne per se, nk nk.

Mkuu mbona self protection is actually queueing silently waiting for ones' turn?

2367592_IMG_20200413_163522.jpg
 
MODs tafadhalini msiufute huu uzi kama mlivyofuta ule wa siku tatu za sala ambao pia ulikuwa wa nia njema mno. Ni wazi kuwa wenye ujasiri wa kuandika nyuzi kama hizi kwa maslahi ya taifa ndani ya vitisho vilivyopo si wengi, hivyo tafadhalini msiwe sehemu ya kuwanyamazisha.

Wanasema nani mwenye kumfunga paka kengele? Ni muhimu sasa bila ya kupoteza muda zaidi wala kumung'unya maneno, tumfunge paka huyu kengele vinginevyo twafa tukijiona.

Wenye ujasiri wamejitahidi kuweka jitihada binafsi kuwahami wananchi.

Heko baba askofu Niwemugizi. Pongezi anazoendelea kuzipata baba askofu huyu ni wazi kuwa hatua za namna hii ndizo zilizokuwa zikihitajika kwa muda sasa.

Mh. Rais tafadhali tuachane na mambo ya uchumi na siasa. Ugonjwa huu utamaliza watu kwa uzembe wenu.

Gharama za kuwaweka watu manyumbani salama wasife kwa njaa (peke yake) tu ni ndogo mno na zitazidi kupanda kadri siku zinavyopita.

Kwa jinsi ambavyo umekuwa ukishughulikia suala hili tangia mwanzoni wewe kama mtendaji mkuu imetugharimu kweli kweli. Hatukuweza kuuzuia ugonjwa
huu kuingia nchini, na bado hatukumwona hata mmoja katika safu zako aliyewajibishwa au kuwajibika.

Umekuwa ukilishughulikia suala hili kuuzuia ugonjwa huu kusambaa na bado ugonjwa unasambaa. Hatujamwona hata mmoja katika safu yenu aliyewajibishwa au hata kuwajibika.

Kwa mwendelezo huu ni wazi kuwa hatunayo nia ya dhati (seriousness) wala hatuchukulii umuhimu wowote mafanikio
au kushindwa katika vita hivi nyeti ambavyo hakuna taifa hata moja duniani lenye watu makini waliojaribu kuidunisha.

Kwa sababu ugonjwa huu unaenda kutuathiri kimaisha moja kwa moja (sisi na wapendwa wetu), kwa vile wawakilishi wetu labda hawakufikishii maoni yetu vilivyo, na kwamba eti wewe huyaoni haya, tunaomba kutumia maneno yako wewe mwenyewe:

"Kwa jinsi ambavyo umekuwa ukiendesha vita vya ugonjwa huu, tafadhali sasa NO!

Tunakupenda sana mheshimiwa. Lakini mheshimiwa kwenye hili la Corona, big No!

Kwa nini angalau Dar na Zanzibar haziko locked down? Mh. rais, Big No! Tumevumilia kweli kweli hadi tumelazimika kukupa ukweli huu. Mkuu big No!"

Cha kufanya kinafahamika. Kenya Rwanda na Uganda walio kama sisi wamefanya nini na sasa wanaudhibiti juu ya ugonjwa huu na karibu wanaanza kurejea kwenye shughuli zao za kawaida?

Please, Big NO!
Ushauri wangu kwa kuwa umekwisha kuenea, serkali isijikite kutoa elimu ya kujikinga tu bali jinsi ya kuhudumia wagonjwa majumbani
 
Mkuu haipo hata nchi moja yenye mtazamo kama huu. Hilo tu halitoshi kukupa homa? Mbona majambazi hatuyakabidhi kwa Mungu?

Zipo nchi zilizofanikiwa kuudhibiti ugonjwa huu kwa jitihada thabiti wakitumia raslimali zao na wengine hawana. Hili nalo halikupi matumaini? Mbona majambazi tunapambana nayo kwa kutumia raslimali zetu?

Umemsikia au kumfuatilia au kumwelewa baba askofu Niwemugizi?

Mkuu tupo tunaompenda sana mtukufu rais lakini kwa hili aah aaah, kwa hakika hawezi kukwepa lawama za moja kwa moja kwa kutokuwajibika.

Nchi hii haina dini. Wananchi wanazao na wengine hawana. Kimsingi hatuna hata haja ya kujuzana dini hizo. Kumbuka dini hizo bado zinakinzana zenyewe. Twalikabidhi hili kwa Mungu kwa dini ipi?

Mkuu huoni kuwa suala hili la msingi mno tunalifanyia mzaha mkubwa?

Kabidhi maombi yako kwa Mungu wa dini unayomwabudu siku zote

Jambazi mtu hawezi kuathiri mfumo wa uendeshaji wa nchi yote. Jambazi anashughulikiwa na watu maalumu wenye jukumu hill

Tauni - Corona huyu ni kitu kingine kabisa. Binadamu kwa NGUVU na AKILI na MAARIFA yake hawezi kushughulika naye na kumshinda huyu adui

Njia pekee ya kumshinda huyu adui, huyu jambazi Corona, ni intervention ya Mungu mwenyewe aliyeumba viumbe wote, mwenye nguvu zote.

Hili limeachiliwa kwa kusudi maalumu na Mungu mwenyewe ili watu wapate kuoona ukuu na utukufu wa Mungu.

Limeachiliwa ili kutenga NGANO na MAKAPI. Ngano ni wale wanaomwabudu Mungu wa PEKEE, na wa KWELI ktk YESU KRISTO. Walio na miungu yao ya uongo, hawatabaki Salama, Corona itawapitia tu na kuwaua kabisa!!

Tazama huko ktk dunia ya kwanza USA, China, UK, Germany, Italy, France, Spain nk ambao ni wababe wenye kiburi cha nguvu za kiuchumi na kijeshi na kiteknolojia, kwa hili wamekwama, ubabe hauja wasaidia kitu. Ndiko wanakokufa kama nzige pamoja na kuchukua hatua unazozipendekeza wewe!!

The choice is whether to say I go to YEHOVA or to the Devil!+)
 
Ushauri wangu kwa kuwa umekwisha kuenea, serkali isijikite kutoa elimu ya kujikinga tu bali jinsi ya kuhudumia wagonjwa majumbani

Mkuu elimu ipi serikali iliyojikita kwa kujikinga mle feri, kwenye masoko, ibada, kwenye usafiri wa umma, nk.

Siyo kuwa tunatwanga maji kwenye kinu?

Muda huu si wa elimu tena. Sasa hivi ni maamuzi magumu. Tumejifikisha hapa mwendo sasa ni wa Rwanda, Uganda au Kenya in that order.

Mkuu anaweza bado kuendelea kutouona ukweli huo.

Kwa hivyo wala asijidanye kwa sasa tumechoka na waziwazi tutamfahamisha kuwa kwa maamuzi yake yasiyo na mashiko kama hayo hatumwuungi mkono.
 
Dar inatakiwa siku nyingi iwe lockdown na Zanzibar lkn hawataki au wanaona wakisema itakuwa aibu kwa sababu walishasema upinzani kabla
Mikusanyiko kama ibada na mambo mengine vilitakiwa visiwepo lkn pia hawataki wanatafuta kura makanisani ugonjwa na wenyewe una wamaliza waumini hii ni vita nyingine
Amebaki Mungu tu kuwatetea na kuwapigania wadanganyika
 
Mkuu haipo sababu sana ya kutafuta mchawi na kuacha jambo nyeti kwa sasa la.kuzuia kusambaa zaidi kwa maambukizi. Hata hivyo, historia ya ugonjwa kuingia inajulikana na hata mwendelezo wa unavyosambaa sasa hivi ninavyoandika hapa inajulikana.

Miito mingapi kutaka ndege zisije kwetu kabla ya ugonjwa kuingia ilikuwapo? Hujasikia waliokuwa wamekataa kufunga anga au kuuzuia ndege tokea china kuja? Hukusikia waliokuwa wakiongelea utalii?

Mada kama hizi je nazo hukuziona?

Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu - JamiiForums

Kwamba ulaya au marekani ugonjwa uliingia hakuhalalishi kutokuwepo uzembe uliopelekea ugonjwa huu kuingia kwetu.

Kumbuka tulisikia na kuona ugonjwa ukiingia mataifa mengine baada ya China yakiwamo ulaya na marekani mapema mno kabla ya ugonjwa kutufikia. Tulikuwa na muda wote wa kujifunza na kuchukua hatua na bado hatukufanya hivyo.

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi. Tumejifunza nini au kwa nani kuhusu huu ugonjwa? Nini tumefanya kufuatia kujifunza huko?

Labda niwe wazi zaidi hili la sala tumejifunza kwa nani?

Tumeshindwa kujifunza hili la hata tokea kwa baba askofu wetu Niwemugizi hapa hapa nchini.

Kama haya yote ndiyo unayasikia sasa utakuwa umewasili tokea sayari nyingine. Haitakuwa bure mkuu.
Nimekwambia huko ulaya nchi nyingi watu wanapukutika haijarishi aliyefanya uzembe au asiyefanya ila wewe bado unashikilia habari za uzembe na huko Russia watu 300 washapukutika na wakati wao walifunga mapema tu mipaka yake.
 
Back
Top Bottom